BRAZIL MABINGWA KOMBE LA MABARA: YAWAADHIBU MABINGWA WA DUNIA SPAIN
BRAZIL YALIBEBA KOMBE KWA MARA YA TATU MFULULIZO
Timu ya taifa ya Brazil imeingia katika historia mpya baada ya kufanikiwa kulibeba kombe la Mabara kwa mara ya 3 mfululizo na hii ni baada ya kuwafunga bila huruma mabingwa wa Ulaya na Dunia timu ya Taifa ya Spain magoli 3-0 .
Baada ya Kulichukua kombe hilo mwaka 2005 Kule Ujerumani wakarudia tena kulichukua mwaka 2009 Nchini Afrika Kusini na sasa katika Ardhi ya nyumbani wameweza kulinyakua kwa kuwafunga Spain katika Fainali.
Katika usiku ambao Spain hawatausahau wamejikuta wakifungwa magoli 3-0 na Brazil na kufuta zile ndoto zao za kuchukua kombe la mabara kwa mara ya Kwanza katika Historia na ndoto za kuchukua kombe ambalo limebaki kwa Spain kulichukua baada ya kushinda kombe la Dunia na Lile la Ulaya.
Magoli ya Brazil yalifungwa na Fred dakika ya 2 na Dakika ya 48 Wakati Neymar naye alikua kati ya wafungaji akifunga dakika chache kabla ya mapumziko.
Katika Mchezo huo ambao ni dhahiri kuwa Spain walizidiwa kila Idara ulishuhudia pia beki wa Spain Sergio Ramos akikosa mkwaju wa penati baada ya Jesus Nervas kuangushwa katika eneo la hatari na beki wa Brazil Marcelo.
Gerald Pique wa Spain alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji Neymar aliyekua akielekea kufunga.
Brazil walimiliki mpira kwa kiwango kikubwa na kuwabana vilivyo mabingwa hao wa Dunia na Ulaya huku kazi nzuri sana ikifanywa na Luis Gustavo, David Luiz na Marcelo ambao mara nyingi walitibua mipango yote iliyofanywa na Viungo wa Spain kama Xavi, Iniesta na Pedro.
Hali ya uwanja wa Maracana ilikua ya kuvutia na ilionekana kabisa Brazil walikua wamejiandaa kwa sherehe hizo huku kocha wa Spain Vicente Del Bosque akisifu kikosi cha Brazil kwa kandanda safi walilocheza usiku huo.
Kwa Matokeo haya ile rekodi ya Spain ya kucheza mechi 26 mfululizo bila kufungwa ilikomeshwa rasmi na ilikua ni mara ya kwanza timu hizo zimekutana Tangu mwaka 1999.
Je Utawala wa Spain ndo umeisha? Je Brazil ndo wamerudi katika utawala wao? Haya ni maswali wanayojiuliza Wapenda Soka kwa sasa.
MABINGWA BRAZIL |

No comments