MIWANI PANA YA EDO ~ KUELEKEA FAINALI YA KOMBE LA MABARA: BRAZIL vs SPAIN
NI MIAKA 23 SPAIN HAIJAMFUNGA BRAZIL
Katika Miaka 23 iliyopita Hispania na Brazil zimekutana mara moja tu ambao ni mwaka 1999 mechi ya kirafiki ambayo iliisha kwa sare ya bila kufungana kipindi hicho ambacho Brazil ilikua namba moja duniani kwa soka safi na ubora.
Kuanzia miaka ya 2000 Utawala mpya wa Soka uliingia hasa kwa nchi iliyofanikiwa kutengeneza vipaji vya hali ya Juu. Naizungumzia Hipania au Spain ambao wengi wetu hupenda kuiita.
Spain imeweza kuchukua makombe yote ambayo imeshiriki isipokua kombe la mabara ambalo sasa wako mguu ndani mguu nje kulipata watakapokutana na Brazil ambao ni mabingwa wa kihistoria wa kombe hilo.
BRAZIL
Baada ya kupoteza mwelekeo kwa miaka mingi hivi sasa Brazil imerudi na kizazi kipya chenye kila aina ya ujanja katika soka. Ukiacha wale walioitwa kuunda kikosi kinachoshiriki mashindano hayo lakini wapo wengine wengi ambao hawakupata nafasi hiyo.
Katika kikosi cha sasa utakutana na Vijana wadogo wenye uchu wa mafanikio yaliyofikiwa na nyota wengine wa nchi hiyo. Nawazungumzia Neymar,Oscar,David Luiz,Fred, Lucas Moura, Paulinho na wengine wengi.
Brazil wameingia fainali kwa kuisukumiza Uruguay bao 2-1 katika hatua ya Nusu fainali. Katika Michezo 8 Iliyopita ya Timu ya Brazil wameweza kufunga magoli 22 na hii inanionyesha jamaa wako vizuri katika kufunga.
SPAIN
Spain nao hakuna aliyeshangaa kuwaona Fainali japokua wengi wanaamini ni bahati tu safari hii imewapeleka fainali baada ya kuwatoa Italia katika nusu fainali kwa mikwaju ya penati 7-6. Wana kikosi bora kabisa chenye uzoefu na kucheza soka safi la kuvutia na licha ya wale tunaowaona katika Fainali hizo lakini wana lundo la wachezaji wamekosa nafasi hiyo nadhani ndo timu iliyobarikiwa kua na kizazi kitakachodumu kwa miaka kadhaa ijayo wakiwa katika ubora ule ule.
Kizazi cha sasa kinaundwa na wakongwe waliopata kila aina ya mafanikio Xav,Iniesta,Torres, Casillas, Villa,Silva na wengineo.
Spain wanatakiwa kuwafunga Brazil leo ili kuuthibitishia ulimwengu kama wao ndo bora kuliko timu yoyote lakini ikumbukwe Brazil hawajawahi kufungwa nyumbani kwao tangu mwaka 1975 so haitakua kazi nyepesi.
Spain mpaka kufikia Fainali hii hawajafungwa goli lolote katika michezo 8 waliyocheza ya mashindano yoyote.
Kwangu mimi Edo na Wapenda soka duniani leo tunaenda kushuhudia pambano safi na la kuvutia katika dimba la Maracana japokua mpira utaanza muda mbaya lakini hupaswi kukosa mechi hii itakayoanza saa 7 usiku saa za Afrika Mashariki.
Hivyo Basi ukiangalia kwa haraka hapa Utaona Brazil wako juu ya Spain kwa rekodi lakini Tukirudi uwanjani hilo halipo kwani Spain hii ya sasa hakuna asiyeifahamu ubora wake chamsingi tusubiri Muda ufike tuangalie soka safi kutoka kwa miamba hii
.... Nipate facebook Edo Daniel Chibo: twitter @edodaniel1; Email. wapendasoka2gmail.com au tembelea Ukurasa wa wapenda soka katika mtandao wa Facebook.
BRAZIL VS SPAIN |

MAMBO USIYOYAJUA KATI YA TIMU HIZI
- Katika mechi 8 zilizokutanisha miamba hii ya soka, Brazil imeshinda 4 wakati Spain ikishinda mechi 2 na mechi 2 ziliisha kwa sare na ushindi pekee walioupata Spain katika mashindano dhidi ya Brazil ilikua mwaka 1934 katika Fainali za kombe la Dunia.
- Brazil iliwahi kuifunga Spain 6-1 katika fainali ya kombe la Dunia mwaka 1950.
BRAZIL
- Brazil wamefunga magoli mawili au zaidi katika mechi zao nane zilizopita wakifungajumla ya magoli 22. Wamefunga pia katika mechi 12 mfululizo za mashindano ya Kombe la Mabara wakishinda mechi 11 kati ya hizo 12
- Ushindi katika fainali hii utaifanya Brazil kushinda kwa mara ya tatu mfululizo kombe hili la Mabara baada ya kushinda 2005 na 2009 na kuwaacha Ufaransa ambao walishinda mara mbili mfululizo 2001 na 2003.
- Katika mechi zote nne walizocheza Brazil wameshinda katika michuano ya mwaka huu ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kushinda mechi mfululizo mara ya mwisho waliwahi kushinda mechi 10 mfululizo mwaka 2009.
- Brazil hawako vizuri katika penati nadhani wataliepuka hilo leo kwani mara ya mwisho ushindi ulipoamuliwa kwa penati walipoteza penati zote dhidi ya Paraguay mwaka 2011 katika Robo fainali ya kombe la Bara la Amerika ya Kusini(Copa America) wakipoteza kwa 2-0 huku wachezaji wake wakikosa penati zote.
HISPANIA (SPAIN)
- Spain wamefunga katika mechi 15 mfululizo walizocheza isipokua mechi dhidi ya Italia ambayo iliisha kwa droo ya 0-0.
- Spain haijafungwa katika mechi 29 za mashindano wakishinda mechi 24 na kutoka sare mechi 5 rekodi ambayo inaendelea na mara ya mwisho kufungwa katika mashindano ilikua katika kombe la Dunia mwaka 2010 dhidi ya Uswisi walifungwa 1-0.
- Spain pia hawajafungwa katika michezo 26 waliyocheza ikiwemo ya kirafiki wakishinda michezo 20 na kutoka sare michezo 6. Mara ya mwisho kufungwa ilikua mwaka 2011 dhidi ya England.
- Kwa Upande wa mikwaju ya Penati jamaa wako vizuri sana kwani mara zot 3 walizoingia hatua ya penati walishinda na zaidi ya yote wamefunga penati 15 kati ya 17 walizopiga.
REKODI YA BRAZIL DHIDI YA SPAIN
- Mwaka 1934: Kombe la Dunia, Brazil ilipoteza 3-1
- Mwaka 1950: Kombe la Dunia, Brazil ilishinda 6-1
- Mwaka 1962: Kombe la Dunia, Brazil ilishinda 2-1
- Mwaka 1978: Kombe la Dunia, Zilitoka sare 0-0
- Mwaka 1981: Mechi ya kirafiki, Brazil ilishinda 1-0
- Mwaka 1986: Kombe la Dunia, Brazil ilishinda 1-0
- Mwaka 1990: Mechi ya Kirafiki, Brazili ilifungwa 3-0
- Mwaka 1999: Mechi ya Kirafiki, Zilitoka sare 0-0

No comments