THE GUNNING MACHINE ~ SIR FERGUSON vs ARSENAL (SEHEMU YA MWISHO)
NI VITA YA MIAKA 27.Kama nilivyoahidi wiki iliyopita kwamba leo tutaendelea na makala hii ya kocha aliyestaafu wa Man UTD, Sir Alex Ferguson dhidi ya Arsenal. Baada ya kuangalia mambo kadhaa, leo tuangalie Vita Ya FFP pamoja na lile bifu kali ya manahodha wa zamani wa timu hizo, Roy Keane na Patrick Vieira.
ROY KEANE VS PATRICK VIEIRA.
Mpaka waamuzi walikua wanawaogopa hawa watu kwani wote walikua ni watu jeuri na wababe. Utasema nini kwa Roy Keane ambaye ilikuwa ni lazima awe nahodha wa Man UTD kutokana na ubabe wake. Hakuna ambae angeweza kuwa juu yake zaidi ya kocha Sir. Ferguson.
Huku akikutana na kiungo mwenye futi 6.4 kwenda juu wa Arsenal Jamaa mweusi, mgumu sana, mbabe na asiyependa masihara hata kidogo.
Waliwahi kukunjana mara kadhaa uwanjani na utakumbuka ilibidi waamuliwe walipotaka kukunjana katika korido la uwanja wa highbury kabla hata ya timu kuingia uwanjani mwaka 2005. Mara nyingine alisikika Vieira koridoni akimwambia Roy atabasamu na jamaa alimjibu "nitatabasamu tukiwa na point 12 juu yenu"
Ugomvi wao unatajwa kuwa mkubwa zaidi mpaka sasa kwa miaka hii ya 2000.
VITA YA FFP.
Nimeiita vita hii FFP kwa kuunganisha majina ya Ferguson, Fabregas na Pizza. Pizza ni chakula maarufa cha waitaliano.
Zikiwa zimesalia dakika 20 tu mpira kumalizika, mwamuzi anaamuru penati ipigwe kuelekezwa katika lango la Arsenal ingawa si kweli kwamba Sol Campbell alimwangusha Wayne Rooney. Ruud Van Nistelrooy safari hii akauweka kambani.
Wakati Arsenal wakijaribu kusawazisha, Wayne Rooney akawaua kwa shambulizi la kushtukiza.
Arsenal wakawa wamekula kichapo lakini inasemekana kulitokea mtafaruku mkubwa katika korido la Old Traford wakati wachezaji wakirudi vyumbani na kwamba wachezaji wa Arsenal walitaka kumpiga Ruud Van Nistelrooy.
Ni katika mtafaruku huo ndipo mtu mmoja ambaye baada ya miaka kadhaa ndipo ilipogundulika kuwa ni Cesc Fabregas alipomtupia Sir. Ferguson Pizza iliyokuwa kwenye Buffet ndani ya vyumba vya uwanja wa Old Traford.
FERGIE VS WENGER.
Fergie hakua mwongeaji sana kwenye vyombo vya habari ingawa magazeti ya Uingereza yalijaribu kutengeneza mazingira ya uhasama kati yake na Wenger.
Mara kadhaa, Wenger aliwahi kukaririwa akiwakandia wachezaji wa Man UTD kama Daren Fletcher na Ruud Van Nistelrooy lakini Fergie alipoulizwa alijibu kwamba yeye anachoamini ni kwamba ana wachezaji wazuri.Kauli tata iliyotolewa na Wenger juu ya majibu hayo mazuri ya Fergie ni kwamba, "kila mwanaume huamini ana mke mzuri nyumbani kwake".
Kuna wakati Fergie akimzungumzia Wenger aliwahi kusema kwa utani kwamba, "wanasema ni profesa na ana akili nyingi kwa sababu anaongea lugha 5, mimi nina kijana pale klabuni ana miaka 17 kutoka Ivory Coast anaongea lugha 5".
Hakukuwa na ugomvi wowote kati ya wazee hao ingawa si marafiki.
"Mashabiki wanataka aondoke? Wanasema uwezo wake umefikia mwisho kwa sababu amefungwa magoli 8. Wanapaswa kuelewa kuwa ni kipindi cha mpito tu na anajenga timu yake. Walisema atafungwa na Udinese kwenye mechi ya mtoano ya ligi ya mabingwa lakini ameshinda.Nadhani bado anafaa kuwa kocha wao"
Yapo mengi sana kuhusu Fergie na Arsenal. Mwaka huu 2013 amepata gwaride la heshima katika uwanja wa Emirates baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu.
Hakika mzee huyu anastahili heshima kubwa kwa mchango wake katika soka. Ndiyo maana THE GUNNING MACHINE haikuona tatizo kutumia nafasi tatu kumwelezea. Kapumzike salama Babu Fergie. Karibu viwanjani kama shabiki.
Imeandikwa na Richard Leonce Chardboy kutoka kundi na page ya Wapenda Soka (kandanda) katika ukurasa wa Facebook.
Nipate katika chardboy7@gmail.com au @chardboy77 kwenye twitter na 0766399341
......Kwa habari za uhakika za Soka usikose kujiunga na kundi la Wapenda Soka (kandanda) au ku like page ya wapenda soka - kandanda katika ukurasa wa Facebook
Wenger atamkosa sana Fergie!
ReplyDeleteKibaya zaidi Wenger ataweza kamwe kumlipa SAF kile kipigo cha 8~2.
ReplyDeleteFergie ni alama ya soka.
ReplyDelete