PAULO DI CANIO NI MWIBA MKALI KWA CHELSEA

Katika mechi kali za Msimu wa 2002/2203 Tarehe 28 Septemba 2002 katika ligi kuu Nchini England basi ni ile iliyopigwa katika dimba la Stamford Bridge (darajani) kati ya wenyeji Chelsea na Wagonga nyundo wa London klabu ya West Ham United ambapo Chelsea walikubali kichapo cha bao 3-2
Di Canio akiipangua ngome ya Chelsea

Shujaa wa mechi hiyo alikua Paulo Di Canio ambaye sasa ni kocha wa Sunderland baada ya kufunga magoli mawili kati ya yale matatu ya West Ham siku hiyo akiwa amevalia jezi namba 10
Chakuvutia zaidi ni nguvu ya lile goli la pili alilofunga Di Canio akiwa umbali wa mita karibia 35 likimwacha kipa wa Chelsea wakati huo Carlo Cudicini ambaye anaichezea Los Angeles Galaxy hivi sasa akiwa hana la kufanya.
Di Canio
Katika Mchezo huo Magoli ya Chelsea yalifungwa na Jimmy Floyd Hasselbaink na Gianfranco Zola wakati lile goli la kwanza la West Ham United lilifungwa na Jermain Defoe.

Kati ya wachezaji ambao wameitesa sana Chelsea Paulo Di Canio raia huyu wa Italia naye yumo Tangu akiwa West Ham mpaka Chalton Athletic.

Aliweza akiwa kama mchezaji je atathubutu akiwa kama kocha kuinyanyasa tena Chelsea?
Tusibiri msimu unaoanza Tarehe 17 Agost kushuhudia hilo


Licha ya Kikosi cha West Ham msimu huo kua na wakali kama David James, Jermain Defoe, Michael Carick, Joe Cole, Paulo Di Canio,Fredric Kanoute,Les Ferdinand, Titi Camara, Lee Bowyer n.k timu hiyo ilishuka daraja msimu huo na kupelekea nyota kibao kuihama.

No comments

Powered by Blogger.