::::: HABARI ZILIZOKAMILIKA ZA USAJILI MPYA ULAYA :::::::

 
  CARLOS TEVEZ (Juventus)

     Juventus Imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Carlos Tevez kwa Ada ya uhamisho paund milioni 10 na anatarajia kufanyiwa vipimo ndani ya masaa 24 yajayo. Tevez amezichezea pia Man United na West Ham
 
 SIMON MIGNOLET (Liverpool)

    Golikipa namba moja wa Sunderland na timu ya Taifa ya Ubelgiji Mignolet amejiunga rasmi na Liverpool kwa Ada ya uhamisho wa Paundi milion 9 na kumfanya kuwa kipa namba mbili aliyesajiliwa kwa pesa nyingi nyuma ya David De Gea wa Man United  aliyesajiliwa kwa ada ya uhamisho paundi milioni 17 kutoka Atlentico Madrid.
Nafasi ya tatu na Nne inakamatwa na Fabian Barthez na Hugo Lloris waliosajiliwa kwa paundi milioni 7.8
 
 
Simon Mignolet mwenye umri wa miaka 24 anakua Mbelgiji wa kwanza kucheza katika historia ya klabu ya Liverpool na kazi kubwa aliyonayo ni kupata nafasi katika kikosi cha kwanza kwani kipa mkongwe wa Timu hiyo Pepe Reina Mustakabali wake haujajulikana.
 
Usaji wa Mignolet unamfanya kuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Liverpool msimu huu wengine wakiwa ni Kolo Toure toka Man City, Luis Alberto toka Sevilla na Lago Aspas toka Celta Vigo.
 
 
 ANDRE SCHURRLE (Chelsea)
 

   Chelsea Imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Bayer Liverkusen na timu ya Taifa ya Ujerumani Andre Schurrle kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 18 na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Kocha Jose Mourinho tangu ahamie Chelsea akitokea Real Madrid.
Andre anaweza kucheza kama Winga na mshambuliaji na atavaa jezi namba 14 na amesaini mkataba wa miaka mitano ndani ya Chelsea wanaotumia uwanja wa Stamford Bridge (darajani)
 
 

 KOCHA: CARLO ANCELLOT (Real Madrid)
Real Madrid Imekamilisha "dili" la kumpata kocha Carlo Ancelot toka Paris Saint Germain ya Ufaransa na amesaini mkataba wa miaka mitatu kuinoa klabu hiyo ya Santiago Bernabeu akichukua mikoba ya Jose Mourinho aliyetimkia Chelsea na kazi yake kubwa itakua kushinda kombe la Klabu bingwa Ulaya ambalo Madrid wamelikosa tangu mwaka 2002 licha ya kuwa na wachezaji nyota kila mwaka.
Ancellot atasaidiwa na Paul Clement aliyekua msaidizi wake alipoifundisha Chelsea, Zenedine Zidane na Straika wa Zamani wa Chelsea Hernan Crespo.

KOCHA: LAURENT BANC (Paris Saint Germain)
 
 Akiwa na miaka 47 tu anachukua mikoba iliyoachwa na Carlo Ancellot kuwafundisha matajiri wa jiji la Paris (PSG) katika mkataba wa miaka miwili.
Baada ya kuwakosa makocha wengine kama fabio Capello, Jose Mourinho, Andre Villas Boas, Frank Rijkaard na Arsene Wenger matajiri wanaomiliki timu hiyo waliamua kumfata Blanc.
 
......... tukutane Siku nyingine
Edo Daniel Chibo (facebook: Wapenda Soka (kandanda) na Edo Daniel1 katika Twitter)
 
 

2 comments:

Powered by Blogger.