WEKUNDU WA MSIMBAZI ~ SIMBA YAMALIZA MSIMU MZIMA BILA KUFUNGWA (INVINCIBLE SIMBA)

 
Simba SC
 
Tarehe 21 Aprili 2010 Simba Sports Club walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa Tanzania Bara kwa staili ya aina yake kwakua timu ya kwanza Tanzania kumaliza ligi bila kufungwa mchezo wowote.

Siku hiyo Simba ilimaliza Ligi kwa kuifunga Mtibwa Sugar 4-0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro. magoli mawili ya Musa Hassan "Mgosi", Ramadhani Chombo "Redondo" akifunga goli moja na lingine likifungwa na Mohamed Kijuso.


Katika Mechi 22 ambazo Simba ilicheza katika msimu wa 2009/2010 ilipoteza point 4 pekee, baada ya kutoka sare mbili pekee dhidi ya African Lyon na Kagera Sugar huku ikishinda mechi 20 ikitoka droo mara mbili na kujikusanyia point 62.

Simba iliweza kufunga jumla ya Magoli 50 na kuruhusu wavu wake kuguswa mara 12 tu ikipata tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa 38 namba ambayo ni kubwa kuwahi kufikiwa na timu nyingi zilizowahi kuchukua ubibgwa wa ligi duniani.

 Simba iliyoanzishwa mwaka 1936 ikiwa na makazi yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar Es Salaam ilikua na kikosi Imara ambacho hakuna timu yoyote iliyoweza kukifunga msimu huo wa mwaka 2009/2010.

Kikosi hicho cha Simba kilikua chini ya kocha Mzambia Patrick Phiri kikiwa na wachezaji nyota kama Ramadhan Chombo maarufu kama Redondo, Mussa Hassan Maarufu kama Mgosi, Mohamed Banka,Nico Nyagawa n.k

>>>>>>>>>

Tukutane mara nyingine katika kona ya Wekundu wa Msimbazi
 
...... Imeandikwa na Edo Daniel Chibo
Nipate katika facebook/wapendasoka(kandanda) group
 

2 comments:

  1. iliweza simba hii tu iliyokuwa chini ya mzee mzima patrick phiri alivokuja kuibadili.
    bahati mbaya akaingizwa kwenye siasa zetu hapo hata yeye aliona team chungu na kuamua kuondoka kwa upuuzi wa mpira wa kitanzania

    ReplyDelete

Powered by Blogger.