THE GUNNING MACHINE ~ KINACHOTARAJIWA KATIKA USAJILI WA MSIMU UJAO NDANI YA ARSENAL
Kama kawaida, msimu wa 2012-2013 nao umemalizika na kinachofuata sasa ni harakati za usajili kwa ajili ya msimu mpya wa 2013/2014 ambao ratiba yake imetoka huku ikiwaweka Arsenal kama wenyeji wa Aston Villa katika uwanja wa Emirates.
Tutasikia tetesi nyingi kuhusu timu Fulani kumwania mchezaji fulani,kukaribia kumnyakua mchezaji fulani na mengi ya namna hiyo kwani Ni kawaida baada ya msimu kuisha.
THE GUNNING MACHINE leo itazungumzia kwa uhalisia inachokitarajia msimu ujao kwa klabu ya Arsenal.Twende Pamoja.
- USAJILI
Mara nyingi tumesikia kuwa msimu huu Arsene Wenger ana bajeti ya Paundi Million 70 kwa ajili ya usajili. "Watu wanasahau kuwa tulijenga uwanja kwa kukopa Paundi Milioni 360, hivyo tulilazimika
kufanya kazi kwa kutumia bajeti finyu na kuwa katika Top level na hatukuwa na pesa kwakweli,
kufanya kazi kwa kutumia bajeti finyu na kuwa katika Top level na hatukuwa na pesa kwakweli,
"Nilikubali kubaki klabuni na nimepitia kipindi cha mpito,tumeibakiza klabu yetu katika Hadhi ya juu (kushiriki Ligi ya Mabingwa) na hapa tulipo sasa tuko vizuri sana kifedha na tuna uwezo wa kupambana tena na timu tajiri. Kipindi chote cha miaka 8 iliyopita kilikuwa kigumu na kinahitaji
ujasiri wa hali ya juu”. Alinukuliwa akisema Arsene Wenger.
Hapa napata picha kuwa wakati wa nyuma pale ambapo tuliambiwa kuwa Arsene alikuwa na pesa ya usajili haikuwa kweli hata kidogo.
Lakini kuanzia msimu ujao kutakuwa na mikataba minono ya Televisheni, mkataba mpya wa Fly Emirates utakaodumu mpaka mwaka 2018 na mkataba mpya wa Puma.
Inaweza kuwa ni kweli kwamba Arsenal wana pesa za kununua wachezaji mahiri msimu ujao na kuendelea lakini nina wasiwasi na kiasi hicho kinachosemwa cha Paundi Milioni 70.
Yawezekana isiwe kweli bali ni uzushi tu wa vyombo vya habari.
- WACHEZAJI WATAKAOONDOKA.
Kuna msululu wa wachezaji ambao natabiri kuwa wataondoka nao ni
- SEBASTIEN SQUILLACI (mkataba unaisha),
- ANDREI ARSHAVIN (mkataba unaisha),
- LUKASZ FABIANSKI (mkataba unaisha),
- NICKLAS BENDTNER (yuko kwamkopo Juventus) na huyu ametumia misimu miwili akizurura kwa mkopo na nadhani atauzwa. Sioni akirejea, labda kama atapata tena muda wa kwenda mahali kwa mkopo mwingine.
- ANDRE SANTOS (yuko Gremio ya Brazil kwa mkopo) nae bila shaka atauzwa kama sio
kukopeshwa kwingine, - PARK CHU YOUNG: (yupo Celta Vigo kwa mkopo) hali yake ni kama ya Bendtner na Santos.
- JOHAN DJOROU (yupo Hannover 96 kwa mkopo) Wenger anaonesha kupoteza kabisa matumaini kwa Mswisi huyu.
- DENILSON PERREIRA (mkataba unaisha).
- BAKARY SAGNA (mwaka mmoja umebakia kwenye mkataba wake) kuna dalili zote kuwa hatokuwepo Arsenal msimu ujao.
- FRANSIC COQUELIN/EMMANUEL FRIMPONG (hapa itategemea yupi Wenger atataka kumbakisha ila mmoja nahisi atauzwa).
- GERVINHO (huyu naumia kichwa) kama anaweza kubaki au kuuzwa lakini nahisi atauzwa kwani amekuwa na kiwango kisichokuwa na uhakika.
- MAROANE CHAMMACKH (Yuko kwa mkopo West Ham United)
anaweza kurejea ufaransa.
- WACHEZAJI WANAOWEZA KUSAJILIWA.
msimu ujao nahisi Arsenal wanahitaji kipa mpya mzoefu wa kumpa presha Szczesny kwani dogo huyu ana mchanganyiko wa "performance" na hatabiriki.
> Rene Alder,Julio Cesar, Simon Magnolet, Michel Vorm, Victor valdes wametajwa kuhusishwa na Arsenal mpaka sasa.
Mlinzi wa kati-
Arsenal watahitaji mlinzi Imara kwa sababu kuondoka kwa
Squillacci na Djorou, bas klabu itabaki na mabeki watatu tu wa kiwango cha juu.
Msimu wa ligi ni mrefu na mechi ni nyingi sana kwa mabeki watatu kumudu. Unapaswa kuwa angalau na mabeki wanne hadi watano wa kiwango cha juu.
> Ashley Williams (nahodha wa Swansea) inasemekana yuko kwenye mazungumzo na Arsenal na anapatikana kwa Paundi milioni 8 tu.
Kiungo mkabaji :-
Hii nafasi ilitakiwa kuimarishwa hata kabla Alex Song hajaondoka na baada ya Song kuuzwa, Arteta amejitahidi kuiziba lakini sio nafasi yake halisi aliyoizoea.
Hapa Wenger anatakiwa atafute mbadala mapema na hatuwezi jua atatokea wapi.kwani nani alimjua NACHO MONREAL kabla hajatua arsenal?
Mshambuliaji :-
Usajili hautakuwa na maana kama Arsenal hawatasajili mshambuliaji angalau wa kufunga magoli 25 kwa msimu kama ilivyokuwa kwa RVP msimu wake wa mwisho pale London.
Habari zinawahusisha STEVAN JOVETIC (fiorentina), GONZALO HIGUAIN (Real Madrid) na WYNE ROONEY (Man United japo sidhani kama wataweza kumlipa mshahara wa paundi 250,000 kwa wiki)
Beki wa kulia :-
Kama Bakary Sagna ataondoka nafasi yake itazibwa na wanaotajwa ni SEBASTIAN CORCHIA na LUKASZ PISZCZEK. Hapa najiuliza Malaga hawana beki wa kulia watuuzie?
Hahaha haaa Bado nina matumanini ya kurejea wachezaji chipukizi kama Ryo Miyaichi ( Yuko Wigan kwa mkopo), Joel Campbell (Real Betis) Serge Gnabry na Ignasi Miguel kushindania namba kama akina Gibbs na Jenkinson walivyofanya.
Arsenal inaweza kuanza kushindana tena kama Arsene Wenger atafanya vizuri sokoni na kitu kizuri msimu huu ni kuwa hakuna dalili ya kupoteza Wachezaji muhimu kama miaka ya nyuma, labda tusubiri tuone.
THE GUNNING MACHINE ya leo imetoka kwa mdau Faraji Abdul Kashengo.
Ungana nami Richard Leonce Chardboy wiki ijayo kuendelea na makala maalum ya FERGUSON Vs WENGER
Akhsante sana Richard kwa kuipost hii article@faraji Abdul kashengo
ReplyDeletePamoja sana Faraji usisite kutuma articles nyingine tutaziedit na kuziweka hewani ~ Edo
ReplyDelete