RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND HADHARANI ~ MAN UNITED KUANZA NA SWANSEA WAKATI ARSENAL WATAANZA NA ASTON VILLA
Msimu mpya wa Ligi kuu England Utaanza katika wikiend ya Tarehe 17-19 Mwezi Agosti kwa timu Ishirini kuingia dimbani
Mabingwa wa ligi kuu England msimu uliomalizika Klabu ya Manchester United Wataanza msimu mpya wa Ligi kwa kucheza na Swansea Ugenini baada ya Maombi ya Timu hiyo kuanzia mechi zake ugenini kupisha ukarabati unaoendelea katika Uwanja wa Old Trafford tofauti na utaratibu ambapo Bingwa mtetezi huanzia nyumbani
Mabingwa hao watakua wakitetea ubingwa wao wa 20 na kuanza kampeni mpya ya kupata ubingwa wa 21 bila ya kocha Alex Ferguson aliyekua mhimili mkubwa wa Timu hiyo kufikia mafanikio yao.
Safari hii watakua na David Moyes katika benchi la ufundi.
Mabingwa wa Europa League Klabu ya Chelsea wakiwa na kocha mpya Joseh Mourinho wataanza kampeni ya kuchukua ubingwa wa England kwa kucheza na Timu iliyopanda daraja na inayofundishwa na Steve Bruce klabu ya Hull City.
Arsenal wenyewe watakua nyumbani kuwakaribisha Aston Villa inayonolewa na Paul Lambert huku wakitegemea kuepuka ukame wa miaka mingi bila kombe.
Manchester City wakiwa na kocha mpya Manuel Pellegrin Watajaribu kurudisha ubingwa wao walioupoteza kwa mahasimu wao wakubwa Man United watakapoanza kibarua hicho kwa kupambana na Newcastle United katika uwanja wa Etihad.
Liverpool wenyewe watakua nyumbani Anfield kuwakaribisha Stoke City ambayo itaanza msimu mpya wakiwa na kocha mpya Mark Hughes
Liverpool wanategemea kupata ubingwa wa kwanza Tangu Ligi kuu England ianzishwe msimu wa 1992/1993 pia wakiwania nafasi ya kurudi katika ligi ya mabingwa Ulaya.
Totenham Hotspurs watasafiri kuwakabili Crystal Palace timu iliyopanda daraja msimu huu huku wakiombea Staa wao Gareth Bale asiwakimbie msimu huu.
Everton wakiwa na kocha mpya Roberto Martinez watasafiri kuwakabili Norwich City.
MECHI KAMILI ZA UFUNGUZI WA LIGI KUU ENGLAND MSIMU WA 2013/2014
- Arsenal vs Aston Villa
- Chelsea vs Hull City
- Crystal Palace vs Totenham Hotspurs
- Liverpool vs Stoke City
- Manchester City vs Newcastle United
- Norwich City vs Everton
- Sunderland vs Fulham
- Swansea City vs Manchester United
- Wes Brom vs Southampton
- West ham vs Cardiff City
Bora ifike tu,tumeshachoka na wikiendi za madisko tu bila soka.
ReplyDelete