MIWANI PANA YA EDO ~ CHIPUKIZI WAKALI 11 ULAYA


Kadri miaka inavyozidi kwenda ndivyo hivyo hivyo Wachezaji Soka wanavyozidi kuwa na umri mdogo huku wakifanya mambo makubwa uwanjani tofauti kabisa na hali ilivyokua miaka ya zamani

Ni rahisi siku hizi kukuta wachezaji wenye umri mdogo kabisa wakicheza katika vilabu vikubwa na hata kucheza fainali kubwa tu barani ulaya ikiwemo ile ya Ligi ya Mabingwa na ligi ya Uropa

Kwa mtazamo wangu mimi Edo leo naangazia kikosi changu cha wachezaji 11 vijana wanaotamba barani Ulaya:-

 
Kipa | Thibaut Courtois | Atletico Madrid (Akicheza kwa mkopo toka Chelsea)

Golikipa wa timu ya taifa ya Ubelgiji amezaliwa tarehe 11 May 1992.
Akiwa katika kiwango bora msimu uliomalizika katika klabu ya Atletico Madrid alikopelekwa kwa mkopo akitokea Chelsea akiisaidia timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu kucheza michezo mingi bila kufungwa na kuokoa michomo mingi ya washambuliaji wa klabu za La Liga. Na pia amekua nguzo kubwa katika kuwasaidia Atletico kutwaa kombe la Mfalme.

Atletico waliripotiwa kumtaka kwa jumla kipa huyo lakini yaonekana Chelsea hawana mpango wa kumuuza hasa wakati huu ambapo Petr Cech anakaribia kustaafu na klabu hiyo tayari imeaacha makipa wake wawili Hillario na Turnbull


Beki wa Kulia| Raphael Da Silva | Manchester United
 


Kijana huyu raia wa Brazil ambaye ni pacha wa beki mwingine wa Man United Fabio Da Silva aliyepelekwa QPR kwa mkopo katika msimu ulioisha.
 

Uwezo wa kukaba na kushambulia unamfanya kupendwa na mashabiki wengi wa United huku wakikumbukwa waliomtangulia kama Garry Neville kwa kuwatendea haki kuvaa “viatu” vyao

Hajaitwa katika timu ya Taifa ya Brazil lakini ni kati ya wachezaji ninaowatabiria kudumu kwa muda mrefu katika timu ya taifa kama atapewa nafasi.Mhimili mkubwa wa United katika beki ya kulia.
 
Beki wa kati | Matija Nastasic | Manchester City

Kukosekana kwa beki Vicent Kompany kulimpa nafasi kijana huyu raia wa Sebia kujijengea jina katika kikosi cha Manchester City kipindi hicho kikiwa chini ya kocha aliyetimuliwa Roberto Mancin kwani aliaminika na kupewa nafasi ambayo iliwaweka bechi wakali wengine wa City akiwemo Kolo Toure.
Spidi yake kama beki wa kati ilikua ya kupendeza huku akitoa pasi za uhakika na kuzuia mipira mingi isifikie lango. Amekua katika msimu mzuri na kama City watamwamini basi atakua tegemeo siku za usoni na mbadala mkubwa wa beki Nemanja Vidic katika timu ya Taifa.

Beki wa Kati | Raphael Varane | Real Madrid
 






Kijana huyu Raia wa Ufaransa amekua katika msimu mzuri sana katika klabu yake ya Real Madrid msimu uliomalizika na hata kupelekea kuitwa katika timu ya Taifa ya Ufaransa.
Kila mmoja anakumbuka jinsi alivyocheza katika mechi nne dhidi ya Barcelona na Man United. Kwangu mimi namwona kama nahodha ajayo wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa kwani amekua gumzo katika wapenda soka duniani kwa uwezo wake wa kupiga vichwa na kuzuia mashuti ya washambuliaji wa timu pinzani.

 Beki wa Kushoto | David Alaba | Bayern Munich

Jamaa ana kasi kama “mwanga” akiichezea timu bora kwa sasa Super bayern Munich walioondoka na vikombe vinne msimu huu (nimehesabia na lile la Germany Super Cup)
Beki huyu raia wa Austria hakuna ambaye hajui uwezo wake na kama ningepata nafasi ya kumshawishi kocha wa timu ninayoishabikia amsajili ningefanya hivyo.
Uwezo wake wa kupanda na kufanya mashambulizi bila kuchoka kumemfanya aonekane bora na hii ndo aina ya mabeki wanaotakiwa kwa sasa duniani. Alaba ameisaidia kwa kiasi kikubwa Bayern Munich kunyakua ubingwa wa Ulaya msimu huu akifunga baadhi ya magoli muhimu.

  Kiungo na Mshambuliaji wa Kulia | Lucas Moura | Paris Saint-Germain

Katika jambo ambalo PSG watajivunia daima ni kuipiku Man United katika “vita” ya kumsajili mchezaji huyu raia wa Brazil.
Ada ya uhamisho wa Paund 40 million ilitosha kwa PSG kumnyakua kijana huyu ambaye kama akiendelea na “form” aliyokua nayo msimu huu basi PSG hawatajutia pesa.
Lucas ni mmoja wa chipukizi ninaowatabiria makubwa katika fainali zijazo za kombe la dunia zitakzofanyika nchini Brazil


Kiungo wa kati  | Paul Pogba | Juventus

Ni mmoja kati ya chipukizi “mashujaa katika maamuzi” baada ya kukataa kuongeza mkataba akiwa  Manchester United na kuchagua kujiunga na mabingwa wa Italia kibibi kizee cha Turin,Juventus.
Na kwa kipaji alichoonyesha akiwa United na Juventus ni dhahiri huyu ataiteka nafasi ya kiungo siku za usoni.


Kiungo mshambuliaji | Mario Gotze | Borussia Dortmund








Mario Gotze ni mmoja kati ya viungo bora zaidi wenye umri mdogo kwa sasa duniani. Spidi yake,Uwezo wa kupiga mashuti yenye mwelekeo, Pasi zenye mwelekeo bora na kupandisha timu ni vitu vinavyomfanya kua lulu duniani na hicho ndo kilichowafanya Mabingwa wa Ulaya kumsajili hata msimu.
Katika Umri wake mdogo wa miaka 20 ameonyesha kua hana wa kumzuia kupata namba katika timu ya Taifa ya Ujerumani

Kiungo mshambuliaji| Isco | Malaga
Jina kamili ni Francisco Román Alarcón Suárez maarufu kama Isco ni mshambuliaji wa Hispania na klabu ya Ma
anti Cazorla kuihama Malaga na kujiunga na Arsenal, Aliletwa kijana huyu




.Kutokana na Uwezo mkubwa aliokua nao Cazorla mashabiki wa Malaga walipata wasiwasi kama kijana huyu mdogo ataweza kuziba nafasi ya Cazorla. Lakini baada ya mechi chache tu amekua kipenzi cha mashabiki wa Malaga huku akifunga magoli mazuri na Muhimu kwa klabu yake.

Kuna tetesi kwamba Isco anaweza kuihama Malaga kumfata kocha wake Pellegrin ambaye amehusishwa kwa kiwango kikubwa kuifundisha Manchester City.


Kiungo wa pembeni kushoto| Stephen El Shaarawy | AC Milan






Ana miaka 20 tu Raia huyu wa Italia akiwa ni mzaliwa wa Misri amekua tegemeo kubwa kwa klabu yake ya AC Milan kabla na baada ya kuwasili kwa mshambuliaji "mtukutu" Mario Ballotell.
Kasi yake uwanjani na uwezo mkubwa wa kupachika mabao umemfanya kuwa kama wakali wachache walioweza kuwika wakicheza nafasi hiyo kama Ryan Giggs wa Man United enzi zake alipokua na Umri kama wa huyu kijana.

Mshambuliaji| Romelu Lukaku | Chelsea

Mchezaji huyu raia wa Ubelgiji na mzaliwa wa Congo alipelekwa kwa mkopo Wes Brom mwanzoni mwa msimu ulioisha na klabu yake ya Chelsea na huku akiisaidia sana Wes Brom kwani magoli 17 katika ligi yameipandisha mpaka nafasi ya 8 katika msimamo
Mashabiki wa Chelsea wangependa kumwona Lukaku akirudi kikosini hasa wakati huu ambapo Torres anaonekana ni butu katika huku vyombo vya habari vikimnukuu kocha Joseh Mourinho kutaka kumfanya “Drogba Mpya” pale Darajani.


........ Wapo Vijana wengi waliowika msimu huu lakini kwa leo naishia hapa

 

2 comments:

Powered by Blogger.