WALIOKUDHARAU SIKU MOJA WATAKUSALIMIA KWA HESHIMA

           
THE MIGHTY BVB VS SUPER BAYERN

 
  Ni usiku mnene ,naangalia kiganja changu cha mkono wa kushoto nakutana uso kwa uso na mshale wa saa yangu ukionesha kuwa imeshafika saa saba usiku.Usingizi hauji,nikiwaangalia  marafiki zangu pembeni ni kama ndo wameamka vile kwani stori zimepamba moto,kila mmoja anaongea lake na kila mmoja anatamani asikilizwe yeye.
Hapo stori ilikua moja tu kila mmoja alijifanya anawajua vizuri wahusika wakuu wa stori. Mara “Lewandoski mbaya” mwingine “Schweinsteiger  kiungo bora kuliko wote duniani” huyu nae akasema “Muller anastahili kua mchezaji bora wa dunia”. Kila mtu aligeuka kua mchambuzi wa soka. Kabla ya hapo sikuwahi kumsikia rafiki yangu hata mmoja akizungumzia uzuri wa Dortmund, sikuwai kumsikia hata mmoja akibashiri kuwa Dortmund atafika walau nusu fainali. 


       Hii iliniumiza sana kichwa, nikarudisha ubongo wangu nyuma  mpaka mwishoni mwa mwezi wa 12. Nikakumbuka jumapili moja nikiwa na mabraza wangu ndani ya London pub, Dan Chibo, Edo Daniel Chibo, Chard boy  na David Samuel Marosi hawa ni wachambuzi wazuri wa soka, pia walikuepo wadau wengine wengi wa soka siku hiyo.
Baada ya Mohamed Diame na wagonga nyundo wenzake(West Ham United) kufanya yao dhidi ya Chelsea,kulikua na mechi mbili zinafuata kwa muda mmoja, mechi moja ilikua kati ya Man United vs Reading na nyingine illikua kati ya Bayern Munich vs Borussia Dortmund. Pasipo kua na shaka niliamini wadau wote tutakubaliana  kuangalia mechi ya Dortmund na Bayern,mara kidogo namuona Patrice Evra akiwaongoza wachezaji wenzake  kuingia ndani ya uwanja wa Madejski Nyumbani kwa Reading. Nikatulia nikisikilizia kauli za wadau Hakuna aliyezungumzia tena kuhusu mechi ya wajerumani, ikabidi nilianzishe nikamuita muhusika nikamwambia kwa sauti “Tubadilishie tuwekee mechi ya Dortmund na Bayern”. Mama yangu! Nilihisi napigwa siku hiyo, Kila neno chafu lilitamkwa juu yangu ,mdau mmoja akapayuka "hao Dortmund ndo wakina nani na wa ligi gani mi simjui hata mchezaji wake mmoja” kashfa hazikua juu yangu tu bali Bundesliga kwa ujumla hata wadau nilotegemea watakua upande wangu, walivaa miwani ya mbao wakajifanya hawakunisikia.


Nikapiga moyo konde nikaenda upande wa pili wa London pub ,huko nako nikakutana na Shorey pamoja na Robin Van Persie,muda huo mechi ya Bayern na Dortmund inakaribia kuanza.
Nilipokaa pembeni yangu alikuwepo mchambuzi nguli tena anayependwa na kukubalika na WATANZANIA wengi bila kupepesa mdomo nikamuuliza “unafurahia kuangalia hii mechi?” hakanijibu hafurahii ila ajui cha kufanya ili waweke mechi ya Dortmund na Bayern.
Nikamuita tena muhusika nikamwambia kwa kua upande ule umeweka mechi ya Man U, upande huu weka  mechi ya Dortmund, ndipo aliponijibu bila haya “Manager ameniambia niweke mechi  moja nzuri ,ndo tukaamua tuweke hii ya Man United na Reading”. Nikawa sina tena cha kuzungumza kwani manager alishaacha maagizo yake Ikabidi nicheze na live score kwenye simu yangu.



            Ila leo mambo yote yamebadilika, mimi wewe pamoja na Meneja wa London Pub wote tumejua kwamba kuna Bayern Munich na Dortmund ulaya. Wote kwa pamoja tumetambua ubora wa ligi ya ujerumani leo tumemjua Muller wa Bayern Munich na Reus wa Dortmund.
Natumai kesho utamjua Draxler wa Shalke 04 au Schurrle wa Leverkusen au  Max Kruse wa Freiburg. Nashukuru kwasababu leo mimi wewe pamoja na meneja wa London Pub tutaachana na promo za waingereza na kuanza kupenda mpira kwa kuangalia Bundesliga. Huko kuna wakina Gundogan wengi,pia kuna Mabeki wengi walowazidi viwango Rio Ferdinand na Vicent Kompany bila kusahau washambuliaji wenye njaa ya magoli kuliko Luiz Suarez na Robin van Persie. Najua kuanzia leo hatutakaa tena tukose mechi ya Dortmund vs Munich.
Najua manager we ndo utakua wa kwanza kuwasha tv kuwaangalia wajerumani ndani ya wembley viva bundesliga ligi bora ulaya nzima

                                      By kaijage jr
                                      Middle ya juu


 

1 comment:

  1. Nakumbuka sana hyo siku. Me sikuangalia mechi yoyote. Niliamua kukaa pemben na dada angu annah!
    Chardboy

    ReplyDelete

Powered by Blogger.