MAN UNITED VS CHELSEA

MUDA: saa 12 jioni

Manchester United wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa tayari mabingwa wakijikusanyia point 85 mpaka sasa  wakati Chelsea iko katika nafasi ya 4 ya simamo wa Ligi ikiwa na pointi 65 yani ni point 20 nyuma ya Mabingwa man United.

TUNAITAZAMAJE HII MECHI?

 Wakati Man United wakitaka kuweka  rekodi ya kuwa mabingwa wakiwa na pointi nyingi kabisa upande wao Chelsea wanaitafuta nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa Ulaya na hii itawezekana tu kama watamaliza katika nafasi 4 za juu maarufu kama Top 4

HARAKATI YA KUWANIA NNE BORA (TOP 4)

 Wakati Man United wakiwa tayari mabingwa na point zao 85 wakicheza michezo 35 nafasi ya pili inashikwa na Manchester City wenye pointi 72 wakicheza michezo 36,
Arsenal inakamata nafasi ya 3 ikiwa na point 67 ikicheza michezo 36 wakati Chelsea na Tottenham Hotspurs wanashika nafasi ya 4 na 5 wote wakiwa na point 65 Chelsea akicheza michezo 34 wakati Spurs wamecheza michezo 35 katika ligi
  Ushindi ni muhimu leo kwa Chelsea kama wanataka kujihakikishia mojawapo ya nafasi kwani wakishinda watapanda mpaka nafasi ya 3 lakini wakipoteza itakua neema kwa Arsenal na Spurs.

HISTORIA INASEMAJE KATI YA HIZI TIMU KATIKA LIGI ?

Man United na Chelsea zimekutana mara 141 katika historia ya Ligi kuu huku Man United wakishinda mara 59 wakati Chelsea wameshinda mara 40 na mara na 42 ikiishia sare.
Lakini Tangu kuanzishwa ligi kuu maarufu kama English Premier League msimu wa mwaka 1992/1993 timu hizo zimekutana mara 41 na kila timu kuondoka na ushindi mara 13 huku mara 15 zikiishia kwa sare.
  •  Ushindi mkubwa wa Man United nyumbani dhidi ya Chelsea ulikua mwaka 1960 ambapo United walishinda goli 6-0
  • Katika michezo 17 ambayo Chelsea walicheza na United katika Uwanja wa Old Trafford ni mchezo mmoja tu ambao Chelsea hawakufungwa goli lolote (clean shit)
  • Javier Hernandez (Chicharito) amefunga magoli 6 katika mechi 8 alizocheza dhidi ya Chelsea
  • Robin van Perse baada ya kucheza michezo 10 bila kufunga amerudi katika chati za ufungaji na katika michezo minne amefunga magoli 6
  • Frank Lampard ana magoli 201 mpaka sasa akiwa na Chelsea goli moja tu kufikia rekodi ya Bobby Tambling ambaye ndo mchezaji aliyefunga magoli mengi akiwa na Chelsea.
  • Katika mechi 6 zlizopita kati ya timu hizi yameshuhudiwa magoli 29 yakifungwa ambayo ni wastani wa magoli matano kila mechi
  • Mara ya mwisho Chelsea kushinda katika uwanja wa Old Trafford katika mechi za ligi ilikua mwaka 2009 wakishinda 2-1 magoli ya Joe Cole na Didier Drogba
  • Man United imefunga katika michezo 66 mfululizo katika uwanja wake wa nyumbani na kuweka rekodi katika ligi.

                             TAARIFA YA VIKOSI

MAN UNITED

Sir Alex Ferguson kwa upande wake ana majeruhi Danny Welbeck na Ashley Young wenye maumivu ya enka, Darren Fletcher bado anasumbuliwa na ugonjwa wa tumbo wakati paul Scholes anatarajia kuwepo benchi katika mechi ya leo
CHELSEA

Rafa BeniteZ kwa upande wake hana majeruhi isipokua Oriel Romeu ambaye ameanza kufanya.
John Obi Mikel,Eden Hazard na Ashley Cole wote wanatarajia kuwemo kikosini

 
                          
           REFA WA LEO NI HOWARD WEBB

Howard Webb ndo atakayepuliza filimbi pale kati ikiwa ameshachezesha michezo 27 msimu huu akitoa kadi za njano 100 na kadi nyekundu 3. 

Muhimu: mechi inayofuata kwa Chelsea itakua Jumatano usiku watakapowakaribisha Tottenham Hotspurs

No comments

Powered by Blogger.