THE GUNNING MACHINE
Nacho Monreal alifunga goli lake la kwanza ndani ya uzi wa Arsenal. Ilikua Machi 16 dhidi ya Swansea. Ni kitu kizuri kwake ingawa anapaswa kukumbuka kuwa siyo kazi rahisi kumng'oa Kieran Gibbs katika nafasi ya beki wa kushoto kama muingereza huyo akiwa fit kwa asilimia 100.
Kama ilivyo ada ya THE GUNNING MACHINE ya mwisho wa mwezi, leo tunafunga mwezi Machi na kuumulika mwezi April. Twende pamoja.
REKODI NZURI YA MWEZI MACHI.
Chini ya Arsene Wenger, Arsenal wameshinda mechi 23, wametoa sare 4 na kufungwa mechi 1 tu. Tena mwaka huu dhidi ya Tottenham. Unaweza kuona kuwa ni rekodi nzuri kwa mwezi wa tatu katika ligi kuu England kwa Arsenal.
Wakiwa kama 'underdogs' Washika Bunduki wa London waliweza kutumia nafasi hiyo kuudhihirishia ulimwengu kwamba wao siyo matawi ya chini kama baadhi ya mashabiki wanavyodhani.
Ilikua ni katika mchezo wa marudiano wa raundi ya 16 bora za ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich ugenini walipotoa kichapo cha mabao 0-2 kwa miamba hiyo ya soka nchini Ujerumani.
Waliondolewa katika michuano kutokana na kufungwa mabao 1-3 katika mchezo wa kwanza.
"hiyo ilikua kama turning point kwetu", Anasema Thomas Rosicky katika mahojiano na tovuti ya klabu. Maneno ambayo yalidhihirika Machi 16 baada ya kutoa kichapo cha 0-2 kwa timu ngumu ya Swansea kwenye ligi kuu ya England.
Mwezi ukafungwa kwa ushindi mnono wa mabao 4-1 na kiwango cha kuvutia (brilliant performance) dhidi ya Reading Machi 30.
HARAKATI ZA TOP 4
The Gunners wamefanikiwa kukusanya alama 6 kati ya 9 zilizokua mezani kwao katika ligi kuu mwezi Machi,2013. Kosa kubwa lilikua ni kushindwa kuizuia Tottenham ambayo walikutana nayo Machi 3 na kuambulia kichapo cha mabao 2-1.
Arsenal sasa wanaendelea kukaa katika nafasi ya 5 wakiwa na alama 53 kwenye msimamo, alama 2 nyuma ya Chelsea wanaoshika nafasi ya 4 na alama 4 nyuma ya Tottenham wanaoshika nafasi ya 3.
Hii inaiweka Arsenal katika hali ngumu, wakihitaji kushinda kila mchezo uliopo mbele yao huku wakiomba mabaya kwa wapinzani wao hasa Tottenham ambao wamecheza michezo 31 dhidi ya 30 ya Arsenal.
Lakini pia Chelsea ambao wanaonekana kuchechemea katika ligi.
MACHO YOTE MWEZI APRIL.
Arsenal wana michezo mitano katika mwezi huu. Hiki ni kipindi ambacho hakuna timu inapoteza mchezo kirahisi kutokana na kuwania nafasi mbalimbali kwenye ligi.
Wataanzia Hawthorns, nyumbani kwa W.B.A April 6 kisha watasafiri mpaka Norwich April 13 kuwakabili watoto wa jiji hilo.
Siku tatu baadae, yaani April 16, Arsenal itabidi warudi nyumbani kwao London katika uwanja wa Emirates kukabiliana kiporo chao cha mchezo dhidi ya Everton ambacho kinaweza kuwapa nafasi nzuri kama watakitumia ipasavyo.
April 20, The Gunners watawasha mitutu yao tena. Safari hii wakisafiri kuwafuata Fulham kabla ya kurudi nyumbani kumkaribisha Robin Van Persie na Mashetani wekundu ambao kwa miezi ya karibuni wamekuwa kama ndoto ya kutisha kwa Arsenal.
Ni safari ngumu ya pointi 15 muhimu kuliko kitu chochote kwa sasa.
Ugumu unatokana na kuwa hakutakuwa na mchezo dhidi ya Chelsea wala Tottenham. Hivyo vita ya top 4 itategemea na matokeo ya Tottenham ambao watacheza na;
EVERTON (H)
CHELSEA (A)
MAN CITY (H)
WIGAN (A)
Na chelsea ambao wao watakabiliana na;
SUNDERLAND (H)
TOTTENHAM (H)
FULHAM (A)
LIVERPOOL (A)
SWANSEA (H)
Katika mwezi huu wa nne.
HALI ILIVYO KIKOSINI.
Abou Diaby atakuwa nje kwa muda wa miezi 9 akihitaji upasuaji wa goti, hivyo msimu umeisha kwa upande wake.
Jack Wilshere hatarajiwi kucheza mchezo wowote mwezi huu kutokana na matatizo yake ya enka.
Theo walcott atakuwa fiti katika mchezo dhidi ya Norwich.
Hii itampa nafasi Aaron Ramsey kucheza kama kiungo mchezeshaji katikati, lakini pia Thom Rosicky atapata nafasi.
Hii itampa nafasi Aaron Ramsey kucheza kama kiungo mchezeshaji katikati, lakini pia Thom Rosicky atapata nafasi.
Lucas Podolski yupo fiti sambamba na Kieran Gibbs huku Gervinho akijaribu kurudisha form yake. Kumbuka amefunga mara 2 na assist 2 katika michezo miwili iliyopita.
BUNDUKI ZIKO TAYARI KWA NGUVU ZATE KURUDI NDANI YA 4 BORA KAMA KAWAIDA YETU.
.......Tukutane mara nyingine ila usisite kutoa ushauri maoni na mtazamo wako kuhusu THE GUNNING MACHINE ya WAPENDA SOKA
BUNDUKI ZIKO TAYARI KWA NGUVU ZATE KURUDI NDANI YA 4 BORA KAMA KAWAIDA YETU.
.......Tukutane mara nyingine ila usisite kutoa ushauri maoni na mtazamo wako kuhusu THE GUNNING MACHINE ya WAPENDA SOKA
Imeandikwa na Richard Leonce Chardboy kutoka Wapenda Soka (Kandanda) Group.
Nipate katika chardboy77@yahoo.com na @chardboy77 kwenye twitter Au 0658399341
No comments