MIWANI PANA YA EDO - AZAM NA SAFARI YA KUELEKEA UBINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

NJIA AMBAZO AZAM WANATAKIWA KUZIPITIA KUFIKIA MAFANIKIO WALIYOSHINDWA SIMBA NA YANGA!!!


AZAM FC
Azam Footbal Club, Timu ngeni kusikika katika masikio ya Wapenda soka Afrika kwani ni mara yake ya kwanza ikishiriki katika michuano mikubwa ya pili Afika baada ile ya Klabu Bingwa.
Timu hiyo kutoka Mbande Chamazi - Mbagala Jijini Dar es Salaam ilianza hatua ya awali kwa kuwatoa Al-Nasri ya Sudan Kusini kwa ushindi wa Jumla wa mabao 8-1 na kutinga Raundi ya kwanza ambapo safari hii walisafiri mpaka Monrovia kuwakabili Barack Young Controllers ya Liberia na kuifumua mabao 2-1kabla ya kurudia jana katika dimba la uwanja wa Taifa na Kulazimishwa sare ya bila kufungana na hivyo kuifanya Azam FC kusonga mbele kwa jumla ya ushindi wa bao 2-1
Mpaka hapa ilipofika tayari ni mafanikio makubwa kwa timu hiyo ambayo inamilikiwa na Tajiri na mmiliki wa makampuni ya Azam, Bakhressa.

                MECHI YA JANA UWANJA WA TAIFA

Azam iliingia uwanjani ikiwa na matumaini kibao ya kusonga mbele hasa ikichagizwa na ushindi wa ugenini iliyoupata Jijini Monrovia wiki mbili zilizopita na mwisho wa siku matokeo yakaishia 0-0 asante kwa ushindi wa ugenini.

SABABU ZILIZOSABABISHA KUTOA SARE

Mimi si mtaalamu sana wa ufundi lakini zipo sababu zinaweza kua ni chanzo cha kutoa sare:-
  • Wachezaji kujiamini kupita kiasi hasa baada ya ushindi wa Ugenini wa 2-1
  • Kutokua makini kwa washambuliaji hasa Kipre Tcheche,John Bocco na Kipre Balou kwani kama wangekua makini ushindi ungepatikana.
  • Wachezaji kuzomewa wakati wakijua kabisa wako uwanja wa nyumbani hii inawapotezea umakini wakiwa na mpira na hili lilijitokeza pia katika mechi dhidi ya Al-Nasri kwani Azam walishinda goli 3-1 hapa nyumbani lakini wakaibuka na ushindi mkubwa ugenini. Watanzania tumekosa uzalendo hasa kwa mashabiki wacheche ambao walikua wamekaa upande wa mashabiki wa Yanga mara nyingi walikua wakiwazomea Azam kila walipokua wakigusa mpira na kushangilia pale Baracks walipokua wakishambulia. Ni utamaduni ambao tulikua tumeuzoea kwa Simba na Yanga baada ya Azam kuja tukajua ungepotea.

HATUA ZIPI ZIMEBAKI MPAKA KUFIKA FAINALI?

RAUNDI YA PILI


 Baada ya kufanikiwa kuvuka raundi ya kwanza sasa Azam FC imekata tiketi ya kutinga hatua ya Raundi ya pili ya Kombe la shirikisho barani Afrika na Itakutana na FAR RABAT wakali kutoka Nchini Moroko ambao waliivurumisha Al Nasr ya Libya baada ya jana kutoka sare ya bao 1-1 nchini Libya hivyo kuwavusha raundi ya kwanza kwa jumla ya mabao 2-1 yani ni kama Azam FC ila wao walichagizwa na ushindi  wa 1-0 walioupata majuma mawili yaliyopita huko Rabat Moroko.
Mechi ya kwanza itapigwa jijini Dar es Salaam kati ya Aprili 19-21 wakati Marudiano ni Mei 3-5 Nchini Moroko.

HATUA YA MTOANO.


Kama Azam Fc Watafanikiwa kuvuka raundi hii basi Wataingia raundi ya mtoano ambapo hapo ni pagumu zaidi kwani watakutana na timu zilizotolewa katika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika na zile ambazo zimevuka raundi ya pili ya kombe hili.

HATUA YA MAKUNDI


Washindi wa Hatua hii ya mtoano ya kombe la shirikisho Barani Afrika ambalo linazaminiwa na kampuni ya Simu za mkononi ya Orange watapangwa katika makundi mawili na kucheza ligi ya mtindo wa nyumbani na ugenini.

Timu 8 zitazopita hatua ya mtoano zitapangwa katika makundi mawili ya timu 4 kila kundi na kucheza ligi ambayo itatoa washindi wawili wa kila kundi ambao wataingia katika hatua inayofata yani Nusu Fainali.
 

NUSU FAINALI


Timu mbili za kila kundi zitaingia hatua ya Nusu Fainali ambapo mshindi wa kundi kundi A atacheza na Mshindi wa Pili wa kundi B na mshindi wa Kundi B atacheza na mshindi wa pili wa kundi A. Ambapo zitacheza mechi za nyumbani na Ugenini na washindi wataingia Fainali. 

FAINALI


Tofauti na ligi ya mabingwa barani Ulaya (UCL) au ile ligi ya Europa ambapo Huteuliwa uwanja mmoja ambao huchezwa fainali, Lakini Fainali za michuano ya Afrika kwa njia ya vilabu ni tofauti kwani fainali huchezwa kwa mtindo wa mechi za nyumbani na ugenini na Bingwa hupatikana kutokana na matokeo ya jumla.
ikumbukwe bingwa wa michuano hii atacheza Super Cup 2014 ambapo itakutanisha bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika na Bingwa wa kombe la shirikisho.
 
>>>> Hii ndiyo safari ya Azam FC, timu pekee iliyobaki katika michuano ya kimataifa ikiwakilisha Taifa la Tanzania lenye jumla ya watu zaidi ya milion 45. Nadhani kumalizika kwa ligi ya Vodacom kutatoa mwanya kwa Azam FC kujiandaa vyema zaidi na pengine kufika mbali.
 
Je wataweza kufanya yale yaliyoshindwa kufanywa na Yanga na Simba wakongwe wa Soka la Tanzania ambao kila mwaka wanashiriki na kutoka kapa.


 
>>>>> MUNGU IBARIKI AZAM FC, MUNGU IBARIKI TANZANIA <<<<<<<
 
.......Imeandikwa na Edo Daniel Chibo wa Wapenda Soka(kandanda) group katika ukurasa wa Facebook.

No comments

Powered by Blogger.