MANCHESTER UNITED vs MANCHESTER CITY: NI ZAIDI YA EL CLASICO?
Baada ya Man City kuiadabisha United msimu uliopita kwa kuichapa 6-1 nyumbani kwa United, timu hiyo inarudi Old Trafford Jumatatu Usiku kutaka kuendeleza walipoachia mwaka msimu uliopita huku United ikitaka kulipiza kisasi na kujihakikishia nafasi ya kuchukua ubingwa wa England msimu huu.
Kwa upande wa Man United:Wayne Rooney
anatarajia kuanza katika mechi hiyo maarufu kama "Manchester derby" baada ya kua nje ya kikosi kwa mechi mbili mfululizo akiwa majeruhi.
Rafael pia anatarajia kuwemo kikosini baada ya kutoka mapema katika mechi iliyopita kwa matatizo ya misuli lakini nahodha Nemanja Vidic na John Evans bado wana mashaka kama watacheza au lah kwani nao wako majeruhi. Manchester City wao kwa upande wao hawana majeruhi wapya zaidi ya Jack Rodwell ambaye anatarajiwa kurudi katika nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Chelsea wikiend ijayo
MTAZAMO WA MECHI
Baada ya kukubali kipigo cha kihistoria msimu uliopita na kupoteza ubingwa kwa mahasimu wao wa jadi Man City, United watataka kulipiza kisasi na pia kuwapokonya City Ubingwa waliouchukua msimu uliopita.Kwa kushinda mechi hiyo kutaifanya United kuongeza wigo wa point kufikia 18 katika uongozi wa ligi hiyo ambayo itawafanya United kuhitaji points 4 tu kuwa mabingwa.
Kocha wa man United alinukuliwa akisema "Arsenal,Chelsea,Man City,Liverpool na Totenham hizi timu zote mashabiki wake wanategemea timu zao kuchukua kombe mojawapo na sisi tunajitahidi tulipate kombe hili ndicho kinachotegemewa na mashabiki wetu"
Huu utakua ubingwa wa 13 kwa Man United na kwa kocha Alex Ferguson katika miaka 21 tangu kuanzishwa Ligi ya Premia ya England.
kocha wa Man City Roberto Mancin amekaririwa akisema " Nimesema mara nyingi sisi ni timu ndogo katika kushindania ubingwa kwani ni miaka miwili tu tumekua tukishindania ubingwa tofauti na timu zingine"
HISTORIA INASEMAJE KUHUSU MECHI KAMA HII?
- Ushindi wa Man City wa magoli 6-1 msimu uliopita ni kati ya vipigo vikubwa kuwahi kutokea kwa klabu ya Man United na mara ya kwanza kuwahi kufungwa magoli sita tangu walipofungwa idadi hiyo mwaka.
- Mechi ya leo ni mechi ya 165 kati ya timu hizo katika mashindano yote huku United ikiongoza kwa kushinda michezo 69 wakati City ikishinda 45 huku droo zikiwa 50.
- Sir Alex Ferguson na Roberto Mancini wamekutana mara 11 wakiwa kama Makocha wa timu hizo huku Ferguson akishinda 6 wakati Mancin akishinda 4 na mara ya mwisho kukutana katika ligi pale katika uwanja wa Man City Etihad, Man United walishinda 3-2.
Manchester United
- Manchester United wameshinda points 50 kati ya points 54 katika mechezo 18 iliyopita katika ligi kuu ikishinda 16 na kudroo 2.
- Kikosi hicho cha Sir Alex Ferguson ndo timu ya kwanza katika historia ya ligi ya England kushinda michezo 25 kati 30 katika msimu mmoja wa ligi.
- Man United wanahitaji points 19 katika mechi 8 zilizobaki kuweka rekodi ya kuwa na points nyingi kwa msimu mmoja (96 points)
- Man United haijafungwa ndani ya dakika 627 walizocheza katika ligi kuu.
- Man United Haijafungwa katika mechi 53 zilizopita katika ligi ambazo walitangulia kufunga goli.
- katika mechi tatu zilizopita (dhidi ya Norwich,Reading na Sunderland), Man United wamekubali shuti moja tu langoni kwake (on target)
- Robin van Persie amefikisha mchezo wa 9 sasa katika mashindano yote akiwa na Man United bila kufunga goli lolote japokua amejaribu kufunga mara 24 katika mechi hizo.
Manchester City
- Man City wako nyuma kwa pointi 8 chache zaidi ya walizokua nazo msimu uliopita katika hatua kama hii.
- Man City wameruhusu magoli 26 katika ligi ikiwa ni magoli 5 pungufu ya timu yoyote iliyo katika ngazi ya 4 bora katika ligi na kutoruhusu wavu wao kuguswa katika michezo 14.
- Carlos Tevez amefunga magoli 7 katika mechi 7 zilizopita katika mashindano yote. Amefunga magoli 34 katika mechi 97 akiichezea man United na amefunga magoli 3 katika mechi 7 tangu alipohama kutoka United na kujiunga na City kila
- Edin Dzeko amefunga magoli 5 katika mechi 6 dhidi ya man United.
Wyne Rooney,Robin Van Perse na Michael Carick kwa upande wa United
Kun Aguero,Yaya Toure na Carlos Tevez
1-2 fergie kazingua
ReplyDeleteGGMU