FIRST ELEVEN AMBAYO HAIJAWAHI KUSHINDA MEDALI ZA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Wyne Rooney,Cristiano Ronaldo, Messi, Drogba na Gerrard ni kati ya mastaa ambao wameshaonja utamu wa kuwa Mabingwa wa Ulaya lakini kuna mastaa wengine waliokua au wenye majina makubwa kwa bahati mbaya hawajawahi kuonja utamu huo kwa sababu mbalimbali.
Hii ni orodha ya wachezaji 11 ambao hawajawahi kuchukua ubingwa wa ulaya katika klabu japokua wamecheza au wanaendelea kucheza Ulaya:-
Hii ni orodha ya wachezaji 11 ambao hawajawahi kuchukua ubingwa wa ulaya katika klabu japokua wamecheza au wanaendelea kucheza Ulaya:-
Gianluigi Buffon | Kipa
Golikipa wa Timu ya Taifa ya Italia na klabu ya Juventus ambaye watu wengi wanamchukulia kama golikipa bora zaidi duniani.
Bufon alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2003 japokua timu yake Juventus ilipoteza katika fainali dhidi ya AC Milan kwa penati.
Bufon alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2003 japokua timu yake Juventus ilipoteza katika fainali dhidi ya AC Milan kwa penati.
Buffon alikua na Juventus wakati ule iliposhushwa daraja kwa hatia ya kupanga matokeo ya mechi na aliisaidia kurudi tena katika Seria A na hatimaye kupata nafasi ya kucheza tena Ligi ya Mabingwa Ulaya. Muda wote amekua na Juventus katika Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini hajafanikiwa kuipa ubingwa wa Ulaya.
Fabio Cannavaro | Mlinzi
Unamkumbuka Mchezaji huyu ambaye amewahi kuwa mchezaji bora wa dunia ambaye ni kati ya mabeki bora kuwahi kutokea katika historia ya Soka. Wakati Juventus ikishushwa daraja huyu alikua kati ya wachezaji walioihama klabu hiyo na kujiunga Real Madrid ambapo aliisaidia Madrid kushinda Ubingwa wa La Liga mara mbili ila hakufanikiwa katika ligi ya mabingwa japokua alifankiwa kuiongoza Italia kuwa mabingwa wa dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.
Philipp Lahm | Beki
Lahm ni kati ya wachezaji wakongwe japokua ana umri wa miaka 29 tu. Ni Nahodha wa Ujerumani na klabu ya Bayern Munich.
Akiwa na Bayern Munich ameishia kushika nafasi ya pili mara mbili wakati Bayern Ikipoteza kwa Inter Milan na Chelsea.
Lahm kama Buffon wako katika harakati za kuziongoza timu zao msimu huu ambapo Bayen Itacheza na Juventus katika hatua ya Robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tony Adams | Beki
Mojawapo kati ya mabeki bora kabisa kuwahi kutokea katika klabu ya Arsenal. Tony amecheza misimu 22 akiwa na Arsenal akishinda Ubingwa wa ligi ya England mara 4, Kombe la FA mara 3,Kombe la ligi mara 2 na ngao ya hisani mara 1.
Muingereza huyo alishindwa kabisa kupata medali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kipindi chote alichoshiriki akiwa na Arsenal na hivi sasa amestaafu mpira basi imebaki tu historia kwani hatoweza kupata tena medali hiyo labda aje awe kocha na kuisaidia timu atakayoifundisha kuwa bingwa.

Mchezaji bora wa Dunia mwaka 2003 akiiongoza Juventus kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya japokua aliikosa fainali kwakua na kadi mbili za njano akishuhudia timu yake ikipoteza dhidi ya AC Milan Tangu hapo hakufanikiwa lolote katika michuano hiyo na sasa ameshastaafu.
Patrick Vieira | Kiungo
Alikua kiungo bora kabisa akicheza kama kiungo mkabaji mwishoni mwa miaka ya 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa na nahodha wa Arsenal alizichezea pia Juventus na Inter Milan hajawahi kushinda Medali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa na nahodha wa Arsenal alizichezea pia Juventus na Inter Milan hajawahi kushinda Medali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
.
Pires ni mmojawapo wa wachezaji wa Arsenal timu ambayo haijawahi kushinda kombe la ligi ya mabingwa ulaya. Pires akiwa mhimili mkuu wa Arsenal msimu wa 2003/2004 ambapo Arsenal walimaliza msimu mzima bila ya kufungwa katika ligi kuu England.
Katika Fainali pekee kwa Arsenal katika Ligi ya Mabingwa mwaka 2006 Pires alitolewa dakika ya 12 wakati Jens Lehman alipotolewa kwa kadi nyekundu kwa faulo aliyomfanyia Samuel Eto'o wa Barcelona ambapo Arsenal walipoteza.

Gwiji la Italia na mmojawapo wa washamuliaji wakali wa mabingwa wa Seria A 2000/2001 klabu ya AS Roma ya Italia.
Roma haijawahi kushinda kombe la mabingwa Ulaya hivyo Totti anaongezeka katika orodha iliyotangulia kwakua mshambuliaji mkali ambaye hajawahi kupata medali ya Ligi ya mabingwa Ulaya.
Roma haijawahi kushinda kombe la mabingwa Ulaya hivyo Totti anaongezeka katika orodha iliyotangulia kwakua mshambuliaji mkali ambaye hajawahi kupata medali ya Ligi ya mabingwa Ulaya.
Zlatan Ibrahimovic | Mshambuliaji
Mchezaji mwenye kipaji raia wa Sweden aliyewahi kuzichezea Ajax,Juventus,Inter Milan,Juventus,Barcelona na Ac Milan kabla ya kujiunga na PSG ya Ufaransa.
Ni moja kati ya wachezaji ambao amekua akishinda ubingwa wa nchi na kila klabu aliyoichezea na hivi sasa anaiongoza PSG ambayo inakaribia kuchukua ubingwa wa League 1 na wakicheza na Barcelona katika hatua ya Robo fainali.
Ibrahimovicana miaka 31 na amebakiza miaka michache astaafu hivyo ana kazi kubwa kufikia mafanikio ya kutwaa medali ya ligi ya mabingwa.

Ruud Van Nistelrooy | Mshambuliaji
Mchezaji wa tatu kwa kufunga magoli mengi katika michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya akiwa na magoli 56.
Ruud alijijengea jina kubwa sana akiwa na klabu ya Man United ya England kabla ya kuhamia Real Madrid akiweka rekodi ya kufunga magoli 14 katika msimu mmoja wa ligi ya mabingwa Ulaya.
Ruud alijijengea jina kubwa sana akiwa na klabu ya Man United ya England kabla ya kuhamia Real Madrid akiweka rekodi ya kufunga magoli 14 katika msimu mmoja wa ligi ya mabingwa Ulaya.
Nistelrooy alifanikiwa kushinda ubingwa wa ligi kuu England akiwa na Man United kabla ya kuhamia Madrid na kushinda La liga pia na kuna tuzo nyingi tu amezipata akiwa kama mchezaji lakini hajawahi kushinda ubingwa wa Ulaya japokua alifanikiwa kufika Nusu fainal ya mashindano hayo mwaka 2002.
Ronaldo Luis Nazario De Lima | Mshambuliaji
Ni mmojawapo kati ya washambuliaji wakli ambao wamewahi kutokea duniani akiwa na nishani 3 za mchezaji bora wa dunia akishinda pia Ubingwa wa ligi ya Hispania akiwa na Real Madrid pia akishinda ubingwa wa Ligi ya Uholanzi akiwa na PSV.
Alishinda pia Copa Del Rey na akashinda pia Uefa Cup akiwa na Inter Milan na hatimaye kuiongoza Brazil kushinda kombe la dunia mwaka 2002.
Ronaldo hajawahi kushinda Ligi ya mabingwa Ulaya lakini aliwahi kufika nusu fainali mwaka 2003 akiwa na Real Madrid.

...... HAWA NI BAADHI TU YA WAKALI 11 AMBAO HAWAJAWAHI KUSHINDA LIGI YA MABINGWA ULAYA
JE UNAWAKUMBUKA WENGINE?
Walistahili kuvaa medali, bahati haikua yao
ReplyDeleteMe nawakumbuka wengine kama Michael Owen, anaondoka Liverpool tu wenzie wanabeba ndoo.
ReplyDeleteKagawa ajipange yasimkute.
RVP pia amepoteza muda arsenal.
ChardBOY