WALICHOANDIKA WAPENDA SOKA KATIKA FACEBOOK
ALLEN D. LYAMUYA Ameandika
\
PICHA KWA HISANI YA PIPO LEON na TANGE |
......Lionel Messi amefunga goli lake la 23 ugenini katika msimu huu wa La Liga dhidi ya Celta Vigo na kufikia rekodi ya Cristiano Ronaldo ya msimu uliopita.
Messi amekua mchezaji wa pili katika historia ya La Liga kuzifunga timu zote 19 wa kwanza akiwa ni Cristiano Ronaldo lakini Messi amemzidi Ronaldo kwa kua mchezaji wa kwanza kuzifunga timu zote za La liga katika mechi mfululizo yaani kila mechi jamaa anafunga.
Mpaka sasa Messi amefunga jumla ya magoli 96 ya ugenini katika La Liga wakati ni mchezaji mmoja tu anayemzidi Hugo Sanchez mchezaji wa zamani wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Mexico yeye alifunga magoli 99, hivyo basi Messi anahitaji magoli manne (4) kumzidi na kuvunja rekodi hiyo.
Huu ni msimu wa 5 mfululizo kwa Messi akiwa na "assists" zaidi ya 11 katika La Liga na klabu yake ya Barcelona.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<,
OMARY BRAVO MOHAMED Ameuliza
........Sunderland wamemfukuza kocha wao Martin O'Neil, Je wamefanya uamuzi sahihi?
Habari zinasema Baada ya Kufungwa nyumbani na Man United, hatimaye Sunderland wameeamua kumtimua kazi aliyekua kocha wa timu hiyo Martin O' Neil wakiwa wamebakiza michezo 7 huku wakiwa juu ya mstari wa kushuka daraja kwa pointi moja tu .
Sunderland hawajashinda michezo 8 waliyocheza.
Taarifa kutoka katika klabu hiyo zilisema "Hakika hakuna anayefurahia uamuzi huu lakini inabidi itokee kwakua tuna vita ya kupigana tusishuke daraja"
Miezi 16 imepita tangu O'Neil kuchukua kibarua cha kuinoa Sunderland alipofukuzwa Steve Bruce na kua na mafanikio katika siku za mwanzo kwani alishinda mechi 7 katika mechi 10 na kuifanya Sunderland kumaliza nafasi ya 13 msimu ulipoisha.
O'Neil anaiacha Sunderland katika rekodi mbaya kwani katika mechi 55 ameweza kushinda mechi 16 tu.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
DULLA JANE ameandika
..........Dakika 633 zimepita tangu De Gea alipofungwa goal la mwisho katika EPL #GGMU
Baada ya Ushindi wa Ugenini walioupata Vinara wa Ligi kuu nchini England, David De Gea amefikisha mechi sita (6) akicheza mfululizo katika ligi bila ya kufungwa goli lolote.
Mara ya mwisho De Gea kufungwa ilikua ilikua dhidi ya Southampton Old Trafford Tarehe 30 January 2013 goli likifungwa na Jay Rodriguez.
Dakika 633 ambazo De Gea amezifikisha ni nusu ya rekodi iliyowekwa na mkali mwingine wa Man United Edwin Van Der Sar ambaye alicheza dakika 1,311 bila kufungwa goli lolote katika EPL
<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
SAM CHICHARITO ameandika
**FACT............. FACT............... FACT.............. FACT............. FACT..........**
BAADA YA MECHI ZA JANA KATIKA LIGI KUU ENGLAND MAN UNITED INAONGOZA KWA POINT 15 KILELENI NA HII NDIYO HALI HALISI KWA SASA.
- MANCHESTER CITY - 15 points nyuma ya Man United{ Man United afungwe mechi 5 na kudroo 1 ili City iweze kukaa juu katika msimamo wa Ligi}
- TOTENHAM HOTSPURS - 20 point Nyuma ya Man United {United afungwe mechi 7 ili Spurs iweze kukaa juu katika msimamo wa ligi}
- CHELSEA- 22 point nyuma ya Man United {United afungwe mechi 8 ili Chelsea iweze kukaa juu katika msimamo}
- ARSENAL - 24 points nyuma ya Man United{United afungwe mechi 8 na kudroo 1 ili Arsenal iweze kuongoza ligi}
- EVERTON -26 points Nyuma ya Man United {United afungwe mechi 9 ili Everton waweze kukaa juu katika msimamo wa Ligi}
- LIVERPOOR- 32 points nyuma ya Man United {United afungwe mechi10 ili kuwaruhusu wao wakae juu katika ligi}
ZIMEBAKI MECHI 8 MPAKA KUMALIZIKA KWA LIGI HII INA MAANA:-
- Man United Ikishinda mechi 3 na kudroo 1 Man CITY hawezi kuwa bingwa {fact}.
- Man United Ikishinda mechi 1 na kudroo 1 Spurs hawezi kuwa bingwa {fact},
- Man United Ikishinda mechi 1 tu Chelsea hawezi kuwa bingwa {fact}.
- Arsenal, Everton, Liverpool hawawezi kuwa mabingwa hata kama Man United wakipoteza mechi zote zilizobaki {facts}
In short MANCHESTER UNITED ANATAKIWA ASHINDE MECHI NNE (4) TU KATI YA NANE (8) ZILIZOBAKI ILI ATANGAZE UBINGWAA.
GGMU-20 {PREMIER LEAGUE WINNER'S MSIMU WA 2012/2013 NI MANCHESTER UNITED (facts)
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
SULEIMAN DONNA JR amepost picha hii
Picha hii inaonyesha Umiliki wa mpira waliokua nao Arsenal katika mechi ya Nyumbani Ligi kuu England dhidi ya Reading na Arsenal kuibuka na Ushindi wa goli 4-1 magoli yakifungwa na Gervinho 11', Carzola 48', Giroud 67' na Arteta 77' kwa penati wakati lile la Reading likifungwa na Hal Robson-Kanu
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
AGUU X AGUSTO ameandika
......... Bayern Munich 9-2 Humburg SV.
Magoli manne (4) ya Claudi Pizzaro, mawili (2) ya Arjen Robben huku Xherdan Shaqiri, Bastian Schweinsteiger na Frank Ribery kila mmoja akifunga goli moja yalitosha kutoa kipigo cha "mbwa mwizi" cha magoli 9-2 ushindi unaowaweka juu kwa points 20 katika kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa Bundesliga huku zikiwa zimebaki mechi 7 kumalizika kwa msimu na kama Bayern wataibuka na ushindi wikiendi Ijayo ugenini dhidi ya Eintracht Frankfurt basi watatawazwa mabingwa wa Bundesliga.
Ushindi huu ni onyo kwa Juventus watakapokutana Jumanne hii katika ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
KHADIJA LIGANGA ameandika
Nimeipenda sana hii!
ReplyDeleteAbel nadhani hii itatusaidia sana kupunguza zile pp
Delete