NDANI YA UKUMBI WA MALKIA NI NGUMU KUTAMBUA NANI ATAOA BINTI MREMBO WA KIFARANSA

May mwaka huu Ndani ya ukumbi wa malkia pale jijini London kutakua na bonge la pati ya harusi ya Binti wa kifaransa huku Mtoto wa Malkia (Howard Webb) pengine akawa mshereheshaji mkuu (MC) katika tafrija hiyo ambayo bahati mbaya malkia ameshindwa kumtoa mwanae yeyote kwakua wanawe wote wanaonekana hawajapevuka kuoa binti huyu mrembo toka Ufaransa.
Badala yake malkia ametoa ukumbi ili "waliopevuka waoe"
Tunaizungumzia Ligi ya Mabingwa Ulaya hapa hasa hatua hii ya Nusu fainali na kuelekea fainali pale katika uwanja wa Wembley.


>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ya mwaka huu imetenda haki katika ulimwengu wa soka kwani Timu zote zilizoingia hatua hii ni zile ambazo kweli zinafanya vizuri  na zinaonekana zipo vizuri sio tu katika michuano hiyo tu lakini hata ligi za nyumbani. Hii ni tofauti na msimu uliopita ambapo Bingwa Chelsea alifanya vibaya katika ligi ya nyumbani.
Barcelona na Real Madrid kutoka Hispania katika La Liga wanakutana na Borussia Dortmund na Bayern Munich kutoka Ujerumani katika Bundesliga
 




Timu hizi zinafanana katika misimamo ya ligi zao Kwani wakati Bayern Munich wameshachukua ubingwa kwa tofauti ya point 20 toka kwa Burussia Dortmund waliokua mabingwa watetezi watakutana na  Barcelona ambao wanaongoza La liga kwa tofauti ya point 13 dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid na ni miujiza tu inahitajika hapa ili Barcelona akose ubingwa wa La liga msimu huu.
Borussia Dortmund ambao wameshapoteza ubingwa wao watakutana na Real Madrid ambao nao wanatarajia kuupoteza ubingwa wao msimu huu  

Hii ni kusema sasa Real Madrid, Borussia Dortmund, Bayern Munich na Barcelona timu hizi zote zina kariba ya kuwa mabingwa wa Ulaya msimu huu.

HALI IKOJE BAADA YA RATIBA KUTOKA


                            BARCELONA v/s BAYERN MUNICH

Ni sawa na kusema Mabingwa wa La liga wakipambana na mabingwa wa Bundesliga kwani Bayern Munich kashachukua ubingwa huku Barcelona akiukaribia ubingwa. Laiti kama Mechi hizi zingechezwa msimu ujao tungeweza kumshuhudia kocha aliyeipatia mafanikio makubwa Barcelona ndani ya muda mfupi, Pep Guadiola akirudi kupambana dhidi ya timu yake ya zamani kwani tayari ameshasaini mkataba wa kuifundisha Bayern Munich Msimu ujao.
              BAYERN MUNICH


Chini ya kocha Jupp Heynckes ilianza safari yake katika kundi F pamoja na Valencia, Bate, LOSC ikiibuka kinara wa kundi hilo kwa kujikusanyia pointi 13 sawa na Valencia. ikatinga 16 bora na kuiondosha Arsenal kabla ya kuitupa nje Juventus katika Robo fainali.

Ikichagizwa na wachezaji wenye uzoefu wa michuano mikubwa na hasa wengi waliofika katika fainali ya kombe hilo  msimu uliopita inaweza ikawa pia ni chachu kubwa ya wao kushinda sio tu kwa Nusu fainali hata Fainali.
Huku Ikiwa imetangazwa mapingwa wa Bundesliga kwa msimu huu ni timu pekee ambayo mpaka sasa inawania vikombe vitatu vikubwa barani ulaya. Timu hii imekitoa kigogo cha Ulaya na Italia Juventus kwa ushindi mpana wa jumla ya magoli 4-0 na kuifanya timu bora zaidi kuingia hatua hii kwani haijafungwa goli lolote hatua ya Robo Fainali na hii ni kusema ina washambuliaji wakali na beki bora kabisa.
Joseph Barton (Joe Barton) mchezaji wa QPR anaekipiga katika klabu ya Marseille ya Ufaransa kwa mkopo aliandika hivi katika Ukurasa wake wa Twita
"Ushujaa kutoka kwa PSG, Hawajafungwa katika mechi mbili dhidi ya Barca ni bahati mbaya tu wametolewa ila hii ni ishara tosha kama ligi ya Ufaransa inakuja kwa kasi. Bado natabiri kama Bayern Watachukua ubingwa"

                                                  BARCELONA


Barcelona ambayo inataka kuudhihirishia Ulimwengu kama wao bado ni timu bora duniani huku ikiwa na point 13 katika uongozi wa La Liga
Hawakuonyesha makali yao katika Ligi ya Mabingwa msimu huu kwa kukubali kufungwa na  Celtic katika hatua ya makundi kabla ya kupoteza San Ciro japokua walijikwamua na kushinda mechi ya marudiano pale Nou Camp. Balaa likaja katika hatua ya Robo fainali ambayo kama si faida za magoli ya ugenini basi Barcelona ingekua pabaya kwani mwisho wa siku matokeo ya jumla yalikua 3-3 na Barca kupita hatua hiyo ya Robo fainali kwa sheria za magoli ya ugenini.

Chini ya Tito Vilanova Barcelona hii ianaonekana si lolote si chochote ukilinganisha na ile ya Pep Guadiola japokua wengi bado tunaamini wanaweza kuvuka hatua hii hasa wakichagizwa na uwepo wa Messi,Xavi na Iniesta kwani uwepo wao tu mara nyingi huogopesha timu pinzani na kupotea mchezoni ila wana beki mbaya ambayo ina kazi kubwa kuhimili mikiki ya washambuliaji wa Bayern.
 

BORUSSIA DORTMUND v/s REAL MADRID.

Hawa walikutana kwenye hatua ya makundi katika kundi D lililojulikana kama kundi la Kifo likizijumuisha pia Man City na Ajax.

 

                                                   DORTMUND

Mabingwa wa Ulaya mwaka 1997 na bingwa mtetezi wa Ligi ya Ujerumani Bundesliga. Kama unataka soka safi la kitabuni basi hapa ndo nyumbani kwake.
Dortmund ndo timu pekee katika michuano ya mwaka huu ambayo haijawahi kufungwa mchezo wowote katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ikiongozwa na viungo wadogo,waongo Mario Gotze na Marco Reus huku babu mkongwe wa Kipoland Jakub Blaszczykowiski akisimama nyuma yao kule mbele yuko Robert Lewandonski.
 
Hapo ndipo Joseh Mourinho na kina Khedira wake wanapoishiwa nguvu.
Wakitumia Uwanja wa Signal Iduna wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 80,000 ni mara chache sana timu pinzani zinatoka salama hapo
 
Dortmund ni aina ya timu ambazo huwa zinapitia kipindi fulani kizuri, ni mfano wa ile Porto ya Mourinho au Ajax ya muongo mmoja nyuma.
.
                                                        REAL MADRID


Real madrid Imetinga hatua hii ikiwa chini ya kocha mwenye mafanikio katika michuano hiyo kwani Joseh mourinho anaungana na Sir alex Ferguson kufikisha nusu fainali ya 7 huku akisaka ubingwa wa 3 akiwa na klabu tatu za ligi 3 tofauti barani Ulaya.
Ikiwa na Mkali wa mabao Cristiano Ronaldo ambaye mpaka sasa katika mechi 10 za michuano hiyo  amefunga magoli 11,Real Madrid, Mabingwa wa kihistoria wa klabu bingwa Ulaya ndiyo mababa wa klabu bingwa Ulaya wakichukua kombe hilo mara 9 japo wana ukame wa kufika fainali na kuchukua kombe hili kwa muda mrefu sasa.

Real Madrid wana kila sababu ya kuchukua kombe hili wakiwa na kikosi kilichokamilika  na kocha mwenye mafanikio katika michuano hiyo na hasa kwa Cristiano Ronaldo ambaye atataka kuudhihirishia uma kama yeye anapaswa kua mchezaji bora wa dunia

Madrid vs Dortmund si mechi ya kukosa hasa ukitaka kuwaangalia  mafundi wa Ujerumani Gotze na Reus wakati huku kwingine wapo Ozil na Khedira.
 
Ni timu zinazojuana vizuri, na kutokana na kujuana huko ndipo ninapopata jeuri ya kumpa credit The Special One, Jose Mourinho wa Real Madrid kutinga fainali.

Siyo rahisi hata kidogo Mourinho kuendelea kunyanyaswa na Dortmund kwenye hatua hii. Mourinho ni mtaalamu wa kuzitafutia timu dawa.

........TIMU IPI UNADHANI ITAIBUKA BINGWA WA MSIMU HUU?

HAKIKA 
Hakutakuwa na mchezo wa kukosa hapa. TuNawatakia wapenda soka burudani njema.


........Imeandaliwa kwa pamoja na

Abel Chimwejo, Allen Kaijage, Edo Daniel Chibo na Richard Leonce Chardboy wote hawa kutoka katika group la Wapenda Soka(Kandanda) katika ukurasa wa Facebook

5 comments:

  1. Hii dunia nzima... imekaa poa sana

    ReplyDelete
  2. Hakika nusu fainali ya msimu huu imetenda haki!

    ReplyDelete
  3. tena imetenda haki sana hapo wote wanajua ila mi Nawapa bayern 90% wanabeba ndoo ~ edo

    ReplyDelete
  4. Mshind kati ya RMFC na Dortmund, me nampa nafasi kubwa sana. Nataman Champions league ingekua pia na mshnd wa pili.
    CHARDBOY

    ReplyDelete
  5. kura yangu inaenda kwa BAYERN MUNICH.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.