MIWANI PANA YA EDO ~ MATOKEO YA SARE YA AZAM FC NYUMBANI NANI ALAUMIWE?


                          •••• AZAM FC 0-0 FAR RABAT ••••

AZAM FC


                                 NILICHOKIONA

Azam fc walicheza kiuoga na mara nyingi waliiga mchezo wa Waarab bila kuelewa kama wao ndo walikua nyumbani hawakuonyesha kabisa kama walikua wanatafuta ushindi hata pale ambapo Kipre Tchetche alijaribu na kugonga mwamba ilikua ni kati ya nafsi chache walizozitengeneza na laiti kama wangetengeneza nafasi nyingi kama zile basi matokeo mazuri yangeweza kupatikana.

UDHAIFU WA AZAM FC KATIKA MECHI YA JANA
 
                             SAFU YA ULINZI
Iliongozwa na Mwatika,Himid Mao na Waziri Salum ilikua makini kuondoa hatari zote tatizo likawa pasi zisizo na macho zilizoishia katika miguu ya Waarabu pia beki namba mbili na tatu walikua wakicheza kama wale mabeki wa zamani  kwani nilitegemea kuwaona mabeki wa pembeni wakipandisha mashambulizi kama mawinga hivyo kuwapa nafasi mawinga kuingia kati na kuongeza mashambulizi hii ni aina ya mabeki kama Rafael wa Man United au Leyton Baines wa Everton najua nikisema hivi mshkaji wangu Abel Chimwejo anajua nini namaanisha
Aina ya mabeki kama Nsajigwa hawana nafasi siku hizi nadhani hapa ndo naona umuhimu wa Morad,Nyoni na Agrey ambao walisimamishwa

SAFU YA KIUNGO

... Mara nyingi kiungo ndo huwa muhimili mkuu wa timu kupata na katika eneo hilo Kipre Balou na Sure boy ambao ndo walimiliki dimba la kati walionekana kabisa kushindwa kutofautisha "a must win match" na "just a match" kwani mara nyingi badala ya kupeleka mipira mbele Sure Boy alikua akizunguka na kurudisha mpira nyuma jambo lililowapa faida waarabu kwani waliweza kujipanga na kuhakikisha hawaruhusu goli.

Kuna nafasi nyingi sana Kipre Tchetche alikua akiomba lakini Sure Boy akawa anazunguka na kurudisha mpira nyuma badala ya kumpitishia Kipre ambaye ni mchezaji mwenye nguvu,chenga na uwezo mkubwa wa kufunga.
Hii pia alikua akiifanya Kipre Balou kwani alikua mzuri sana kutibua mipango ya Waarabu lakini pasi zake nyingi zilipotea yani ni pasi ambazo hazikua na malengo.

Hapo ndo nikawa namkumbuka marehemu Patrick Mafisango au Haruna Niyonzima wa Yanga ambao ni msaada mkubwa wa timu zao katika kutafuta ushindi kwani hupeleka mashambulizi mbele hata kufunga magoli na aina hii ya viungo utaikuta pia kwa Jack Wilshere wa Arsenal au Andreas Iniesta wa Barcelona. Nadhani mshkaji wangu Richard mzee wa THE GUNNING MACHINE anaelewa nini namaanisha hapa.


 SAFU YA USHAMBULIAJI

 Safu ya ushambuliaji ya Azam ilikua haina mipango kabisa sijajua kama ndo walivyofundishwa au hapana kwani safu hii iliongozwa na Kipre Tchetche aliyecheza namba 11, Mcha Hamisi "Viali" aliyecheza 7 na pale kati alisimama John Bocco "Adebayor"

Kutoka katika jukwaa la simba zilisikika kelele nyingi za kumtaka kocha kumtoa Mcha Hamis kwani mara nyingi alikua anapoteza malengo ya timu na kuharibu nafasi chache zilizopatikana
Mshambuliaji huyo kutoka Zanzibar hakua na mbinu na mara nyingi alionekana kuchoka baadae nafasi yake ikachukuliwa na Gaudence Mwaikimba mabye kwangu mimi naona hastahili kucheza klabu kubwa kama Azam

Washambuliaji wa Azam walikosa maamuzi kama aliyonayo kiungo mshambuliaji wa simba Amiri kiemba kwani Tchetche muda wote alikua amekaa upande wa kushoto wakati angeweza kuingia kati na kuruhusu mabeki kupanda na yeye akaongeza nguvu katika ushambuliaji muda ukayoyoma na Adebayor kwakua alibanwa vilivyo basi ikaishia ilipoishia

           NAFASI YA AZAM FC KUSONGA MBELE

Wametuaminisha kama wanaweza kufanya vizuri wakiwa ugenini kuliko nyumbani hasa baada ya kuibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Al Nasr ya Sudan kusini wakati walishinda 3-1 hapa nyumbani kabla ya kuifunga Barack Young Controllers ya Liberia goli 2-1 ugenini wakati hapa nyumbani wakaja kutoka sare.

Azam FC Jana imevunja rekodi iliyowekwa na Simba SC wakati walipofika fainali za kombe la CAF kwa kucheza Mechi tano za awali bila kupoteza, Hadi sasa Azam FC imecheza Mechi 5, imeshinda 3 na kwenda sare 2

Ushindi wowote au sare ya magoli itawavusha Azam katika hatua hii na kuingia hatua ya 16 bora
Naamini kocha atakua ameyaona mengi na atayarekebisha ila haya ndo niliyoyaona na miwani yangu pana.


.......Kama vipi next time
www.facebook.com/edodanielchibo

4 comments:

  1. Me nilikuambia edo, Mabeki wa pembeni siku hz ndo wale mawinga teleza, hawa akina Mbuyu twite watafute nafasi nyingine, nilikua cjui kwamba hata Abel alishakuambia.
    CHARD

    ReplyDelete
  2. Niliangalia first half tu jana. Sure Boy alikua anacheza kama Abdulhalim Humud, asipoangalia nae atapitwa na wakati. Siku hz visheti siyo mabosi, ubosi umehamia kwa namba 6 ambae anafanya kazi ya kupunch na kubalance team kwa kuhold mipira, visheti siku hz wako sharp manake wanakabwa sana.

    ReplyDelete
  3. Nina wasiwasi na kitu kimoja tu kule Rabat,fitna.Naamini hawa jamaa wanajua umuhimu na maana ya mashindano haya.Sidhani kama watafanya masikhara au uzembe wa aina yeyote ile.Ninaamini AZAM wanaweza kufanya vizuri ila tu kama watajiandaa kukabiliana na hali yeyote itakayojitokeza na hasa FITNA.

    ReplyDelete
  4. kOCHA NATAKIWA KUJIPANGA KWA NAMNA YOYOTE PALE MOROKO WAPATE JAPO SARE ~ Edo

    ReplyDelete

Powered by Blogger.