LIGI KUU ENGLAND SASA NI MAKUNDI MAWILI YALIYOBAKI
Baada ya kuwafunga Aston Villa 3-0 katika uwanja wa Old Trafford, Man United waliweza kutawazwa mabingwa wapya wa ligi kuu England wakiwavua rasmi ubingwa Man city walioonja taji hilo msimu uliopita.
Wakati bingwa wa ligi kuu England msimu huu wa 2012/13 akiwa ameshajulikana sasa, utamu wa ligi hiyo pendwa bado haujaisha na umejigawa katika makundi mawili.
Wakati bingwa wa ligi kuu England msimu huu wa 2012/13 akiwa ameshajulikana sasa, utamu wa ligi hiyo pendwa bado haujaisha na umejigawa katika makundi mawili.
(a) KUNDI LA KWANZA: WABABE WA LIGI
NAFASI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA (TOP FOUR)
Hili ni kundi la kwanza likiongozwa na Bingwa ambaye ni Man United mwenye point 84 na kujihakikishia nafsi ya kucheza katika ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya makundi msimu ujao huku Liverpool iliyo na point 51 katika nafasi ya 7 inashika mkia katika kundi hili linaloonekana ni la timu maarufu zenye mashabiki wengi sio tu England bali hata duniani kote
Kundi hili kila timu ina nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kama ikicheza vyema na kushinda michezo yote iliyobaki
Kwani aliyekua bingwa mtetezi Man City anashika nafasi ya pili akiwa na points 68 zinazoweza kufikiwa na timu yoyote hapo katika timu 5 zilizobaki katika kundi hili.
Nafasi ya 3 inakamatwa na Arsenal wenye point 63, wakati Chelsea wako katika nafasi ya 4 wakiwa na points 62 yani ni point moja mbele ya Spurs yenye point 61 katika nafasi ya 5 huku Everton wakikamata nafasi ya 6 wakiwa na points 56.
Man City, Man United,Arsenal na Chelsea ndo walikua wawakilishi wa England katika michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu na sasa tuna timu nyingine ambayo mwaka jana ilipokwa nafasi yake na Chelsea walioshika nafasi ya 6 katika ligi lakini wakashinda ligi ya mabingwa Ulaya hivyo kuchukua nafasi ya timu hiyo namaanisha Tottenham Hotspurs..
KWA KIFUPI HIZI NDO MECHI ZILIZOBAKI KWA TIMU ZA KUNDI HILI
- MAN CITY
Man City haweza kubweteka na points alizonazo katika msimamo kwani timu yoyote katika kundi hili inaweza kuzifikia isipokua Liverpool na hizi ni mechi zilizobaki kwa Man City
- Man City vs West Ham (H)
- Man City vs Wes Brom (H)
- Swansea vs Man City (A)
- Reading vs Man City (A)
- Man City vs Norwich (H)
- ARSENAL
Kwa upande wa Arsenal, wao wapo katika nafasi ya tatu, wakiwa na pointi 63, pointi 5 tu nyuma ya Man City wanaokamata nafasi ya pili.
Haizungumzwi sana, lakini kwa michezo iliyosalia, kama Arsenal wakichanga vyema karata zao wanaweza hata kumaliza katika nafasi ya 2 iwapo Man City watateleza.
Lakini Arsenal wanaweza kuwa na kibarua kigumu kutokana na timu watakazokutana nazo kuwa katika lile kundi lingine la kukwepa kushuka daraja na hizi mara nyingi huwa mechi ngumu sana japokua Profesa Wenger anajua zaidi nini anapaswa kukifanya kulinda heshima ya Timu Mechi zilizosalia kwa Upande wa Arsenal ni :-
- Arsenal vs Man United (H)
- QPR vs Arsenal (A)
- Arsenal vs Wigan (H)
- Newcastle vs Arsenal (A)
- CHELSEA
Hizi ndo mechi walizobakiza :-
- Chelsea vs Swansea (H)
- Man United vs Chelsea (A)
- Chelsea vs Tottenham Hotspurs (H)
- Aston Villa vs Chelsea (A)
- Chelsea vs Everton (H)
- TOTENHAM HOTSPURS
Ukiwatazama Tottenham HotSpurs ambao walitoa kichapo cha mabao 3-1 kwa aliyekua bingwa mtetezi Man City wiki iliyopita, utagundua kuwa wakali hao wa London wana uwezo wa kumfunga yeyote katika mechi zao zilizobakia.
Wanashika nafasi ya 5 kwenye msimamo hivi sasa, wakiwa na pointi 61. Pointi 1 nyuma ya Chelsea wenye pointi 62 na pointi 2 nyuma ya Arsenal wenye pointi 63 lakini wakiwa na mchezo mmoja zaidi ya Arsenal.
Hizi ndo mechi zilizosalia kwa Tottenham Hotspurs
- Wigan vs Tottenham Hotspurs (A)
- Tottenham Hotspurs vs Southampton (H)
- Chelsea vs Tottenham Hotspurs (A)
- Stoke City vs Tottenham Hotspurs (A)
- Tottenham Hotspurs vs Sunderland (H)
Hiyo yote ni michezo migumu kwa sababu timu kama Wigan na hata Stoke, bado hazipo salama katika msimamo. Lakini kiwango cha Tottenham hivi sasa kinaridhisha na siyo ajabu wakashinda michezo hiyo.
Hizi ndo timu ambazo tunazipa nafasi ya kuwania zile nafasi 4 za juu japokua Everton na liverpool nao wamo katika kinyang'anyiro hicho.
(b) KUNDI LA PILI : KUNDI LA KIFO(MKASI WA KUSHUKA DARAJA)
Kundi hili linaongozwa na Wes Bromwich Albion wenye point 45 wakikamata nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi huku Aston Villa wenye point 34 wakiwa nafasi ya 17 yani wanachungulia mstari wa kuteremka daraja lakini ukiangalia kwa makini hapo kuna tofauti ya point 11 ambazo zimebebwa na timu 8 toka nafasi ya 8 mpaka nafasi ya 17
Reading wanakamata mkia wa kundi hili wakiwa na point 24 sawa na QPR huku Wigan wakiwa nafasi ya 18 na point zao 31 japokua Wigan wanaonekana bado wako katika hali nzuri ya kujiokoa kushuka daraja kwani wana mchezo mmoja pungufu na kama wakishinda huo basi watalingana na Aston Villa huku Newcastle ambao msimu uliopita walimaliza wakiwa nafasi ya Tano wana point 37 sawa na Stoke na Sunderland.
Yani kwa kifupi hapa timu yoyote inaweza kuungana na QPR na Reading kushuka daraja japokua lolote laweza kutokea.
Katika Kundi hili ipo Southampton ambayo kwasasa inashika nafasi ya 12 ikiwa na point 39 point tatu nyuma ya West Ham wanaokamata nafasi ya 10. Hii ni timu ambayo kwa kipindi kirefu ilikamata mkia wa Ligi kuu msimu huu wakipanda daraja pamoja na Reading na West Ham lakini sasa wako nafasi nzuri na hii ni baada ya kufanya mabadiliko ya kocha katikati ya msimu
MECHI ZILIZOBAKI KWA TIMU ZINAZOKIMBIA KUSHUKA DARAJA MSIMU HUU
- READING
Reading imebakiza mechi hizi :-
- Reading vs QPR (H)
- Fulham vs Reading (A)
- Reading vs Man City (H)
- West Ham vs Reading (A)
- QUEEN'S PARK RANGERS (QPR)
Ikumbukwe msimu uliopita QPR ilikua chupuchupu washuke daraja na wakaja kujiimarisha msimu huu kwa kufanya usajili wa maana lakini matokeo yake ni mabaya kuliko msimu ulioisha.
QPR Imebakiza mechi zifuatazo:-
- Reading vs QPR (A)
- QPR vs Arsenal (H)
- QPR vs Newcastle (H)
- Liverpool vs QPR (A)
- WIGAN ATHLETIC
Msimu uliopita walifanya vizuri katika mechi za mwisho na kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya 15 juu ya Aston Villa waliomaliza katika nafasi ya 16.
Wigan tayari wamekata tiketi ya kucheza fainali ya kombe la FA ambapo watakutana na Man City mwezi ujao.
Mechi zilizobaki kwa Wigan kuweza kubaki katika Ligi ni :-
- Wigan vs Tottenham (H)
- WBA vs Wigan (A)
- Wigan vs Swansea (H)
- Arsenal vs Wigan (A)
- Wigan vs Aston Villa (H)
Hiyo mechi ya mwisho inaweza kua mechi bora kabisa msimu huu kama msimamo utaendelea kuabaki hivi mpaka mwisho.
- ASTON VILLA
Hali si nzuri kwa timu hiyo sasa na kama hawatajitahidi michezo iliyobaki basi itakua imeshuka daraja msimu huu kwani wana points 34 wakiwa wameshacheza mechi 34 point 3 mbele ya Wigan na point 3 nyuma ya Newcastle, Stoke na Sunderland walio na points 37.
Mechi zake za Mwisho ziko kama Ifuatavyo:-
- Aston Villa vs Sunderland (H)
- Norwich vs Aston Villa (A)
- Aston Villa vs Chelsea (H)
- Wigan vs Aston Villa (A)
Haya ndo makundi mawili ambayo yameigawa ligi kuu nchini England tukielekea katika hatua za mwisho.
Je wewe kama Mpenda Soka unaweza kutabiri watakaopenya Nne bora (Top Four) na wale watakaoshuka daraja?
Na kitu gani kinakufanya ufikiri unachofikiri?
""""""""""" Imeandaliwa kwa pamoja na Richard Leonce Chardboy na Edo Daniel Chibo kutoka katika Group makini la Wapenda Soka (kandanda) katika Ukurasa wa Facebook
Sioni qpr atakavopenya hapo. Alishindwa kutumia mechi zake zilizokuwa rahisi. CHARD BOY
ReplyDeletekama QPR atashinda kesho na Sunderland akadraw au kumfunga Villa bado wamo aisee
ReplyDelete...Edo