WEKUNDU WA MSIMBAZI

SABABU 6 ZA KUAMINI SIMBA LEO INAWEZA KUSHINDA DHIDI YA RECREATIVO DE LIBOLO YA ANGOLA.
 
Simba SC
 
 Mabingwa wa Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba wanashuka jioni hii katika uwanja wa Estadio de Libolo nchini Angola kuwavaa mabingwa wa Angola Recreativo de Libolo katika pambano la marudiano la ligi ya Mabingwa Barani Afrika huku wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa goli moja katika mchezo uliopigwa wiki mbili zilizopita jijini Dar Es Salaam
Wengi wa mashabiki hawakipi nafasi ikosi hicho cha Simba kuwez kufanikiwa kuvuka hatua hii lakini makala ya WEKUNDU WA MSIMBAZI Inachambua baadhi ya sababu za kuamini leo Simba itashinda.
 
1. MASHABIKI KUTOIPA NAFASI
 
 
Watanzania wengi hasa wasiokua mashabiki wa Simba na hata wale mashabiki wa Simba ambao hawakiamini kikosi chao wanaamini leo Simba watafungawa goli nyingi lakini wachache tunaamini Simba leo ina kila sababu ya kushinda kwani haina ile presha ya mashabiki wake hivyo wanaingia uwanjani wakiwa hawana mchecheto kwani kwa matokeo yoyote yale hasa wakifungwa hakuna atakaeshangaa hivyo wachezaji watacheza kwa bidii kutaka kuwadhhirishia mashabiki kuwa bado wamo na wanaweza
 
2. UZOEFU WA WACHEZAJI
Felix Sunzu ambaye hakuwepo katika kikosi kilichofungwa wiki mbili zilizopita anatarajia kuanza leo japokua atakosekana Haruna Moshi Boban ambaye hakusafiri na timu kwani ni mgonjwa.
Kikosi cha Simba kimesheheni wachezaji wenye uzoefu na michuano ya kimataifa hapa nawazungimzia golikipa Juma Kaseja,Mrisho Ngassa,Juma Nyosso, Amir Maftah, Shomari kapombe,Mwinyi Kazimoto,Felix Sunzu, Masoud Chollo na Redondo hawa wataongezewa nguvu na vijana kama Chanongo, Mkude, Seseme na Singano.
 
Uzoefu wa wachezaji katika kikosi chaSimba itawasaidia kujua nini wanatakiwa wafanye wakiwa ugenini na wapo ambao walikuwepo katika historia za kushinda katika ardhi ya ugenini.
 
3. HISTORIA NZURI KATIKA MICHUANO YA KIMATAIFA
 
Kila mmoja anakikumbuka kikosi kilichoitoa Zamalek ya Misri waliokua mabingwa wa Afrika mwaka 2003. Baada ya kufungwa goli moja katika uwanja wa Taifa wa zamani ( Uwanja wa Uhuru kwa sasa) Simba waliweza kuwafunga Zamalek goli moja katika mchezo wa marudiano na kupelekea kupigiana penati hatimaye Simba kuibuka kidedea huku shujaa akiwa Juma Kaseja ambaye leo ataanza kama golikipa namba moja.

Hii haikua mara ya kwanza lakini ni mara nyingi Simba imekua ikifanya vizuri katika mechi za kimataifa.
 
4. AHADI YA FEDHA
 
Zipo taarifa kama Bosi wa Friends of Simba Zacharia Hanspope amewaahidi wachezaji milioni 10 kama watashinda na kusonga mbele. Hii ni hamasa kubwa kwa wachezaji wetu kwani itawapa moyo na ari ya mchezo hivyo kua na kila sababu ya kufanya vizuri.
 
5. HUDUMA BORA WALIZOPATA
                                                                   FC LIBOLO
Tumezoea kila linapokuja swala la mechi za ugenini katika michuano ya kimataifa basi ni mateso kwa timu zetu kwani hupelekwa katika hoteli mbovu zenye huduma mbovu lakini hivi sasa taarifa zinasema Simba wamepata kila aina ya huduma bora hii itawajenga wachezaji na kuwafanya kujisikia wako nyumbani.
 
6. KUFUNGWA MECHI YA KWANZA
Ushindi wa goli moja walioupata Libolo walipokuja nchini unaweza kuwafanya wakadhani kua wameshamaliza kazi na hii itawafanya Simba kucheza kwa umakini mkubwa na kuweka akilini kama wana deni hivyo wapigane kufa na kupona

 
>>>> Yote kwa yote ni dakika 90 zitakazoamua nini hatma ya Simba katika michuano hii
 
MUNGU IBARIKI SIMBA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
SIMBA TAIFA KUBWA DAIMA
 

1 comment:

  1. kama ilikuwa unaipa nafasi simba amini ulikuwa unajidanganya kwa sasa baada ya kaburu kuondoka ndo naamini hii makala ungeiandika basi tungeweza kuona maajabu, lakini team imeenda na mzee hanspope peke yake ulitegemea ishinde..? hata siku moja baada ya mabadiliko yalofanyika jana sasa utaskia simba wameshinda mechi zote zilizobaki ndo ugundue upuuzi wa mpira wetu

    ReplyDelete

Powered by Blogger.