Ryan Joseph Giggs ndo jina la Mkongwe huyu raia wa kisiwa cha Wales nchini Uingereza ambaye amezaliwa Tarehe 29 November 1973 (miaka 39) katika mji wa Cardiff huko Wales.
Alijiunga na Man United na kusaini mkataba wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17 tu mnamo tarehe 29 Novemba 1990 siku ya "birthday" yake.
Giggs alicheza mechi yake ya kwanza katika ligi akiwa na jezi ya Man United dhidi ya Everton tarehe 2 March 1991 yani siku kama ya kesho miaka 22 iliyopita akichukua nafasi ya beki Dennis Irwin ambapo Man United iliambulia kichapo cha 2-0.
Tangu wakati huo amekua mhimili mkubwa wa United hasa katika nafasi ya Winga wa Kushoto na kujipatia mafanikio kadhaa.
Mafanikio hayo ni pamoja na kushinda ubingwa wa Ligi mara 12, Kombe la FA mara 4 na kombe la ligi mara 3 huku akishinda ubingwa wa Ulaya mara 2.
Mafanikio hayo ni pamoja na kushinda ubingwa wa Ligi mara 12, Kombe la FA mara 4 na kombe la ligi mara 3 huku akishinda ubingwa wa Ulaya mara 2.
Taarifa zimeripoti leo kama Giggs amekubali kuongeza mkataba klabuni United ambao ni wa mwaka mmoja zaidi na kutupilia mbali zile habari zilizoripotiwa kama angestaafu mwishoni mwa msimu huu. Wajuzi wa Mambo wanasema ataendelea mpaka Ferguson atakapostaafu japokua Giggs pia anaendelea na kozi za ukocha ndipo ninapoamini kama anaweza kua mbadala wa Ferguson pia kama Kocha hapo baadae.
Giggs Anapaswa kupongezwa kwa kila hali kwani amefikia mafanikio ambayo wachezaji wengi wamekua wakiyaota kwani Tangu March 2,1991 mpaka leo ameshacheza michezo 999 na kama Ferguson atampanga katika mechi dhidi ya Norwich Jumamosi basi atafikisha mechi ya 1000 akiwa na klabu na timu ya Taifa pia atakua amefikisha mchezo wa 931 ndani ya kikosi cha United.
Giggs amecheza misimu 22 ya ligi ya England mpaka sasa na kushinda makombe 34 na ni kati ya wachezaji wachache ambao hawajawahi kupata kadi nyekundu japokua wamecheza michezo mingi.
Giggs pia ni mchezaji pekee katika historia ya klabu za Ulaya ambaye amefunga katika misimu yote 22 aliyocheza katika ligi na katika amefunga mfululizo katika misimu 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
MAAJABU YANAYOFURAHISHA
Ryan Giggs amecheza na wachezaji wengi sana katika misimu 22 aliyoichezea Man United na katika kikosi cha sasa kuna jambo la kushangaza na kufurahisha kwani Wakati Giggs akiichezea United mechi yake ya kwanza katika ligi March 2, 1991
Paul Scholes alikua na umri wa miaka 16
Rio Ferdinand alikua na umri wa miaka 12
Nemanja Vidic ambaye ndo nahodha wa timu hiyo kwa sasa alikua na umri wa miaka 9 sawa na Patrice Evra na Michael Carick.
Robin Van Perse yeye wakati huo alikua na umri wa miaka 7 sawa na Darren Fletcher.
Andes Lindegaard alikua na umri wa miaka 6.
Wakati huo Ashley Young,Antonio Valencia na Wyne Rooney ambao ni tegemeo katika kikosi cha United sasa walikua na umri wa miaka 5 kila mmoja.
Luis Nani na John Evans wao wakati huo walikua na umri wa miaka 4 kila mmoja.
Dunia Inashangaza na miaka inaenda kwa haraka sana kwani Anderson,Chicharito na Buttner wao walikua na umri wa miaka 2 kila mmoja.
Kiungo anayekuja kwa kasi na kuonyesha kama atakua lulu katika kikosi cha United na England, Tom Cleverley, Mjapani Shinji Kagawa na Chriss Smalling wao ndo kwanza walikua na umri wa mwaka mmoja tangu walipozaliwa.
Ben Amos alikua na miezi 11 tangu alipozaliwa
Rafael na Fabio(yuko QPR kwa mkopo) wao ndo kwanza walikua na miezi 8 tu tangu walipozaliwa huko kwao Brazil.
Golikipa namba moja na tegemeo kwa sasa katika Kikosi cha Kwanza cha United David De Gea pamoja na Mshambuliaji chipukizi aliyefunga goli katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora pale katika uwanja wa Santiago Bernabeu, Danny Welbeck wao ndo kwanza walikua na miezi mitatu tu tangu walipozaliwa.
Wapo watu watacheka katika hizi data Lakini ukweli ni kwamba Phil Jones na Nick Powell wao ndo kwanza walikua hawajazaliwa.
Huyo ndo Ryan Giggs Ambaye sisi mashabiki wa United tutaendelea kumwona katika jezi zetu msimu ujao.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
Kwa leo naishia hapa lakini huu ni mwanzo tu katika kuwaletea mengi yahusuyo MANCHESTER UNITED katika kipengele hiki ambacho kwa sasa nimekiita THE TRUE RED DEVILS
kijana umetisha GGMU
ReplyDeleteNa hii ndo The True Red Devils bana tuna mengi sanaya kuzungumzia katika hatua klabu hii
ReplyDeleteLet us join together n produce something good for United fans tena kwa lugha ya Kiswahili