THE GUNNING MACHINE
NAFASI YA ARSENAL NA HARAKATI ZA TOP FOUR.
Mwezi Februari haukua wa kuvutia kwa Arsenal uwanjani. Umeiacha Arsenal kwa mara nyingine ikiwa na nafasi finyu ya kupata kombe.
Nafasi pekee iliyobaki ni ya katika ligi ya mabingwa Ulaya wakiwa na kazi nzito ya kushinda ugenini dhidi ya Bayern Munich.
Japo walishinda mechi zote tatu za ligi zilizopigwa mwezi huu, lakini walifanikiwa kufunga mabao manne tu. Shukrani kwa Santiago Cazorla aliyefunga matatu kati ya hayo.
Kuondolewa na Blackburn Rovers kwenye kombe la FA kunakamilisha usemi wangu kwamba haukua mwezi mzuri.
Vita pekee iliyobakia ni ya kuwania moja kati ya nafasi nne za juu. Ni vita ambayo Arsenal wamezoea kushinda kwa muda mrefu sana.
Unaweza kuiona kama vita ngumu sana msimu huu lakini 'The Gunning Machine' inakuhabarisha kuwa msimu uliopita vita hiyo ilikua ngumu zaidi. Iliwalazimu Arsenal wasubiri kushinda mchezo wa mwisho wa Ligi dhidi ya Norwich ili kujihakikishia nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa.
Msimu huu kunaonekana kuwa na timu nne zinazowania nafasi mbili, yaani nafasi ya tatu na ya nne.
Kuna Tottenham ambao wanashika nafasi ya 3 kwa pointi 51 zikiwa ni pointi 2 mbele ya Chelsea wenye pointi 49 kunako nafasi ya 4.
Nafasi ya 5 inakaliwa na Arsenal wenye pointi 47. Pointi 2 tu nyuma ya Chelsea.
Lakini huwezi kuwatoa Everton pia ambao wana pointi 42. Wana mlima wa pointi 7 tu kutoka kwa anaeshika nafasi ya 4 ambazo zinaweza kupatikana.
The Gunning Machine inaangalia nasasi ya Arsenal katika kinyang'anyiro hicho, hasa katika mwezi ujao wa Machi.
Arsenal wana mfululizo wa mechi ngumu ambazo ni lazima washinde kama kweli wana nia ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.
Watafungua mwezi kwa kucheza na Tottenham jumapili ya Machi 3,2012. Matokeo ya mchezo huu ndiyo yatakayotoa mustakabali wa nafasi ya Arsenal.
Wakishinda watafikisha pointi 50, watakua nyuma ya Spurs kwa pointi 1. Bila kujali matokeo ya Chelsea ambao watakua nyumbani kuwaalika West Bromwich, Arsenal watakuwa na uhakika angalau wa kukaa pointi 1 nje ya 'top four.'
Ugumu wa mechi dhidi ya Spurs ndiyo urahisi wake kwa sababu njia nzuri ya kumshinda mpinzani wako ni kupambana naye.
Chelsea wanaweza kuwatoa Tottenham katika nafasi ya 3 kutokana na ratiba ilivyo. Inaonekana Chelsea watacheza mechi rahisi zaidi ya Spurs.
Baada ya kucheza na Arsenal Machi 3,2012 Tottenham watakuwa wageni wa Liverpool Machi 10 kabla ya kurudi nyumbani kuwapokea Fulham kisha kumalizia mwezi kwa kupambana na Swansea. Baada ya hapo watacheza na Everton, Chelsea na Man City. Mechi ambazo siyo rahisi kushinda zote kwa mfululizo.
Chelsea wao watacheza na West Bromwich nyumbani machi 2 kisha watawafuata Fulham Machi 10 kabla ya kurudi nyumbani kuwaalika West Ham na kumaliza mwezi Na Southampton ugenini. Hivyo Chelsea anaweza kuwa salama kuliko Tottenham kwenye nafasi ya 3.
Nafasi ya Arsenal inaonekana kuwa kwa Tottenham sasa, lakini kama ilivyo kwa Tottenham, Arsenal nao hawana ratiba rahisi. Wana michezo migumu ambayo kama wakifanikiwa kushinda watakua katika nafasi nzuri ya kushinda vita hii.
Baada ya kumalizana na Tottenham ugenini, watarudi nyumbani kuwasubiri Everton. Hii ni mechi ngumu sana, kumbuka katika mzunguko wa kwanza timu hizi zilitoka sare ya bao 1-1. Matokeo ya mchezo huu pia yatatoa mustakabali wa Everton ambao wanaifukuzia Arsenal kwa karibu.
Baada ya Everton, Arsenal wataifuata Swansea. Hakuna asiyejua Swansea ni timu ya aina gani. Kumbuka walimfunga Arsenal ugenini mabao 0-2 katika mzunguko wa kwanza.
Arsenal watarudi nyumbani kukamilisha mwezi wa Machi kwa kuwaalika Reading tarehe 30.
"The Gunning Machine" inajiuliza kama ina risasi za kutosha kukusanya pointi zote 12 za mwezi Machi kama ilivoweza kukusanya zote 9 za mwezi Februari.
Kama lengo hili likitimia, Arsenal wanaweza kuwa salama kwani baada ya Reading, watawavaa West Bromwich, Norwich na Fulham kabla ya kukutana na Manchester UTD.
Imeandikwa na Richard Leonce ChardBoy kutoka wapenda soka (kandanda) group.
Nipate katika chardboy77@yahoo.com
@chardboy77 kwenye twitter.
Na 0658399341
Bale vs Carzola |
Mwezi Februari haukua wa kuvutia kwa Arsenal uwanjani. Umeiacha Arsenal kwa mara nyingine ikiwa na nafasi finyu ya kupata kombe.
Nafasi pekee iliyobaki ni ya katika ligi ya mabingwa Ulaya wakiwa na kazi nzito ya kushinda ugenini dhidi ya Bayern Munich.
Japo walishinda mechi zote tatu za ligi zilizopigwa mwezi huu, lakini walifanikiwa kufunga mabao manne tu. Shukrani kwa Santiago Cazorla aliyefunga matatu kati ya hayo.
Kuondolewa na Blackburn Rovers kwenye kombe la FA kunakamilisha usemi wangu kwamba haukua mwezi mzuri.
Gunner's bullets |
Unaweza kuiona kama vita ngumu sana msimu huu lakini 'The Gunning Machine' inakuhabarisha kuwa msimu uliopita vita hiyo ilikua ngumu zaidi. Iliwalazimu Arsenal wasubiri kushinda mchezo wa mwisho wa Ligi dhidi ya Norwich ili kujihakikishia nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa.
Msimu huu kunaonekana kuwa na timu nne zinazowania nafasi mbili, yaani nafasi ya tatu na ya nne.
Kuna Tottenham ambao wanashika nafasi ya 3 kwa pointi 51 zikiwa ni pointi 2 mbele ya Chelsea wenye pointi 49 kunako nafasi ya 4.
Nafasi ya 5 inakaliwa na Arsenal wenye pointi 47. Pointi 2 tu nyuma ya Chelsea.
Lakini huwezi kuwatoa Everton pia ambao wana pointi 42. Wana mlima wa pointi 7 tu kutoka kwa anaeshika nafasi ya 4 ambazo zinaweza kupatikana.
The Gunning Machine inaangalia nasasi ya Arsenal katika kinyang'anyiro hicho, hasa katika mwezi ujao wa Machi.
Arsenal wana mfululizo wa mechi ngumu ambazo ni lazima washinde kama kweli wana nia ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.
Watafungua mwezi kwa kucheza na Tottenham jumapili ya Machi 3,2012. Matokeo ya mchezo huu ndiyo yatakayotoa mustakabali wa nafasi ya Arsenal.
Wakishinda watafikisha pointi 50, watakua nyuma ya Spurs kwa pointi 1. Bila kujali matokeo ya Chelsea ambao watakua nyumbani kuwaalika West Bromwich, Arsenal watakuwa na uhakika angalau wa kukaa pointi 1 nje ya 'top four.'
Ugumu wa mechi dhidi ya Spurs ndiyo urahisi wake kwa sababu njia nzuri ya kumshinda mpinzani wako ni kupambana naye.
Chelsea wanaweza kuwatoa Tottenham katika nafasi ya 3 kutokana na ratiba ilivyo. Inaonekana Chelsea watacheza mechi rahisi zaidi ya Spurs.
Baada ya kucheza na Arsenal Machi 3,2012 Tottenham watakuwa wageni wa Liverpool Machi 10 kabla ya kurudi nyumbani kuwapokea Fulham kisha kumalizia mwezi kwa kupambana na Swansea. Baada ya hapo watacheza na Everton, Chelsea na Man City. Mechi ambazo siyo rahisi kushinda zote kwa mfululizo.
Chelsea wao watacheza na West Bromwich nyumbani machi 2 kisha watawafuata Fulham Machi 10 kabla ya kurudi nyumbani kuwaalika West Ham na kumaliza mwezi Na Southampton ugenini. Hivyo Chelsea anaweza kuwa salama kuliko Tottenham kwenye nafasi ya 3.
Nafasi ya Arsenal inaonekana kuwa kwa Tottenham sasa, lakini kama ilivyo kwa Tottenham, Arsenal nao hawana ratiba rahisi. Wana michezo migumu ambayo kama wakifanikiwa kushinda watakua katika nafasi nzuri ya kushinda vita hii.
Baada ya kumalizana na Tottenham ugenini, watarudi nyumbani kuwasubiri Everton. Hii ni mechi ngumu sana, kumbuka katika mzunguko wa kwanza timu hizi zilitoka sare ya bao 1-1. Matokeo ya mchezo huu pia yatatoa mustakabali wa Everton ambao wanaifukuzia Arsenal kwa karibu.
Baada ya Everton, Arsenal wataifuata Swansea. Hakuna asiyejua Swansea ni timu ya aina gani. Kumbuka walimfunga Arsenal ugenini mabao 0-2 katika mzunguko wa kwanza.
Arsenal watarudi nyumbani kukamilisha mwezi wa Machi kwa kuwaalika Reading tarehe 30.
"The Gunning Machine" inajiuliza kama ina risasi za kutosha kukusanya pointi zote 12 za mwezi Machi kama ilivoweza kukusanya zote 9 za mwezi Februari.
Kama lengo hili likitimia, Arsenal wanaweza kuwa salama kwani baada ya Reading, watawavaa West Bromwich, Norwich na Fulham kabla ya kukutana na Manchester UTD.
Imeandikwa na Richard Leonce ChardBoy kutoka wapenda soka (kandanda) group.
Nipate katika chardboy77@yahoo.com
@chardboy77 kwenye twitter.
Na 0658399341
Mahesabu mazuri, lakini kweli mnawachezaji wa kutimiza hayo?
ReplyDeleteNgoja tuone..
Kipimo ni mechi ya weekend hii
ReplyDelete