WEKUNDU WA MSIMBAZI

SIMBA KUFANYA VIBAYA KATIKA MICHEZO YAKE,  MCHAWI NANI?



Simba Sc

Ni jumapili nyingine Tamu sana kwa Wapenda Soka kwani kuna mechi nyingi za kuangalia tena nyingine zikiwa zimegongana muda: Man City Wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Etihad waliikaribisha Chelsea wakati huo huo katika Ligi kuu ya VodaCom Tanzania Bara, Mabingwa Watetezi Simba waliikaribisha Mtibwa toka Morogoro:
Uzalendo uliingia katika miwani yangu na kuwasha gari kuelekea Taifa kwa mara nyingine kuiangalia Simba ambayo katikati ya Wiki iliifunga Prisons kule Mbeya nikitegemea timu itakua imebadilika na hapa nilichagizwa na maneno ya kocha mkuu wa Simba Mfaransa Patrick Lewig ambaye alijinadi kwamba ndo ameanza kazi sasa.

Baada ya dakika 90 najikuta niko katikati ya mashabiki wa Simba ambao kila mmoja alikua akizungumza lake wakati upande wa Pili kwa mashabiki wa Yanga walikua wakishangilia na hii ni baada ya Mtibwa Sugar kuifunga Simba goli moja bila.
Nikiwa katikati ya mashabiki wa Simba niligundua wengi wana maswali ambayo ni ngumu kuyajibu.

Wapo waliosema kocha hafai atimuliwe na arudi Cirkovic  lakini kuna wengine wakawajibu alipokua Cirkovic  ile michezo mitano ya mwisho mbona timu ilivurunda so ikabaki ni maswali yasiyo na majibu.

Nami kwa kutumia Miwani yangu pana nikaona ngoja niandike kile ambacho nimekiona ndani ya "WEKUNDU WA MSIMBAZI" ambao miaka michache iliyopita walimaliza ligi bila ya kufungwa mchezo wowote (INVINSIBLE SIMBA) sikumbuki vizuri lakini nadhani walikua chini ya kocha Mzambia Patrick Phiri. Hiyo inabaki kuwa katika Historia kwani kwa Simba ya sasa ni ngumu kuifikia.

 

Katika Makala hii ya WEKUNDU WA MSIMBAZI tutakua tukiwaletea habari zinayoihusu Simba Sports Club tulikotoka tulipo na tunapoelekea.
Sababu nilizoziona kwa haraka kama ndo kati ya vitu vinavoonekana kwa haraka ambavyo vinapelekea Simba kufanya vibaya ni pamoja na:

                                                            UONGOZI
Simba inaongozwa na Ismail Aden Rage ambaye n mwenyekiti akisaidiwa na Geoffrey Nyange Kaburu ila yupo mtu mwingine anaitwa Zakaria Hanspope sijui huyu jamaa ana cheo gani pale  nadhani ni kati ya wale marafiki wa Simba lakini hilo halinihusu kujua kwa sasa.

Maamuzi ya nani asajiliwe mara nyingi hutolewa na watu hawa japokua mara nyingine tumesikia Friends of Simba nao wakiingia katika zoezi hili la usajili hapa bado pananipa mashaka kwani mara nyingi nimeona wakisajiliwa wachezaji sidhani hata kama Kocha huwa hushirikishwa hili linaweza kua jambo mojawapo la kwanini Simba inafanya vibaya sasa
Viongozi wamejivika jukumu la kusajili na mwishowe ndo wakapatikana wachezaji "maghalasa" kama Akuffo,Kanu Biyavanga,Lino Musombo,Ochieng n.k

Mimi naamini hapa mamlaka ya kocha yaliingiliwa na hawa viongozi kupelekea kusajiliwa wachezaji ambao hawana hadhi ya kuchezea Simba.

                                 NGUVU ZA MATAJIRI
Inashangaza sana kwa timu yenye mashabiki wengi ndani na nje ya nchi na iliyoanzishwa miongo kibao iliyopita haijawahi kushinda kombe lolote lenye hadhi ya chama cha soka Afrika CAF acha hilo hakuna pia mipango ya kushinda kombe lolote.

Nguvu ya matajiri imeingia tangu miaka tunazaliwa mpaka leo japokua tofauti ya kipindi hicho na sasa kipindi hicho pesa zilitolewa kuhamasisha ushindi lakini siku hizi pesa zimekua kama kichocheo cha watu kutaka kuonekana hapo ndo utakuta majina kama Malkia wa Nyuki, Friends of Simba na wengine husikika


Ili Klabu iendelee inahitaji pesa lakini ni njia zipi zinatumika kuingiza hizi pesa katika klabu hapo ndo kuna tatizo. Ni hatari leo hii kusikia eti kuna mtu alileta wachezaji wake katika kikosi na hapo ndo husikia habari zingine za hawa ni wachezaji wa Friends of Simba hawa ni wa Kaburu n.k
Hili jambo naliona ni mojawapo ya mambo yanayopelekea timu kufanya vibaya hasa pale inapotokea kama kati ya watu walioleta wachezaji akakorofishana na uongozi uliopo.
Nadhani kulipaswa kuwe na utaratibu wa hawa watu kuingia katika uongozi.
  
MAISHA BILA YA OKWI,YONDANI NA MAFISANGO

Msimu uliopita Simba ilikua timu bora kwa kutandaza soka safi huku lilkichagizwa na mshabuliaji raia wa Uganda Emmanuel Okwi,Beki kisiki Kelvin Yondani  na Marehemu Mafisango (R.I.P) ambao kwa mchango wao Simba iliweza kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara tena kwa kuweka historia mpya ya kuichapa Yanga bao 5-0.

Baada ya Kifo cha Mafisango timu ilianza kuyumba kwani Okwi nae alikua mguu ndani mguu nje akishughulikia swala lake la kuondoka nchini hata mechi alizocheza hakua katika kiwango bora kama msimu uliopita, wakati huo pia ikimpoteza Yondani ambaye alijiunga na Watani Yanga.


Hili mimi naliona kama tatizo lingine la Simba kutofanya vizuri kwani ni dhahiri kama Simba hawakujiandaa kupata mbadala wa wachezaji hao hasa nafasi ya beki (Yondani) na mshambuliaji (Okwi)

          KUBADILISHA KOCHA NA WACHEZAJI


Wakati Mzunguko wa kwanza ukiwa umemalizika Simba ilimtimua kocha wake Milovan Cirkovic kwasababu ambazo mpaka leo sijazijua huku ikimleta Kocha mbadala wake Patric Lewig huku ikiwaacha wachezaji tofauti ambao walikua nao mzunguko wa kwanza akiwemo Daniel Akuffo na Pascal Ochieng.

Hili mimi naliona pia ni tatizo sababishi la Simba kufanya vibaya kwani kocha mwingine amekuja na falsafa zake huku akiwa na muda mchache kabla ya timu haijacheza michuano ya kimataifa na ligi ya ndani na hii kwa aina ya wachezaji wetu ni ngumu kushika mafundisho ya kocha pia wale walioachwa na klabu  ambao walishatengenezea  mfumo mzuri  sasa amekuja kocha mpya anataka mfumo wake ndo utumike hapo ndo utaona si mchezo hili swala.

Huwezi kushangaa ukimkuta Kapombe akicheza kama kiungo huku Ngassa na Kiemba wakianza benchi hii yote inatokana na mfumo wa kocha


                              UWEZO WA KOCHA

Naungana na washabiki wa Simba ambao wanahoji uwezo wa kocha Patrick Lewig. Kwa Mtazamo wangu huyu kocha anaweza kua ni sababu nyingine ya timu kufanya vibaya
nilikuwepo mechi ya kwanza raundi hii ya pili pale Simba walipocheza na African Lyon baadae nikaenda tena Taifa  siku Simba walipotoka suluhu na JKT RUVU siku hiyo nilishuhudia mabadiliko yaliyonishangaza kwani Ngassa ambaye alikua kiisumbua ngome ya JKT Ruvu

Timu ilionekana imechoka sana hasa kipindi cha pili na hili limeendelea katika mechi zote  nilitegemea kama Lewig ni kocha mzuri basi angepigania kurekebisha jambo hilo. Uzuri wa kocha ni kuweza kufanyia kazi mapungufu yaliyoonekana.

          WACHEZAJI KUTOJITAMBUA


Simba ya Sasa inaundwa na vijana wengi ambao wametoka katika kikosi cha pili cha Simba
Vijana hawa walifanya vizuri sana katika kikosi cha Simba B lakini wachezaji hawa wameshindwa kufurukuta huku katika kikosi cha wakubwa labda kwakua wamepewa majukumu makubwa au pengine hawajashika maelekezo ya kocha Patrick au pengine pia walimwelewa zaidi Suleiman Matola kuliko huyu na kama Simba walidhamiria basi kuwatumia vijana hawa walipaswa kumpa nafasi Matola pengine.
Wachezaji ambao ni wakongwe katika kikosi cha Simba hawajitumi ipasavyo au pengine mwisho wao ndo unafika sasa. hapa nawazungumzia mtu kama Haruna Moshi na Amir Maftah
Hivyo basi hili naweza kusema kama mojawapo ya sababu ya Simba kuendelea kufanya vibaya.

Pengine yanaweza kuwepo mengi zaidi ya haya lakini kwa haraka miwani yangu pana iliweza kuyaona haya. Tukutane Mara nyingine Tukijiandaa kwenda kuwakabili Recreativo Libolo ya Angola katika mchezo wa marudiano wa Klabu bingwa ya Afrika huku tukiwa na matumaini hafifu ya kusonga mbele japokua Simba ni wazuri sana katika historia ya mechi za kimataifa.

MUNGU IBARIKI SIMBA
DAIMA TAIFA KUBWA

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
Kwa maoni, ushauri au chochote usisite kunitafuta kupitia  mfalme.edo@gmail.com au 0715 12 7272

6 comments:

  1. Kama vile simba na Yanga wanapokezana matatizo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakika nakubaliana na wewe bundi wa matatizo anaama mtaa hadi mtaa. Hakitoka Msimbazi atarudi tena @Abel

      Delete
  2. Yap mwaka jana ilikua ni Yanga walichemka mbaya mpaka ikapelekea kufungwa zile 5
    sasa mwaka huu ni zamu ya Simba mwendo ule ule sijui itakuaje

    ReplyDelete
  3. hiyo picha ya nne ni friends of simba hao wanajifanya ndio wanaipenda team kumbe ndio wanafki na ndio wanaiharibu team watu wabaya sana hao jamaa.

    mchezaji anaejitambua simba ni mmoja tu shomari kapombe peke yake ila kwa sasa team nzima imeacha ule uchezaji wake minyi kazimoto,kiemba ukiwaona uwanjani ni kama mzigo kwa sasa, ngasa ndo usiseme team inagoma kabisa kucheza uwanjani unategemea utapata matokeo mazuri..? kiukweli mpira wa tanzania kluendelea inahitajika kazi kweli ndugu zangu ni bora kizazi kilichjopo kiondoke kwenye madaraka haya ya mpira ndo tutakuja kuona mabadiliko kuliko kubaki kwa hawa waliopo na kubadilishana leo huyu kesho huyu wote wanasera moja, angetille osiah wa tff alikuwa mmoja wa waandishi habari nzuri alikuwa yupo na waandishi wenzie wa habari alivopata nafasi TFF kabadilika kawa sio tena mtaka haki bali mbomoa haki
    Tanzania kufikia mafanikio sio rahisi hata kidogo

    ReplyDelete
  4. Bab umenena vyema nadhani ipo haja ya hizi timu kuzibinafsisha pengine itasaidia
    timu kama Azam huwezi kukuta mambo haya yanayoendelea kwa hawa Pacha
    Ila ipo haja pia tukaanza na vijana sasa kwakua hatuna la kupoteza ni bora akabidhiwe timu Matola na Amri Said halafu tujipe miaka mitano ya kutafuta mafanikio

    ReplyDelete

Powered by Blogger.