RAGE AMESOMA NA KUELEWA KITABU CHA KROENKE NA HILLWOOD
Miaka 12 iliyopita nilikua na umri wa
takribani miaka 8,Katika umri huo nilikua na akili ya utambuzi wa mema na
mabaya.Darasa langu la tatu lilitosha kujua nini Wazazi wanapenda nifanye na
nini hawataki kusikia nafanya. Japo ilikua ngumu kutimiza matakwa yote ya
wazazi ila nilijaribu kuwaridhisha.Kati ya mambo ambayo wazazi wangu walichukia
ni mchezo wa mpira wa miguu,hapo ndo kulikua na kazi,nilipopenda sana wao ndipo
walipochukia sana. Nikakubali kuitwa mtoto msumbufu,mjeuri,mkaidi na majina
mengine mengi mabaya kwa ajili ya huu mchezo. Wazazi hawakuishia hapo kila
waliposikia nimeenda kucheza mpira jioni yake sebule hujaa fimbo
nyingi,ungefikiri sungusungu wanafanya maandalizi kwa ajili ya kwenda kukamata
na kupiga waarifu usiku huo,La hasha fimbo zote zilikua zinasubiri mwili wangu
mdogo mfano wa fidodido.
Nakumbuka nilikua Napata kipigo mithili ya mbwa mwizi. Lakini fimbo hizo hazikunizuia kesho yake kuibuka kwenye kiwanja changu cha koloni kilichopo mpakani mwa Vingunguti na Tabata na kuendelea kula ladha za sembo,nyuzi banana au kipere pasi na kukumbuka kipigo cha jana nillichopewa na bi mkubwa. Kabumbu litasakatwa mpaka mishale ya saa 12 na nusu jioni. Kila mmoja na njia yake kuelekea nyumbani kwake,hapo ndipo mafua ya ghafla yanaponianza sambamba na moyo kudunda mara 180 kwa dakika,huku nikihisi kibofu cha mkojo kinataka kupasuka. Hiyo ilikua ni hofu ya bakora kutoka kwa mama au baba. Nisipowakuta wazee nyumbani hua nafanya kazi nyingi za nyumbani hata zile zisizonihusu ili nifunike kombe mwanaharamu apite. Lakini sikuweza kuwashawishi mahakimu wangu kuwa huru na adhabu ya bakora.Ikafika kipindi ikawa ratiba niliyoizoea,asubuhi naenda shule nikitoka shule naelekea viwanja vya soka nikirudi nyumbani nachezea fimbo kabla ya kwenda kulala.

Nikaendelea kukua kiumri
pia kiakili,Siku moja nikamuweka mama kitako na kumuuliza “Mama kwanini hutaki
na upendi nicheze mpira?” Mama akanijibu “nakupenda sana mwanangu,sitaki
uharibikiwe kama watoto wengine (huku akitoa mifano ya watoto hao kwa
majina),wamepoteza muda wao mwingi kwenye michezo,shule imewashinda ona walivyo
sasa hawana mbele wala nyuma(mama aliendelea)” Akaniuliza na wewe unataka kuja
kua kama wao? Nikajibu kwa haraka “hapana mama”
“basi mwanangu soma sana ili uje kua daktari,engeneer,au mwalimu hachana
na habari za mpira hakuna mtu aliyefanikiwa kwa mpira mpira wa miguu”
Maneno ya mama yaliniingia na kugusa moyo wangu,hasa pale nilipogeuza shingo yangu na kuanglia maisha ya wachezaji soka mashuhuri mtaani kwangu,niliangalia maisha ya Athumani machepe aliyekua akiichezea Simba, sikuona tofauti yake na kijana asiye na ajira kwa kipindi hicho. Si machepe peke yake bali kuna wachezaji wengi wa miaka ya nyuma walipata kuwa maarufu sana huku mifuko yao ya suruali ikiwa imetoboka.Hao ndo wasakata kabumbu wa zamani,walikua na uzalendo na mapenzi thabiti na soka.

Achana na Habari za mwanzoni mwa
karne ya21,Siku hizi kuna MAONO MAPYA YA DUNIA. Ndani ya maono hayo kuna bosi na kiongozi mmoja tu. Bosi
huyo ana majina mengi kwa kila nchi na kwa kila kabila,wengine watamuita
maela,faranga,kwacha,yen,dollar,shilingi na kwa majina ya jumla anaitwa money
au Pesa. Majina ya bosi huyu ni mengi lakini yana maana,Lengo na kazi
zinazofanana.Miaka ya nyuma ili uheshimike kwenye jamii ilikua lazima uwe na
Elimu,Hapo utashinda dhidi ya umma. Lakini Maono mapya ya Dunia Hayatambui
Elimu juu ya heshima,
Maono mapya ya Dunia yanaamini Mtu mwenye busara,Hekima na kustahili Kuheshimiwa ni Yule mwenye pesa.
Uingeneer,Udaktari,ualimu wako bila shekeli hakuna atakayetambua,kuthamini wala
kuheshimu taaluma yako.Kwenye Dunia yetu mpya kila kitu pesa.Kinachonifurahisha
zaidi hata kwenye ulimwengu wetu wa soka pesa ndiyo inacheza mpira, Wazungu
wanasema “Money plays Football” Siku hizi Wazazi Wanaupenda na kuheshimu mchezo
huu sababu ya pesa. Ni wazazi Wachache sana wanawazuia watoto wao kucheza
soka.Mbwana Samatta,Mrisho Ngassa na Juma kaseja Wamefanya Wazazi kuwahamasisha
Watoto Wao kucheza mpira, Miaka hii ya mpira pesa ukiomba hela kwa ajili ya
njumu itawahi kuliko pesa ya daftari na peni,Samatta na gari lake anatafuta
wapi pesa zake atawekeza huku engenner mwenye degree yake kila siku kwenye
daladala na vyeti akitafuta ajira.Hiyo ndo Heshima ya soka bwana.
Katika miaka ya Karibu Tumeona
mabilionea kama Moize Katumbi chapwe kutoka CONGO DR,Patrice Thopane Motsepe wa
south Afrika,Said Salim Bakhresa wa Tanzania na wengine wengi wamewekeza zaidi
kwenye soka Na kufanya soka letu Afrika liwe La ushindani. Leo hii Teko Modise
anaheshimika kuliko Viongozi na watu wengi maharufu wa mjini kwao SOWETO,Tresor
Mabi mputu ndiye mfalme wa KINSHASA,John Boko amekua maarufu kuliko vibopa wa
Sinza na kijitonyama,hiyo ndo Heshimi ya pesa za Motsepe ,Bakhresa na Katumbi.
Lakini kwenye Ulimwengu huu huu wa
mpira pesa kuna watu wajanja wajanja,wenye pesa kiasi wanaojua kuwatumia
wachezaji kuchota pesa za kina Motsepe,Bakhresa na katumbi.
Wengi wao hua wenyeviti au Viongozi wangazi za juu kwenye timu husika. Kule uingereza utamkuta mwenyekiti wa Arsenal,Bwana Peter Hillwood hakuna arsenal bila hillwood babu yake mzee Samwel Hillwood alikua mwenyekiti wa Arsernal mnamo mwaka 1926-1936 na 1946-1949,pia baba yake mzee Dennis Hillwood alipata kuwa mwenyekiti wa Arsenal mnamo mwaka 1962-1982 kabla ya kufariki na mtoto wake Peter Hillwood kushika hatamu mpaka hivi leo. Peter Hillwood,Ivan Gazids na Mjasiliamali wa kimarekani Stan Kroenke hawa ndo wanaounda CC(central comitee) ya Arsenal.
Watu hawa wamejaa siasa na roho ya ujasiliamali zaidi,Akili yao yote ipo kwenye kutengeneza pesa kuliko kuimarisha na kujenga timu ya upinzani,Mungu awape nini watu hawa? Wamepata na kocha Mchumi anayejua kucheza na akili ya mashabiki.
Profesa Wenger miaka 8 bila kombe ameingiza zaidi ya paund 50 million kama mshahara, Huku akina Piers Morgan na washabiki wenzake wa Arsenal Wakiumia juu ya mwenendo wa timu wa kutoka kapa kila msimu,sambamba na kuuza wachezaji nguli bila kutafuta mbadala sahihi, CC ya Arsenal na wenger wao hutazama kwenye zizi na kutafuta kondoo aliyenona kwa ajili ya kuuza na mwisho wa mwaka kugawana malupulupu kutokana na faida ya kondoo huyo. Hawa kwa kiasi wameifanya Man City iitwe Man City,wamejua jinsi ya kufyonza pesa za Sheikh Mansor, huku wakiumiza mioyo ya mashabiki wa arsenal

Hapa kwetu Bongo Yupo fundi aliyepata mafunzo
kama ya CC ya arsenal japo kwenye vyuo tofauti. Si mwingine yeye anaitwa
muheshimiwa Ismail Aden Rage,
Rage
mtu huyu amejaaliwa fitina ya soka,siasa pamoja na ujasiriamali. Mashabiki wa msimbazi nikiwauliza mbadala wa Samatta ni nani hawatanipa jibu,Ila Rage kawapa kiburicha kujisifu kwa kumuuza Samatta kwa mamilioni ya pesa, Hayo mamilioni ya Samatta yameenda wapi? au yameifanyia nini simba hilo ndo swali la kujiuliza kama mshabiki wa simba,Vipi kuhusu Ochieng na Okwi?
Kama mmeshindwa kuhoji pesa zilipoenda hojini hata mbadala wa wachezaji hao. Simba Ya sasa inawachezaji wa kawaida na wasio na hadhi ya kuchezea simba si kwenye mashindano ya kimataifa pekee bali hata ligi ya ndani.sina uhakika kama rage alikua anamtaka Yondani au pesa za usajili za Yondani? Si vibaya Simba kuuza Wachezaji nje ya nchi, ni vizuri sana hasa kwa maendeleo ya soka
Leo hii Haruna Chanongo, Ramadhani Singano na Christopher Edward wanapewa majukumu makubwa kuzidi umri wao.
Piers Morgan
Si lazima uwe mshabiki maarufu wa Simba kama
Mzee Magoma moto au Mshabiki Nguli wa Arsenal kama Piers Morgan ili uwe na
machungu juu ya kupotea kwa ladha kutoka kwenye timu hizi zinazoongozwa na
wajasiliamali waliojaa siasa za soka
By kaijage jr
middle ya juu
No comments