WATOTO WA MZEE MANENO NI WASHAMBULIAJI HATARI WA MEDIA FC

 
                Miaka mingi iliyopita, mtaani kwetu alipata kuishi mzee mmoja maarufu aliyejulikana kwa jina la bwana maneno.Mfupi,mweusi,mnene kiasi ambaye jina lake la maneno linasadifu yaliyomo kinywani mwake.Mzee maneno hakuwai kua mwanasiasa ila alikua na maneno matamu yasiyochosha kumsikiliza.uwepo wa bwana maneno kijiweni hautahitaji kahawa ili kunogesha utamu wa bao.kutokana na maneno yake mengi bwana maneno alipendwa na watu wa rika zote mtaani.ukitaka upendwe mtaani pendwa na mzee maneno kwanza,atakuvisha kilemba cha ukoka mbele za watu na watu wote watakupenda na kukubali.
                     Bwana maneno alikua mume wa wake wawili,Mke mkubwa wa bwana maneno alijulikana kwa jina la  bi ulaya na bi mdogo alitwa Afrika,Bwana maneno aliwapenda sana wake zake na kila mmoja alikua na kaya yake.Bi ulaya aliishi kwenye nchi ya bahari huku bi afrika alikua akiishi kwenye nchi ya milima.Bwana maneno alikua na watoto wengi, ila aliwapendasana  watoto wake wawili Uingereza wa bi ulaya, na Mtoto wa mwisho wa bi Afrika aliyejulikana kwajina la afrikakusini.
Kikosi cha England
 
                    Watoto hawa aliwapendelea kwa kuwapa malezi na elimu bora.Watoto hawa wakahitimu masomo  yao na wote wawili wakafanikiwa.Watoto hawa wa bwana maneno walifungua viwanda na makampuni mengi yaliyojulikana Duniani kote,bwana uingereza maneno alikua tajiri kuliko mtu yeyote aliyeishi kwenye nchi ya bahari na nchi jirani zote, vivyo hivyo kwa bwana Afrikakusini maneno kwa nchi ya milima na nchi jirani zote.Pamoja na utajiri wao Watoto hawa walikua na mapenzi na mpira wa miguu huku wakiwa na vipaji kiasi katika mchezo wa soka.
 
Watoto hawa kwa Hekima yao wakajumuika pamoja na kuamua kuanzisha timu yao ya soka iliyojulikana na kujulikana mpaka sasa  kwa jina la MEDIA FC,media fc ilikua ina uwezo wa kununua mchezaji yeyote na kwa bei yeyote,Ukitaka kua maarufu kupita uwezo wako we chezea media fc,Ukitaka dunia yote ikutambue wewe ni nani We chezea media fc.Kwa utajiri wa watoto hawa wa Mzee Maneno Wamemwaga pesa nyingi sana Kwa maendeleo ya Media Fc huku maendeleo ya timu zao za taifa yakidumaa

                  Cha ajabu timu ya Taifa ya Bwana Uingereza Maneno na  ya Bwana Afrikakusini Maneno hazifanyi vizuri kwenye mashindano ya kimataifa kama Nchi zingine,Bwana Uingereza Amejaribu kutumia Pesa zake nyingi kuwafanyia promo wachezaji wake.
 
Pia kuwapa uraia baadhi ya wachezaji ambao wamengara kwenye timu ya media fc,Lakini bado kwenye mashindano ya kimataifa Robo Fainali Ndo kombe lake,Bwana UIngereza maneno akatumia mbinu za media na kutuaminisha Wayne Rooney ndiye Pele mzungu,Steven Gerald ndio Kiungo Pekee Duniani Aliyekamilika,Dany Welbeck na Theo walcoth ni washambuliaj hatari wenye kasi kuliko wote duniani,Wilshere na Cleverely ni Sawa na Xavi na Iniesta,Joe Hart ni Kipa Bora Duniani Kwa sasa.
 
Lakini wachezaji hao overrated wakikutana na Timu kama Germany,Spain au Italy huonekana kama wamekunywa pombe ya ulanzi kabla ya kuingia uwanjani
 
 
 
            Kwa upande wa nchi ya  bwana afrikakusini maneno,amefilisi sehemu ya migodi yake kwa ajili ya kujenga viwanja bora vya soka kwenye nchi yake lakini naye hana tofauti na kaka yake wa damu kutoka kwa mama mwingine. Huyu nae kufuzu kwenye mashindano ya kimataifa ni ngumu,hutumia umaarufu na miundombinu yake kuandaa mashindano na yeye kushiriki kama mwenyeji wa mashindano.
 
 Pamoja na bwana afrikakusini kuamini Teko Modise ndiye mchezaji mwenye kipaji Afrika,tresor mputu si lolote si chochote kwa Katlego mphela,aboutrika ni mwanafunzi kwa mwalimu Tshabalala,lakini timu hii ya Taifa Ya Bwana Afrikakusini Kila kukicha hugombania Kufuzu tu mashindano makubwa ya kimataifa bila mafanikio

                  Bwana uingereza na afrikakusini wataendelea kutamba na media fc ila timu zao za taifa hasilani hazitafanikiwa kwa maneno yao.

                                                 




Imeandaliwa na  MIDDLE YA JUU

                                                  KAIJAGE Jr

5 comments:

Powered by Blogger.