THE GUNNING MACHINE

TIMU BORA KATIKA MIAKA 20 YA LIGI KUU ENGLAND (E.P.L)
INVINCIBLE


Msimu wa  2003-2004 ulikua msimu wa 12 wa Arsenal katika Ligi Kuu nchini England (EPL) na msimu wa 74 mfululizo katika ligi ngazi ya juu katika soka la England.
THE GUNNING MACHINE leo tunaangalia Msimu huu ambao unabaki kua wa historia katika katika klabu ya Arsenal. Timu hii kutoka London ya Kaskazini iliweza kumaliza msimu mzima wa ligi bila kupoteza mchezo wowote na kuifanya kua timu ya pili kuingia katika historia ya soka kwa kumaliza msimu mzima bila kufungwa timu ya kwanza ikiwa ni Preston North End mwaka 1889 timu zote hizo zikipewa majina ya utani "The Invincible" (Isiyofungika)

Meneja wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger alitabiri mwaka 2002 kwamba ana kikose bora kinachoweza kumaliza msimu mzima bila kufungwa.
 Ni kweli mafanikio hayo yalifikiwa japokua hali haikua hivyo katika michuano mingine ambayo kikosi hicho kilishiriki mwaka huo kwani waliweza kutolewa na Chelsea katika hatua ya Robo fainali ya Ligi ya mabingwa ulaya (UCL)  na kufika hatua ya nusu fainali katika Kombe la Fa na lile kombe la Ligi ( Carling Cup zamani hivi sasa ni Capital one)

              KIKOSI HIKI KILITOKA WAPI?

Baada ya kikosi cha Wenger kukubali kufungwa 2-1 na Liverpool msimu uliotangulia katika fainali ya kombe la FA wakati wakitangulia kwa goli 1-0.
Msimu mpya ulipoanza Wenger alimsajili Jens Lehmann kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa paundi milioni 1.5 huku ikiwapa mikataba mipya wachezaji wake nahodha Patrick Viera na winga Robert Pires.

 Giovanni van Bronckhorst alisajiliwa kutoka Rangers kwa paundi milion 8.5 wakati Sol Campbell alijiunga na Arsenal akitokea kwa wapinzani wa jadi Spurs.
Kinda Francis Jeffers alijiunga akitokea Everton kwa ada ya uhamisho paundi milion 8. Janichi Inamoto  na Richard Wright, Johan Djourou, Gael Clichy,Cesc Fabrigas pia waliongezwa kikosini wakati msimu mpya ulipokaribia.


Hawa waliungana na wachezaji wengine waliokuwepo kikosini katika kuweka historia. Wakiwemo Mfungaji bora wa msimu huo Thiery Henry akifunga magoli 30 katika ligi na magoli 39 katika michuano yote. Walikuwemo pia Ashley Cole,Patrick Viera,Martin Keown,Fredrick Ljungberg, Dennis Bergkamp,Sylvain Wiltord, Lauren, Edu,Gilberto Silva,Reyes, Nwankwo Kanu, Kolo Toure n.k


       MATOKEO YA MSIMU MZIMA 2003-2004
Arsenal                  2-1      Everton
Middlesbrough    0-4      Arsenal
Arsenal                  2-0      Aston Villa
Man City                1-2      Arsenal
Arsenal                   1-1      Portsmouth
Man United          0-0       Arsenal
Arsenal                  3-2       Newcastle United
Liverpool               1-2       Arsenal
Arsenal                   2-1      Chelsea
Chalton Athletic    1-1      Arsenal
Leeds United         1-4      Arsenal
 Arsenal                   2-1      Totenham Hotspurs
Birmingham City   0-3       Arsenal
 Arsenal                   0-0      Fulham
Leicester City          1-1      Arsenal
 Arsenal                   1-0      Blackburn Rovers
Bolton                      1-1      Arsenal
 Arsenal                  3-0     Wolves
Southampton         0-1      Arsenal
Everton                    1-1      Arsenal
 Arsenal                   4-1      Middlesbrough
Aston Villa              0-2      Arsenal
 Arsenal                   2-1       Man City
Wolves                    1-3        Arsenal
 Arsenal                   2-0       Southampton
Chelsea                    1-2       Arsenal
 Arsenal                   2-1        Chalton Athletic
Blackburn               0-2       Arsenal
 Arsenal                   2-1        Bolton
 Arsenal                   1-1        Man United
 Arsenal                   4-2       Liverpool
Newcastle                0-0       Arsenal
 Arsenal                   5-0       Leeds United
Totenham                2-2       Arsenal
Arsenal                   0-0       Birmingham
Portsmouth              1-1       Arsenal
Fulham                     0-1       Arsenal
Arsenal                     2-1       Leicester City

Ukiangalia kwa Makini timu zote zilifungwa na Arsenal hii isipokua Man United na Portsmouth ambao waliambulia droo katika mechi zao zote mbili.
Msimu ulimalizika na Arsenal kuweka historia mpya katika Ligi kuu England kwa kushika nafasi ya kwanza Ikitawazwa mabingwa wapya wa England: Ikicheza jumla ya mechi 38, ikishinda 26, Ikadroo mechi 12 na kutopoteza mechi yoyote.
Ilifunga magoli 73 na kufungwa magoli 26 na kupata jumla ya pointi 90 magoli 30 yakifungwa na Thierry Henry ambaye ndo aliibuka mfungaji bora wa msimu huo.


  •     WAKO WAPI WAKALI HAWA INVINCILE SEASON.

1. Jens Lehmann ambaye alikua golikipa mwenye miaka miaka 43 hivi sasa amestaafu soka.
2. Lauren mwenye miaka 35 naye ameshastaa amestaafu  kucheza soka.
3. Kolo Toure mwenye miaka 32 yuko Manchester City akiendelea kucheza soka
4. Sol Campbell mwenye umri wa miaka 38 amestaafu kucheza soka.
5. Ashley Cole mwenye miaka 31 anaichezea Chelsea yenye makazi yake Stamford Bridge London.

6. Fredrik Ljungberg mwenye miaka 36 yuko huru.
7. Gilberto Silva ana miaka 36 anacheza katika klabu ya Gremio
8. Patrick Vieira  mwenye miaka 36 yuko Man City kama "Football Development Executive"
9. Robert Pires ana miaka 39 hivi sasa yuko huru.
10. Dennis Bergkamp mwenye miaka 44 yuko Ajax kama kocha msaidizi.
11. Thiery Henry ana miaka 35 yuko New York Red Bull ya Marekani inayoshiriki ligi ya MLS


Kwa leo naishia hapa katika THE GUNNING MACHINE na Tutaungana na Richard Leonce Chardboy wiki ijayo akiendeleza gurudumu hili la kutuhabarisha kuhusu Arsenal.

>>> Imeandikwa na Edo Daniel Chibo wa Wapenda Soka (kandanda) group katika facebook
Kwa maoni niandikie katika mfalme.edo@gmail.com


 
          
 
              
 

1 comment:

Powered by Blogger.