MILANGO SAHIHI YA MANJI NA MALKIA WA NYUKI
Shinda hata bahati nasibu ya milioni mia nane kisha panda ndege hadi Malaga nchini Hispania. Mtafute mtu mmoja anaitwa Sheikh Abdullah Al Thani. Huyu ni mwenyekiti wa klabu ya Malaga ambayo haipo vizuri kiuchumi. Nenda kamwambie mimi naipenda Malaga, nimekuja kuwa mfadhili hapa.
Utashangazwa na jibu lake. Atakuambia, "hapa itabidi ununue hisa, uwe mmoja kati ya wamiliki wa klabu ama la, lete biashara yako tuingie mkataba wa kuitangaza".
Ukiona analeta mbwembwe, fanya kitu kimoja. Panda ndege mpaka Julius Kambarage Nyerere Airport, chukua tax mpaka Kariakoo-Msimbazi. Omba namba ya mtu mmoja anaitwa Ismail Aden Rage. Mpigie simu (huna haja ya kuonana nae).
Atakuambia jinsi anavyozihitaji pesa hizo sana. Atakupamba kuliko matajiri wa Masaki wanavyopamba majeneza ya baba zao.
Hiyo ndiyo kawaida yetu. Tunajua kua mpira unahitaji pesa. Baadhi yetu tunajua tufanye nini kupitia mpira ili pesa hiyo ipatikane. Lakini hatufanyi hivyo, badala yake tunategemea wafadhili.
Unajua maana ya ufadhili?
Ufadhili hauna tofauti na zawadi ambayo anaeyetoa ndiye anayeamua atoe kiasi gani na lini mpaka lini.
Kuna watu wana akili sana, namkumbuka mtu mmoja anaitwa Imani Mahungila Madega. Alipata kuwa mwenyekiti wa klabu moja hapa nchini inaitwa Yanga. Nayo ni klabu yenye njaa njaa tu tena zisizo na sababu. Njaa zake ni zaidi ya Malaga mara zote.
Akatokea mtu mmoja anaitwa Yusuph Manji (mwenyekiti wa sasa wa Yanga) akajitolea kuwa mdhamini wa klabu kwa pesa zake. Hapa kwetu ni kitu cha kawaida tu, hivyo hakupata tatizo kupokelewa kwa mikono yote.
Akafanya mengi mazuri lakini akaanza kuwa na sauti kubwa klabuni. Utaachaje kutia 'kibesi' kwa watu ambao unawalipa wote kuanzia maofisa hadi wachezaji?
Madega alipoona hali ile akamwambia Bwana Manji kwamba, "nataka uwe mdhamini wa klabu yetu na siyo mfadhili tena, kwa vile una kampuni njoo tusaini mkataba na kampuni yako".
Manji akakataa, sijui kwa nini!
Madega akalala, akaamka. Akaamua kumtimulia mbali. Sawa kabisa, hata Sylvio Berlusconi angefanya kama Madega. Sawa na ambavyo Shekh Abdullah angekufanyia wewe.
Lakini mambo yalienda chinichini, wazee wakatumia busara kumweka sawa Madega na kumkumbusha kuwa hii ni Yanga. Basi, wakaipalilia ndoa ya Manji na Yanga na inaendelea vizuri hadi sasa Manji ni Bosi wa Yanga.
Hawa wafadhili nia zao ni nzuri kabisa. Huyu malkia wa nyuki ana nia ya dhati kabisa ya kuiona Simba na Tanzania kwa ujumla ikipaa katika anga la soka.
Manji aliumizwa sana na wajanja waliokuwa wanakata cha juu kwenye pesa alizokua anaifadhili Yanga kwa mapenzi yake akaamua kugombea uenyekiti wa klabu.
Tatizo ni kwamba tunawaruhusu wapite milango isiyo sahihi.
Wafadhili ni mashabiki ambao wana mitazamo na mapenzi yao ambayo siyo kila mara ni sahihi kwa maslahi ya klabu.
Lakini pia kama binadamu wengine wenye pesa hawa pia wanapenda misifa na mikogo na kuangukiwa kila mara na wenye shida.
Na kwa sababu wana pesa basi tunalazimika kuwabembeleza.
Manji huwa akijisikia anatangaza kujiondoa Yanga, akina Mzee Akilimali wanachanganyikiwa kabisa. Panakuwa hapatoshi.
Sasa namna ya kudhibiti ubinadamu wa hawa watu usitawale klabu kwa sababu ya pesa zao, ndipo unapopaswa kuwaambia, "kama unaipenda klabu na unajiskia kutusaidia basi nunua hisa".
Uzuri wa hisa ni kwamba zitamlipa hata Malkia Wa Nyuki pia kupitia Simba. Kwani nani kasema yeye hataki kuongeza pesa zake?
Lakini sasa atakua na mkataba ambao utamweka mbali na vipaza sauti vya klabu. Kinachoshangaza ni kuwa hawa wafadhili ni wafanya biashara na wanaelewa yote haya lakini hawataki. Sijui kwa nini!
Hivi inakuingia akilini kweli? Unaambiwa weka hapa pesa zako utapata faida, wewe unasema hutaki. Unataka uweke tu bila faida yoyote.
Unamtafsiri vipi mtu huyu?
Anatafuta sifa?
Na kama ni sifa zitamsaidia nini?
Kwa nini asitafute sifa kwa jina la kampuni yake ili akue kibiashara mara dufu?
Sina majibu ya maswali hayo, lakini sisi wa soka tufanye ya soka.
Tuanzishe utaratibu wa hisa kwenye klabu zetu, kisha tuwaoneshe hawa wanaoitwa wafadhili wetu kwamba kama unavutiwa na sisi pitia hapa. Kama hutaki, anzisha timu yako kama Wanalamba lamba walivofanya. Ni vizuri pia.
Napata mashaka kama tunazo sauti za kuunguruma kama Sheikh Abdullah tukishaoneshwa pesa kwa sababu hapa kwetu tuna msemo wa 'pesa ni sabuni ya roho'.
Imetayarishwa na Richard Leonce Chardboy kutoka Wapenda Soka 'kandanda' Group.
Nipate katika chardboy77@yahoo.com na @chardboy77 kwenye twitter au 0658399341
Umasikini na mipango duni ndio chanzo
ReplyDeleteSafi sana Richard Leonce Chardboy, Artical yako iko poa kwa maana ina kitu ndani yake, ila nadhani kuna changamoto inayokabili blog kwa sasa, nadhani kuna haja ya kuwa na Editor ambaye atakuwa anahariri post za waandaa kabala ya kuziweka kwenye blog.
ReplyDeleteSo far am doing that ila anatakiwa mtu makini zaid na alie fast
DeleteTunayo sfr ndefu sana mpk kufika huko mnakotaka tufke.
ReplyDeleteSi safari ndefu ni suala la maamuzu tu!
ReplyDeleteof coz hicho nikitu muhimu kwa sasa. hapa naomba tuelewane tu kwamba hat mie natumia uwezo wangu tu. sina elimu yoyote juu haya mambo. kama ilivyo kwa edo ambaye mpk sasa yeye ndo ananipa mimi sauti kwa kuedit kaz zangu. ila tusife moyo.tutaenda polepole .a hatimaye tutafika. muhimu tuendelee kupeana suport kama hihi na ushauri kwenye haya mawasiliano tunayotoa. thanks alot guys.chard
ReplyDeletekistaarabu haya si mambo ya kujadiriwa hapa......... rich igot u
ReplyDeleteThanx alen. CHARDBOY
ReplyDelete