THE TRUE RED DEVILS
MATUKIO YA TAREHE YA LEO 23/03/2013 KATIKA HISTORIA YA MAN UNITED.
Nick Powell |
Tarehe kama ya leo mwaka 1912, Tom Nuttall alifunga goli la kwanza katika mechi ya kwanza kuichezea Man United katika droo ya 1-1 dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Old Trafford.
Tarehe kama ya leo mwaka 1957, Bobby Charlton alifunga alifunga katika mechi yake ya kwanza United katika kombe la FA katika ushindi wa 2-0 ugenini wakicheza na Birmingham City.
...
Tarehe kama ya leo mwaka 1989, mchezaji wa zamani wa Man United Gordon Strachan aliikacha United na kujiunga na mahasimu wetu wakati huo Leeds United.
Tarehe kama ya leo mwaka 1994, Eric Cantona alikua mchezaji wa kwanza wa Man United kutolewa nje katika michezo miwili mfululizo baada ya kupata kadi nyekundu katika mechi ya 2-2 dhidi ya Arsenal huku magoli yote mawili ya United siku hiyo yakifungwa na mkali LEE SHARPE.
Tarehe kama ya leo mwaka huo huo 1994, Chipukizi wa United Nicholas Edward "Nick" Powell alizaliwa katika mji wa Crewe.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
WALICHOKIFANYA MASHUJAA WA MAN UNITED WAKIWA KATIKA TIMU ZAO ZA TAIFA KATIKA KUTAFUTA NAFASI YA KUCHEZA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA MWAKANI
Wikiendi hii Ligi mbalimbali zilipumzika kupisha michuano ya kimataifa kutafuta nafasi ya kucheza fainali za FIFA za dunia nchini Brazil. Na hapa ni wachezaji wa United waliofungia timu zao na kutoa michango ya pasi za magoli.
- Robin Van Perse alifunga goli moja na kutoa asisti 1 katika ushindi wa magoli 3-0 walioupata Uholanzi dhidi ya Estonia
- Wyne "Wazza" Rooney akiwa katika kikosi cha England kilichoipiga San Marino 8-0 aliweza kufunga goli zuri kwa njia ya "free kick" pia alitoa pasi moja iliyozaa goli huku Staa mwingine Ashley Young akifunga goli mojawapo na kutoa pasi moja ya goli.
- Javier Hernandez "Chicharito" aliifungia timu yake ya Mexico magoli mawili yaliyoipelekea Mexico kutoa droo ya 2-2 dhidi Hondurus.
Imetayarishwa na Edo nicheki katika mfalme.edo@gmail.com au Facebook Edo Daniel Chibo na Twitter Edo Daniel1.
Umesomeka kaka!
ReplyDelete