MIWANI PANA YA EDO - TAIFA STARS KUELEKEA BRAZIL

TATHMINI YA MECHI NA MSIMAMO WA KUNDI C KATIKA KUTAFUTA NAFASI YA KWENDA BRAZIL MWAKANI


Taifa Stars vs Morroco
....Ikicheza kwa kujiamini na pengine ikichagizwa na hamasa kubwa toka kwa mashabiki lukuki waliojitokeza Uwanja mpya wa Taifa Dar es Salaam, Taifa Stars waliweza kuibuka na ushindi mnono nyumbani dhidi ya Moroko timu ambayo inaaminiwa kua kat ya timu bora za Afrika.

Baada ya kuingia kipindi cha pili kilipoanza akichukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto, Mshambuliaji anayekipiga katika timu ya TP Mazembe ya Congo DR aliwainua maelfu ya waTanzania waliofurika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kwa kuucheza vizuri mpira wa kurushwa wa Erasto Nyoni.
Magoli mengine ya Stars yalifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 67 na dakika ya 79 kazi nzuri ikiwa imefanywa na Tomas Ulimwengu ambaye kuingia kwake kipindi cha pili kulibadilisha sura nzima ya mchezo.
Kazi nzuri pia ilifanywa na Juma Kaseja kwani aliokoa michomo mingi iliyoelekezwa langoni mwa Stars japokua aliruhusu goli jepesi dakika za mwisho baada ya mpira kumteleza.
Taifa Stars inashika nafasi ya 119 wakati Moroko inashika nafasi ya 77 katika Ubora wa Soka kwa viwango vilivyotolewa na FIFA Machi 14,2013.

Kwa ujumla timu ilicheza vizuri na kwa jinsi nilivyoona hii inaweza kua ni tathmini ya mchezaji mmoja mmoja
  1. JUMA KASEJA
Ameendelea kuonyesha kama Kocha Marcio Maximo alikosea sana kumwacha kipindi kile kocha huyo alipokua akiinoa Taifa Stars kwani aliokoa michomo mingi ya hatari ambayo kama Moroko wangefanikiwa kufunga ingewasaidia sana  na kuwapa hamasa ya kuibuka na ushindi katika mechi hiyo japokua makosa yake yaliigharimu timu na kufungwa goli dakika za nyongeza aliposhindwa kuudaka mpira.

      2.  ERASTO NYONI
 
Ni ngumu sana kuamini kama beki huyu ana miezi kadhaa hajacheza mechi ya mashindano ngazi ya klabu kwani ameweza kucheza vizuri sana akijiamini huku akipanda na kupiga krosi na ni huyu jamaa ambaye mpira wake wa kurusha ulizaa goli la kwanza lililofungwa na Tomas Ulimwengu.
Erasto Nyoni amefungiwa na klabu yake ya Azam na mwalimu alimwita vivyo hivyo nadhani alijua uwezo wake na hakumwangusha katika hili

      3.  SHOMARI KAPOMBE
 
Mchezaji bora wa Mwaka wa 2012 Tanzania akiichezea timu ya Simba ya Dar es Salaam alionekana kupotea nyakati flani na hii ilitoa mwanya kwa winga wa Moroko kupiga krosi na pengine kupita na kutia kashikashi katika lango la Taifa Stars. Nadhani sababu iliyomfanya Kapombe kupotea mchezoni ilitokana na nafasi aliyokua akiicheza mana mara nyingi tumemzoea kumwona akicheza beki namba 2 na pengine beki ya kati lakini ni hazina kubwa ya Taifa kwa siku zijazo.


      4. AGREY MORRIS
 
Moja kati ya mabeki bora kabisa tulionao katika kikosi cha Stars akiichezea timu ya Azam ya Dar es salaam. Huyu ni kati ya wachezaji watatu waliosimamishwa na uongozi wa Azam kufuatia tuhuma za kuhujumu timu na amekua nje ya klabu yake kwa miezi kadhaa sasa lakini kocha Kim Paulsen alimwamini na kumwita katika kikosi chake na bila kupepesa macho alicheza vizuri mno akiungana na Kelvin Yondani.

      5.  KELVIN YONDANI
 
Beki bora kabisa akiichezea timu ya Yanga aliweza kuwazuia ipasavyo washambuliaji wa Morocco na amekua akielewana vyema na kipa wake Juma Kaseja. Yondani jana alicheza vizuri sana kwa nafasi yake anastahili pongezi.

      6. SALUM ABUBAKARY (SURE BOY)
 
Kazi kubwa ya kiungo huyu anayekipiga klabu ya Azam ya Dar es salaam ilikua ni kutibua mipango yote iliyofanywa na Moroko na hakika alifanikiwa katika hili kwani aliweza kucheza vizuri na kutibua kabisa mipango ya Moroko pale katikati.
 
      7.  MRISHO NGASSA
 
Ni kati ya wachezaji ambao walibanwa vilivyo na mabeki wa Moroko nadhani walishamfahamu hivyo uwepo wake haukuwa na madhara sana na hatimae kocha alimpumzisha kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Athumani Iddi "Chuji"
 
     8. FRANK DOMAYO
 
Kijana huyu toka katika klabu ya Yanga ameonyesha ni hazina kubwa kwa Taifa kwani alimiliki vilivyo kiungo cha ushamuliaji na mara chache akijaribu kupiga mashuti ya mbali ambayo hayakua na madhara kwa Moroko
 
    9.  MBWANA SAMATTA
 

Jamaa ni Tegemeo la Tanzania uwezo wake wa kukaa na mpira na kutoa pasi zenye akili uliweza kumtofautisha na wachezaji wanaocheza katika ligi ya ndani.
Samatta ndo mfungaji wa magoli mawili kati ya matatu ya Taifa Srats.
 
     10. MWINYI  KAZIMOTO
 
Alianza vizuri kipindi cha kwanza na kadri muda ulivyosega alikua akipotea mchezoni na mara nyingi pasi zake ziliishia miguuni mwa Moroko nadhani mwalimu aliliona hilo na akampumzisha kilipoisha kipindi cha kwanza na nafasi yake ikachukuliwa na Tomas Ulimwengu.
 
    11. AMRI KIEMBA
 
Huyu jamaa ni kati ya wachezaji waliocheza vizuri katika mchezo huo akitoa pasi zenye akili na mara nyingine kujaribu kupiga golini na bado kidogo angefunga kama shuti lake alilopiga dakika za mwishoni lisingegonga mwamba.
 
                      WALIOINGIA WAKITOKEA AKIBA
  • THOMAS ULIMWENGU


Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Kim kumwingiza Ulimwengu akichukua nafasi ya Kazimoto yalizidisha chachu ya ushindi kwani kwa Stars kwani alicheza vizuri sana na kuwasumbua vilivyo mabaki wa Moroko. Goli lake ambalo lilikua la Kwanza kwa Stars lilikua muhimu kuamsha hamasa kwa wachezaji na kupatikana magoli mengine mawili.
 
  • ATHUMANI IDD "CHUJI"
Kiungo huyu Mkongwe aliingia kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa lengo likiwa ni lile lile kuharibu mipango ya wapinzani kama alivyokua akifanya Sure Boy na alijitahidi sana kufanikisha hilo
 
  • JOHN BOCCO
Aliingia dakika za majeruhi akichukua nafasi ya Mbwana Samatta nadhi lengo lilikua ni kupoteza muda kwa dakika hizo chache.
 
MSIMAMO ULIVYO KATIKA KUNDI HILI LA C KATIKA HATUA YA KUFUZU KWENDA BRAZIL 2014.
 
 
 
Msimamo katika kundi letu hili unaonyesha Taifa Stars inashika nafasi ya Pili baada ya kucheza michezo 3 Ikifungwa mchezo mmoja na Ivory Coast kabla ya kushinda dhidi ya Gambia na Moroko.
Mechi inayofata kwa Stars itakua Juni 7 2013 nchini Moroko watakaporudiana na Moroko na wiki moja baadae yani Juni 14,2013 Taifa Stars itakua Dar es salaam kurudiana na Ivory Coast na mechi ya mwisho kwa Stars itakua Ugenini Dhidi ya Gambia Septemba 6,2013 huko Gambia.
 
 
 
ILI KUFUZU KWENDA BRAZILI INATAKIWA TAIFA STARS IPITIE HAPA
 

Makundi yapo 10 ambapo kila nchi itakayoongoza katika kundi lake itaingia katika hatua ya pili ambapo zitapangwa mechi za mtoano nyumbani na ugenini kwa timu hizo 10 zitakazoingia hatua hiyo na washindi wa jumla ndio watakaofanikiwa kwenda Brazil moja kwa moja katika nafasi 5 ambazo Afrika wanazo katika uwakilishi.
Mechi hizo zimepangwa kufanyika Octoba 11-15 na Marudiano ni Novemba 15-19 mwaka huu 2013.
 
JE TUTAFIKA?
 
.......kama una lolote nicheki facebook kwa Edo Daniel Chibo au Join group la Wapenda soka(kandanda) tujadili yahusuyo soka. 

3 comments:

  1. Tukiwa more focused tu naweza pita

    ReplyDelete
  2. Sifikirii sana kufika worldcup ila target hii inaweza kutufikisha pazuri kwenye AFCON zijazo (R. Lighongo )

    ReplyDelete
  3. World cup ni maji marefu kwetu. Ila hatuna cha kupoteza so tusiwe na presure, tupige soka tu. CHARDBOY

    ReplyDelete

Powered by Blogger.