THE GUNNING MACHINE
DENNIS NICOLAAS BERGKAMP NI WAKIPEKEE (SEHEMU YA PILI)
Baada ya kuona jinsi nafasi ya Bergkamp katika kikosi cha kwanza cha Arsenal ilivyoanza kutia shaka kutokana na uwepo wa Thierry Henry na Sylvain Wiltord. Leo THE GUNNING MACHINE inakuonesha ni nini ambacho Bergkamp alikifanya lakini hasa mara nyingi akitokea benchi (super sub)
2001/02 Arsenal walitwaa Ubingwa wa ligi kuu pamoja na kombe la FA. Bergkamp alitengeneza magoli 15 msimu huo. Huku akifunga goli la kukumbukwa katika Ligi kuu ya Uingereza kwa pasi ya Robert Pires, Machi 3,2002 dhidi ya Newcastle.
Anapokea pasi akiwa amekabwa vilivyo na Nikos Dabizas, lango la Newcastle likiwa mgongoni kwake. Anaugonga mpira kulia kwake, yeye anazungukia kushoto,anaukuta na kuutia kambani. Lazima useme kitu ukiangalia marudio ya goli hilo.
Msimu wa 2002/03, Bergkamp alifunga goli lake la 100 akiwa na Arsenal dhidi ya Oxford UTD. Arsenal walishindwa kutetea kombe la ligi kuu lakini walilirudisha lile la FA huku Bergkamp akipewa mkataba wa mwaka mmoja.
Msimu wa 2003/04 Bergkamp akachangia mafanikio ya Arsenal kutwaa kombe la ligi kuu bila kupoteza mchezo. Akaamua kusaini mkataba mrefu zaidi na Arsenal.
Msimu wa 2004/05, Arsenal walipoteza kombe hilo kwa Chelsea. Bergkamp alivaa kitambaa cha unahodha katika mchezo dhidi ya Midlessbrough baada ya Patrick Vieira kuumia, Arsenal wakitoka nyuma kwa 1-3 na kushinda 5-3.
Katika mchezo wa mwisho dhidi ya Everton, Bergkamp alikua "Man Of The Match" kwa kufunga goli moja na kutengeneza matatu katika ushindi wa 7-0.
Arsenal walifanikiwa kutwaa kombe la FA kwa kuwafunga Man UTD kwa penati huku Bergkamp akitangaza nia ya kutundika njumu zake.
Shinikizo kutoka kwa mashabiki wakiimba "One more year!" "One more year!" likamfanya Bergkamp kubadili mawazo na kuongeza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.
Arsenal wakamaliza katika nafasi ya 4 kwenye msimu wa 2005/06 ukiwa ni wa mwisho kwa Bergkamp.
Mechi ya mwisho dhidi ya Wesbrom, Aprili 15,2006 iliitwa 'Bergkamp Day' ambapo mashabiki wa Arsenal walipewa jezi za rangi ya machungwa zilizoandikwa DB10. Kumbuka huo ulikua msimu wa mwisho kwa Arsenal kuutumia uwanja wa Highbury kama uwanja wao wa nyumbani.
Katika mechi hiyo, Bergkamp aliingia kipindi cha pili kama kawaida. Akatoa pasi ya goli kwa Robert Pires kisha akafunga goli lake la mwisho la mashindano kwa Arsenal dakika ya 89.
Heshima ya kuitumikia klabu kwa miaka 12 na kustaafu akiwa Arsenal ikampa zawadi ya mechi ya ufunguzi wa uwanja mpya wa Arsenal. Mechi dhidi ya Ajax Amsterdam ambako ndiko alikoanzia soka yake.
Kipindi cha kwanza cha mchezo huo kilichezwa na vikosi vya wakati huo vya timu zote mbili wakati kipindi cha pili kikichezwa na wachezaji wa zamani wa timu hizo kama David Seaman, Ian Wright, Marc Overmars, Petit na Viera kwa Arsenal na Marco Van Basten, Danny Blind na Ronald De Boer kwa Ajax.
Arsenal walishinda mchezo huo kwa mabao 2-1 huku Jan Klaas Huntelaar akiwa wa kwanza kufunga goli katika uwanja wa Emirates.
Huyo ndiye Dennis Nicolaas Bergkamp, mchezaji wa mwisho kustaafu soka akiwa na Arsenal. Siyo rahisi kumalizia soka lako Arsenal kwa sababu siyo timu yenye desturi ya kukumbatia wakongwe, lakini Bergkamp aliweza.
Nani kufuata? Tuna muda mrefu sana wa kusubiri kuona.
Imeandikwa na Richard Leonce Chardboy kutoka Wapenda soka (kandanda) group katika Facebook.
Nipate katika chardboy77@yahoo.com na @chardboy77 kwenye twitter au 0658399341

Berkamp vs Irwin |

No comments