THE GUNNING MACHINE
DENNIS NICOLAAS BERGKAMP NI WAKIPEKEE
( SEHEMU YA KWANZA)
Dennis Bergkamp |
Wakati nikipekua huku na kule kumtafuta kwa kina ndiyo wakati ambao uongozi wa uwanja wa Emirates ulikubali kujenga sanamu yake kama kumbukumbu katika uwanja huo wa nyumbani wa washika mitutu wa London.
Unaweza kumwita kocha msaidizi wa Ajax ya nyumbani kwao Uholanzi kwa sasa, akimsaidia kocha mkuu Franck De Boer.
Achana na hayo,lakini leo The Gunning Machine inakukumbusha miaka ya nyuma ambapo bunduki hii iliishi katika Ghala kubwa la silaha pale Highbury. Dennis Bergkamp katika klabu ya Arsenal.
Mtoto huyu wa fundi umeme alianza soka lake katika klabu ya Ajax akiwa na umri wa miaka 11. Akahamia katika klabu ya Internationale Milan ya Italia mwaka 1993 ambako alikuwa na misimu miwili migumu sana.
Mwaka 1995 klabu hiyo ikapata mmiliki mpya, Bwana. Massimo Moratti ambaye aliamuru kufagia wachezaji ambao walionekana mizigo kikosini.
Fagio hilo likamkuta Bergkamp. Bruce Rioch akiwa Kocha wa Arsenal wakati huo, akaamua kufungua pochi lake la kwanza na kutoa £7.5m kama ada ya uhamisho wa Mdachi huyo.
Ada hiyo ilivunja rekodi. Kwa taarifa yako kabla ya Bergkamp, rekodi kubwa ya usajili Arsenal ilikua £2.5 tu!, huu ubahili hakuanza Wenger hata kidogo!
Mechi ya ufunguzi wa msimu wa 1995-96, Bergkamp akacheza dhidi ya Middlesbrough. Kama unavyoelewa kuwa ligi ya England siyo lelemama, Bergkamp alicheza mechi 5 bila kuzigusa nyavu tena akiwa kama mshambuliaji wa mwisho.
Hatimaye Septemba 23,1995 akafanikiwa kufunga goli lake la kwanza dhidi ya Southampton katika uwanja wa Highbury. Msimu wa kwanza wa Bergkamp ukampa magoli 11 katika michezo 33. Arsenal ikamaliza katika nafasi ya 5.
Prof. Arsene Wenger akawasili na mpya katika klabu ya Arsenal. Akatambua kipaji cha Bergkamp na akaamua kumtoa katika nafasi ya mshambuliaji wa mwisho na kumweka katika nafasi ya nyuma ya mshambuliaji wa mwisho maarufu kama 'second striker'.
Akacheza mechi chache katika msimu wa 1996-97 kwenye nafasi yake mpya. Ikamkubali kwani alifanikiwa kupiga 'assist' 13 ikiwemo ile ya Novemba 1996 katika mchezo dhidi ya Totenham dakika ya 88 kwa nahodha Tony Adams kisha Bergkamp mwenyewe akafunga goli dakika za majeruhi.
Msimu uliofuata wa 1997-98 ulikua mzuri kwa Bergkamp kwani alifunga magoli 22 yaliyoipa Arsenal ubingwa wa ligi kuu na kombe la FA. Ni katika msimu huo Bergkamp alipoifungia Arsenal 'hat trick' yake ya kwanza dhidi ya Leicester City.
Akawa mchezaji wa pili kutoka nje ya England kushinda tuzo ya Mchezaji bora wa kulipwa (PFA).
Msimu wa 1998-99, Arsenal walishindwa kutetea ubingwa wao wa ligi kuu lakini Bergkamp alifanikiwa kufunga magoli 16. Wakafungwa na Manchester UTD katika nusu fainali ya kombe la FA kwenye mchezo ambao Bergkamp alikosa penati dakika za majeruhi matokeo yakiwa 1-1 na hatimaye katika kipindi cha pili cha muda wa ziada (extra time), Ryan Giggs akawatungua Arsenal.
1999-2000 haikwenda vizuri kwa Bergkamp na timu yake. Walishika nafasi ya pili kwenye ligi, pointi 18 nyuma ya Man UTD sambamba na kufungwa na Galatasaray kwa matuta katika fainali ya UEFA CUP.
Desemba 2000, Bergkamp akakubali kuongeza mkataba wake klabuni.
Arsenal wakashika nafasi ya pili kwa mara ya tatu mfululizo kwenye ligi kuu katika msimu wa 2000-2001 huku nafasi ya Bergkamp kwenye kikosi cha kwanza ikiwa kwenye hati-hati kutokana na uwepo wa Thierry Henry na Sylvain Wiltord. Sasa akawa akitumika kama 'Super Sub'....
Akiwa kama super sub hivo hivo, tukutane next time uone alichokifanya legend huyu hadi THE GUNNING MACHINE kusema ni wa kipekee ndani ya Arsenal.
Imeandikwa na Richard Leonce Chardboy kutoa Wapenda Soka Kandanda Group katika ukurasa wa Facebook
Nipate katika chardboy77@yahoo.com na @chardboy77 kwenye twitter au 0658399341
Huyo alikua amekamilika hakika, sitamsahau kamwe!
ReplyDeleteMchezaji simple lakini mwenye roho ya paka.
ReplyDeletekuna nchi zimebarikiwa kutoa wachezaji bora mojawapo ni Holland nadhani academies za soka ni muhimu sana
ReplyDeletejaap Starm,huyu jamaa,RVP,De Bouer.Roben,Kluivert n.k hawa ni baadhi tu lakini for sure jamaa wameweza tatizo tu hawana bahati when it comes to trophies