THE GUNNING MACHINE
THE VA-VA-VOOM!!!
Thiery Daniel Henry |
Kuna timu moja nchini Ufaransa inaitwa AS Monaco. Arsene Wenger aliwahi kuitwa kocha mkuu pale. Wakati huo palikua na winga mdogo raia wa Ufaransa akihangaika kupata namba katika kikosi hicho.
Miaka ikasogea, Arsene Wenger akaenda zake Japan kisha akaibukia Arsenal.
Yule kijana nae akaenda zake Italia katika klabu ya Juventus.
Ndani ya Arsenal, Arsene Wenger akatumia taaluma yake ya uchumi kufanya biashara murua ya kumuuza Nicolas Anelka. Mpaka leo hiyo inatajwa kua biashara nzuri kuwahi kufanywa na Wenger.
Wakati huo yule kijana alikua hana raha kabisa ndani ya Juventus,soka la Italia lilishindwa kumwingia kijana huyu.
Ndipo Arsene Wenger alipomkumbuka na Agosti 3,1999 akaweka mezani kiasi cha pauni milioni 11 ili kuungana na kinda lake hilo la zamani.
Hapa ndipo "The Gunning Machine" inapokita leo.
Siyo mwingine,ni Va-va-voom, Thierry Daniel Henry. Legend mwenye sanamu yake katika uwanja wa nyumbani wa Arsenal Emirates.
Anafika arsenal akionekana ni kijana wa kawaida tu,anakutana na habari ya kushangaza kutoka kwa kocha wake kwamba "utacheza kama mshambuliaji", Ilikua ni habari ya kushtua kwake na anasema mwenyewe kwamba, "sikutegemea kabisa kama naweza kucheza nafasi hiyo,lakini mimi ni mchezaji,nafasi ni majukumu tu"
Wasiwasi wa wataalamu wa soka ukatawala vyombo vya habari,hii ni baada ya Thierry Henry kuanza hovyo maisha yake ya soka nchini Uingereza. Akicheza mechi nane mfululizo bila kuliona lango.
Yeye mwenyewe akaanza kukata tamaa baada ya miezi migumu ya mwanzo katika ligi kuu,Henry alikiri kwamba, "nahitaji kuanza upya kujifunza mbinu za ufungaji".
Lakini wasiwasi ukaondoka baada ya kufanikiwa kufunga magoli 26 katika msimu wake wa kwanza wa 1999-2000 huku Arsenal ikimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Man UTD pamoja na kufungwa na Galatasaray katika fainali ya UEFA CUP.
Msimu wa 2000/2001 Henry alifanikiwa kuwa mfungaji bora wa timu yake ingawa hakufunga magoli mengi zaidi ya ilivyokua katika msimu wake wa kwanza.
Arsenal ikakosa ubingwa mbele ya MAN UTD. Henry anakiri kwamba jambo hilo lilimnyima raha.
Mgaagaa na upwa hali wali mkavu, hatimaye katika msimu wa 2001/2002,akaiwezesha Arsenal kutwaa kombe la ligi kuu na kombe la FA. Akafanikiwa kutwaa ufungaji bora wa ligi kuu pia,akifunga magoli 32 kwa msimu.
Msimu wa 2002/03 ulikua mzuri pia kwake kwani alifanikiwa kufunga magoli 32 na kutoa pasi 23 za mabao na kuiwezesha Arsenal kutwaa kombe la FA tena akiwa mchezaji bora katika mchezo wa fainali.
Akatwaa tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa (PFA) pamoja na tuzo kutoka kwa waandishi wa habari za soka (FWA).
Msimu wa 2003/2004,Arsenal ilitabiriwa mapema kutwaa ubingwa. Msimu huo ukamshuhudia Va-Va-Voom akiwa miongoni mwa wachezaji wa Arsenal waliounda ile Invinsible Arsenal ambayo ilitwaa ubingwa wa ligi bila kupoteza mchezo. Msimu huo Henry alifunga magoli 39 katika michuano yote na akawa mfungaji bora wa bara la Ulaya na kutwaa tuzo ya European Golden Boot.
Msimu wa 2004/2005,Arsenal ilipoteza ubingwa wake kwa Chelsea lakini ilitwaa kombe la FA katika mchezo wa fainali ambao Henry aliukosa kutokana na majeruhi. Msimu huo Henry alifunga magoli 31 na kutwaa tena tuzo ya mfungaji bora wa bara la Ulaya (European Golden Boot) kwa mara ya pili mfululizo lakini msimu huo akifungana na Diego Forlan.
Kuondoka kwa Patrick Vieira mwaka 2005 kukashuhudia Henry akirithi kitamba cha unahodha. Akawa na jukumu zito la kuongoza kikosi kilichosheheni vijana wadogo.
Kustaafu kwa Dennis Bergkamp kukampa Thierry Henry partna mpya katika safu ya ushambuliaji ya Arsenal ambaye ni Robin Van Persie.
2005/2006 ukawa wa mafanikio kwa Henry. Kwani Oktoba 17,2005 Henry akafunga magoli mawili dhidi ya Sparta Prague na kuvunja rekodi ya ufungaji ya klabu iliyokuwa ikishikiliwa na Ian Wright ya magoli 185.
Februari 1,2005 akafunga goli dhidi ya West Ham ambalo lilikua ni la 151 katika ligi kuu na kuvunja rekodi ya klabu iliyokuwa ikishikiliwa na Cliff Bastin. Pia msimu huo Henry alifunga goli lake la 100 katika uwanja wa Highbury.
Akamaliza msimu akiongoza kwa ufungaji katika ligi kuu na kwa mara ya tatu mfululizo akatwaa tena tuzo ya waandishi wa habari za soka FWA.
Akaiongoza Arsenal katika fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Barcelona ambapo Arsenal walipoteza mchezo huo.
Kushindwa kuipa klabu mafanikio kwa misimu miwili mfululizo kukamnyima raha Henry,lakini akakubali mkataba mpya wa miaka minne na akasema kwamba atamaliza maisha yake ya soka akiwa Arsenal.
Makamu mwenyekiti wa Arsenal David Dein alitanabaisha kuwa Arsenal walikataa ofa ya Pauni milioni 50 kutoka Hispania kwa ajili ya Va-va-voom. Kama dili hilo lingekubaliwa lingevunja rekodi ya dunia iliyokua ikishikiliwa na Zinedine Zidane
Msimu wa 2006/2007, Henry aliandamwa na majeruhi. Akacheza michezo 17 na kufunga magoli 10. Alimaliza msimu wake mwezi Februari kutokana na majeruhi,akakosa kipindi chote kilichosalia. Alijaribu kurejea mapema lakini ikashindikana.
25 Juni,2007 Arsenal wakakubali Pauni milioni 24 kutoka Barcelona na Henry akahamia huko kwa mkataba wa miaka minne.
Sasa,Henry ni mchezaji wa New York Redbulls ya Marekani. Katika msimu wa 2011/12, Henry alirejea Arsenal kwa mkopo wa muda mfupi na katika usiku wa kukumbukwa uliopewa jina la 'THE RETURN OF THE KING' katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Leeds UTD dakika ya 78, Henry anaingia uwanjani kuchukua nafasi ya Maroane Chammackh na bila ajizi,anafunga goli pekee na la ushindi na kuongeza heshima yake ndani ya Arsenal.
Henry alifanikiwa kufunga magoli matatu katika kipindi chake cha mkopo lakini bao moja dhidi ya Blackburn halikuhesabiwa baada ya kudaiwa kuwa bekiwa Blackburna alijifunga.
Yapo mengi yanayomhusu shujaa huyu wa arsenal,lakini kwa leo,hayo yanatosha kuonesha ni kwa nini katika uwanja wa Emirates kuna sanamu yake pamoja na kwamba anachezea klabu nyingine kwa sasa.
~AHSANTE~
Imeandikwa na Richard Leonce Chardboy kutoka Wapenda Soka 'Kandanda' group.
Nipate katika Chardboy77@yahoo.com au 0658399341
one of my best forward
ReplyDeletehivi jamaa mnadhani anaweza kua kocha hapo baadae?
ReplyDelete