THE GUNNING MACHNIE

             KARIBUNI TENA,TUKO PAMOJA.

The Gunning ground
Ni takriban mwezi sasa 'The gunning machine' haijaruka hewani,kwa wapenzi na mashabiki wake watakua wameimiss. Lakini sasa imerudi tena kwa jicho pana zaidi kuitazama Arsenal na Mavuno yake kwa mwaka huu 2013.

Yapo mengi ambayo tungeyazungumza kwa mwezi huu wa Januari lakini kwa bahati mbaya hatukupata fursa hiyo,lakini hiyo ilinipa mimi fursa ya kipekee ya kuichunguza vizuri Arsenal kwa mwezi huu na yapo ambayo nimeyaona.

Tulipoachana kwenye ile THE GUNNING MACHINE YA MWAKA MPYA ambayo ilizungumzia mikataba mitano kwa wachezaji wa Kiingereza pale Arsenal ambao ni Aaron Ramsey,Alex-Oxlade Chamberlain,Carl Jenkinson,Kieran Gibbs na Jack Wilshere, tulikua bado hatujatuliza roho zetu kwa uzuri.
Sasa tunakutana tena tukiwa tumeongeza mkataba wa Muingereza wa sita katika orodha ile,huyu si mwingine ni Theo Walcott. Theo amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu ukimwingizia pauni 100,000 kwa juma.Hii ni faraja kwani kila Siku tumekua tukitamani wachezaji wetu walipwe hivi au zaidi.

Lakini maana ya hiki kitu ni nini?
Maana halisi ni kwamba Tunajenga timu yetu. Walau tuna uhakika wa kuwa na timu iliyo pamoja kwa muda mrefu misimu miwili au mitatu ijayo.Tena ukiwa na wachezaji wenye mapenzi na timu yao na wengine wakianzia kwenye academy yako.
Ni kweli kwamba Alex Song aliuzwa kwenda Barcelona akiwa na mkataba wa miaka mitatu lakini sioni dalili ya jambo kama hilo kutokea tena katika kikosi cha sasa.

Kitu kingine kizuri kwa Arsenal kwa mwezi Januari ni viwango vya wachezaji kupanda. Imeshuhudiwa kiwango cha Jack Wilshere kinapanda kwa kasi na wataalamu wa mambo ya soka wanasema bado hajafikia ukomo wa kiwango chake yani bado ana mengi anayoweza kuyaonyesha.


Olivier Giroud akifunga magoli matano katika mechi Tatu mfululizo,inaonesha kwamba yupo kwenye kiwango bora kwa sasa na ameanza kuizoea ligi. Magoli manne ya Theo Walcott katika mechi tatu mfululizo pia pamoja na msaada wake mkubwa kwenye kikosi pia ni mwanzo mzuri wa smshambuliaji huyo huyo mpya ambaye bado ana kiwango cha kucheza kama Winga.

Pasi zenye macho za Lucas Podoski na uwezo wake mkubwa wa kufunga magoli ni faraja pia kwenye kikosi cha Arsenal kwa sasa. Unahitaji watu kama Podolski kwenye timu hasa mechi inapokupa mazingira magumu ya kupata ushindi. Nadhani wote tunakumbuka goli lake la kusawazisha dhidi ya Swansea katika mchezo wa kwanza wa kombe la FA mapema mwezi huu lilivoirudisha Arsenal mchezoni.

Tumeshuhudia pia kurejea kwa Thomas Rosicky na Abou Diaby waliokua majeruhi. Kiwango cha Diaby mara nyingi huchelewa kurejea kila anapotoka kwenye majeraha,lakini Rosicky tayari ameanza kuonesha cheche zake katika safu ya kiungo ya Arsenal.Akili zake nyingi zinamfanya aelewane vizuri na Lucas Podolski.
Sasa unaweza kumpumzisha Jack Wilshere na bado combination ya Cazorla,Rosicky na Podolski ikakupa mchezo mzuri.

Pamoja na hayo yote lakini timu yetu kwa msimu huu bado imeonesha udhaifu mkubwa wa kupambana hasa na timu kubwa.
Tumeshuhudia Januari ya vipigo kutoka kwa Man City na Chelsea bila kusahau droo dhidi ya Liverpool. Hilo linadhihirisha kwamba bado tutaendelea kuumwa njaa ya vikombe kwa sababu huwezi kutwaa ubingwa bila uwezo wa kupambana hasa na timu kubwa.

Tusitegemee muujiza katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.

Lakini tunapaswa kuelewa na dalili zipo kwamba timu yetu inajengwa.
Timu nzuri ni ile inayojengwa taratibu. Mara nyingine usajili mkubwa siyo tiba pekee. Unaweza kununua washambuliaji wenye hadhi ya Dunia kwa pesa nyingi kisha wakakupa matokeo kama ya Torres pale Chelsea.

Kwa ujumla hayo ndiyo tuliyoyaona katika kipindi ambacho hatukuwepo hewani. Sasa tumerejea na tegemea mazuri kutoka hapa.
Karibu tena na tupo pamoja.
Mungu wabariki wapenda soka, Mungu ibariki THE GUNNING MACHINE.

Imeandikwa na Richard Leonce Chardboy kutoka Wapenda Soka 'Kandanda'

 
Nipate katika chardboy77@yahoo.com au 0658399341

1 comment:

  1. Giroud nilimtabiria mazuri na ndo kinachoendelea

    ReplyDelete

Powered by Blogger.