MIWANI PANA YA EDO
KUELEKEA JUMATANO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA
REAL MADRID VS MAN UNITED
Ferguson vs Mourinho |
RONALDO ATOA ONYO KWA MAN UNITED
Wakati homa ya pambano kali la ligi ya mabingwa likipanda, Mchezaji nyota wa timu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo alifunga magoli matatu katika ushindi wa 4-1 walioupata nyumbani dhidi ya Sevilla katika La liga huku goli lingine likifungwa na BenzemaNilishuhudia mpira wa Kasi kutoka kwa kikosi cha Mourinho safari hii akiwatumia Kaka na Michael Essien katika kiungo.
Ushindi huo umewafanya Madrid kubaki katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi point 2 nyuma ya Atlentico Madrid na point 16 nyuma ya Vinara Barcelona.
Ushindi huo pia umetoa Onyo kwa Man United watakapotembelea Santiago Bernabeu Jumatano katika mechi ya kusisimua ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora.
Kwa upande wa Man united wao walikua na wikiendi nzuri kwani waliweza kupata ushindi wa wa 2-0 dhidi ya Everton magoli ya Giggs na Robin Van Perse na zaidi ya yote kuongeza wigo wa points kileleni mwa ligi kwa tofauti ya points 12 dhidi ya bingwa mtetezi Man City ambaye alipoteza kwa
3-1 huko St.Mary's nyumbani kwa Southampton.
HISTORIA INASEMAJE KUHUSU TIMU HIZI ZILIPOKUTANA?
Historia inasema timu hizi zimekutana mara 8 na katika hizo mechi Man United imeweza kushinda mechi 2 sawa na 25% wakati Real Madrid wao wameshinda mara 3 sawa na 37.5% huku droo zikiwa 3 sawa na 37.5%Mechi hii ni ya Kwanza kwa Mchezaji wa zamani wa Man United, Cristiano Ronaldo kucheza dhidi ya timu yake ya zamani na hii ikimfanya kila mpenda soka kutaka kujua nini kitatokea Jumatano hii.
Kwa upande wa Magoli katika michezo hiyo 8 Man United imefunga magoli 14 Wakati Real Madrid wao wamefunga magoli 17
Real Madrid inajivunia kuwa na kikosi bora kabisa huku ikijaza wachezaji waliosajiliwa kwa pesa nyingi kuzidi timu yeyote ile japokua kikosi hcho kimeonekana si lolote mbele ya Barcelona ambao ndo wanaongoza ligi kwa sasa tena kwa tofauti ya points nyingi tu.
Man United wao wanajivunia kuwa na wachezaji wenye "spirit na passion" ya mchezo huku ikichagizwa na safu kali ya ushambuliaji ikiongozwa na Mdachi Rud Van Perse na Wyne Rooney.
Miwani yangu pana Inatarajia kuona magoli mengi yakifungwa katika mechi hii hasa kutokana na kutokua makini kwa beki za pande zote huku pande zote zikiwa na safu kali za ushambuliaji.
Mara ya mwisho timu hizi kukutana Santiago Bernabeu, United ilifungwa goli 3-1 kabla ya United kuifunga Madrid 4-3 katika mechi ya marudiano Old Trafford mwaka 2003.
MECHI NYINGINE JUMATANO
Mechi zote hizi zitaanza saa 4:45 Usiku kwa saa za Africa ya MasharikiSHAKHTAR DONETSK VS BORUSSIA DORTMUND
.......Tukutane muda mwingine............
No comments