THE GUNNING MACHINE

  JEZI YA ARSENAL HAIMTOSHI KILA MCHEZAJI.

 
Santos

Unamjua Andre Santos?
Yule beki wa kushoto aliyesajiliwa na Arsene Wenger kutoka Fenerbache ya Uturuki kuziba nafasi ya Gael Clichy aliyetimkia Man City.

Amepelekwa kwa mkopo katika klabu ya Gremio ya nchini kwake Brazil. Hiyo ni timu sahihi kabisa kwake. Maisha ya England tena ukiwa katika jezi za timu kubwa kama Arsenal ni magumu sana. Muulize Jose Antonio Reyes atakuambia hataki kusikia lolote kuhusu Uingereza.

"The Gunning Machine" leo inawaangalia wachezaji sita ambao jezi za Arsenal zilikua kubwa sana kwao.

                   ANDRE SANTOS

 
Santos anaingia katika orodha ya wachezaji walioshindwa kabisa kumudu mchezo wa Arsenal na pia Anaingia katika orodha ya wachezaji wabovu kuwahi kusajiliwa na Arsene Wenger ambao "The Gunning Machine" imewaona.

Alisajiliwa kwa ada ya £6.2m Agosti 2011 lakini alishindwa kabisa kumudu majukumu yake kama beki wa kushoto ndani ya Arsenal. Alicheza michezo 13 tu katika ligi kuu kwa msimu mmoja na nusu aliokaa Emirates.

Aliwaudhi mashabiki wa Arsenal kwa kitendo chake cha kuchukua jezi ya Robin Van Persie wakati wa mapumziko, Arsenal walipocheza na Man UTD mapema msimu huu.

            SEBASTIEN SQUILLACCI

 
Huyu alisajiliwa kwa ada ya £4.5m baada ya Thomas Varmaelen kupata majeraha ambayo yalimweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Akacheza michezo 32 katika msimu wake wa kwanza wa 2010/11 lakini 'partnership' yake na Laurent Koscienly ilikua moja kati xa partnership mbovu katika ligi kuu.

Tangu aliporejea Varmaelen kutoka kwenye majeruhi, jezi ya Arsenal imekua kubwa sana na haimpendezi Squillacci.
Mchezo wake wa mwisho ni ule wa kombe la Capital One ambao Arsenal waliondolewa mashindanoni na timu ya Bradford. Hata Johan Djourou anatajwa kuwa bora kuliko Squillacci.

          MAROANE CHAMACKH

 
Arsenal walimpata bure mchezaji huyo raia wa Morocco kutoka Bordeux ya Ufaransa mwaka 2010. Alianza vizuri kiasi, akifunga magoli 11 katika mechi 22 za kwanzi. Baada ya hapo akaanza kuporomoka kwa mtindo wa kipekee kabisa.

Tangu Novemba 2010 mpaka leo, Chamackh amefunga magoli manne tu. Ndiyo, haujakosea kusoma, Chamackh amefunga magoli manne tu tangu Novemba 2010.
Kuna wachezaji huwa tunawaita wabovu kama akina Andrey Arshavin,Nicklas Bendtner na Pack Chu Young lakini hutokua sahihi ukimweka Chamackh mbele yao kwa sababu yeye alipata nafasi nyingi sana za kucheza na kufunga.

             PASCAL CYGAN

 
Usiombe kuvaa jezi namba 18 ya Arsenal. Kwa sasa inavaliwa na Sebastien Squillacci ambae nae yupo kwenye list hii, lakini iliwahi kuvaliwa na Mikael Silvestre ambae nae aliirithi kwa Pascal Cygan.

Cygan ni beki mfaransa ambae alisajiliwa kutoka Lille kwa ada ya £2m mwaka 2002. Alicheza michezo 98 kwa misimu minne lakini mtindo wake mbovu wa uchezaji pamoja na kukosa kasi vilikua vikiifanya mioyo ya mashabiki wengi wa Arsenal kupata kimuhemue kila alipokua akimiliki mpira.

                       RICHARD WRIGHT

Arsene Wenger amewahi kupata matatizo ya magolikipa mara kwa mara, wamepita watu kama Alex Manninger, Manuel Almunia na Lucas Fabianski. Hawa wote waliwahi kuwa na nyakati mbaya ndani ya Arsenal lakini walau walipata nyakati nzuri chache.

Huyu Richard Wright nadhani alivishwa jezi ya golikipa wa Arsenal kimakosa na ilimpwaya kwelikweli.

Alikuja mwaka 2001 akitajwa kuwa mrithi wa David Seaman lakini ilibidi auzwe msimu uliofuata kutokana na ubovu wa kiwango chake kuonekana na kutokua siyo golikipa sahihi.

                         FRANCIS JAFFERS.

Huwezi kumwacha FRANNY a.k.a 'fox in the box' kwenye list hii.
Mshambuliaji huyo akitokea Everton kwa ada ya £8m mwaka 2001. Alikutana na upinzani mkali kutoka kwa Thierry Henry na Sylvain Wiltord na akaishia kucheza michezo minne tu ya ligi kuu.

Faida pekee ilikua ni Charlton kukubali kulipa £2.6m mwaka 2004.

Ni wengi sana ambao jezi za Arsenal ziliwapwaya lakini kwa leo tuishie hapa.
"The gunning machine" inawataki wapenzi wa Arsenal kila la heri katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich usiku wa Jumanne ya Februari 19.

Imeandikwa na Richard Leonce Chardboy kutoka Wapenda Soka (kandanda) group.


Nipate katika chardboy77@yahoo.com au 0658399341

No comments

Powered by Blogger.