ARSENAL VS BAYERN MUNICH

KARATASI ZINAIBEBA BAYERN MUNICH

arsenal vs bayern munich


Arsenal hawajawahi kutwaa kombe la Klabu bingwa Ulaya, wamewahi kufika fainali mara moja. Hivyo hii ni nafasi yao kufanya hivyo msimu huu. Wanakutana na Bayern Munich ambao wamecheza fainali tisa na kushinda nne kati ya hizo.

Nani ataibuka kidedea katika mchezo huu wa hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League 2013 kati ya wapiga mizinga wa London na Mbogo wa Munich?

                                                             Arsenal


Walifanya shopping kwenye usajili lakini wamekua na msimu mbovu. Wamekua dhaifu katika ushambuliaji na wapo nje ya 'top four' ya ligi kuu ya England kwa pointi nne wakiwa hawajaifunga timu yoyote kati ya tatu za juu.

Hii inaonesha kwamba arsenal hawana uwezo wa kushindana na timu kubwa. Wameondolewa katika kombe la Capital na kombe la FA na timu za madaraja ya chini. Hili ndilo kombe pekee lililosalia kwa Arsenal kushindania msimu huu.

                              Bayern Munich

 
 


Ndiyo timu inayotajwa kuwa kwenye 'form' nzuri duniani hivi sasa. Wamepoteza mchezo mmoja tu kwenye Bundesliga msimu huu na wanaongoza msimamo wa ligi hiyo. Wameruhusu magoli 7 tu katika michezo 22. Ugenini ndo wanatisha zaidi kwani wameruhusu goli 1 tu katika michezo 11 waliyocheza.


                              Tathmini Ya Mchezo

Upande wa kushoto wa Arsenal utamkosa Kieran Gibbs ambaye ni majeruhi. Nacho Monreal ambaye anabanwa na sheria za UEFA kwa sababu alishaichezea Malaga kwenye michuano hii nae hatakuwepo.


Hii itamlazimu Arsene Wenger kumpanga Thomas Varmaelen kama beki wa kushoto, akiwaacha Laurent Koscienly na Per Martesacker kwenye 'central defence'.

Mario Gomez anaweza kuongoza mashambulizi ya Bayern Munich leo, Thomas Muller akitokea kulia atakakosimama Varmaelen.


Hii inaweza kumzuia Varmaelen kupanda mbele mara kwa mara kusaidia mashambulizi kwani atalazimika kukaa nyuma kuwasaidia Martesacker na Koscienly kwenye ulinzi.

Frank Ribery atakuwepo pia na bila shaka Bacar Sagna atakuwa na usiku mgumu. Hii inamaanisha mawinga wa Arsenal (Lucas Poldoski na Teo Walcott) watalazimika kufuata mipira nyuma kama Arsenal wataka kupita pembeni.

Kupona kwa Javi Martinez kunamaanisha kuwa Bayern watamtumia kwa pamoja na Bastian Schweinsteiger kwenye 'midfield' ambao wana nguvu kuliko viungo wa Arsenal.

Kwa upande wa Arsenal nafasi yao itategemea kiwango cha Mikel Arteta kwenye kiungo cha chini. Anapaswa kusaidiana na akina Koscienly na Martesacker kuhakikisha Javi na Schweinsteiger hawapitishi mipira kwenda kwa Muller na Ribery au 'pennetration passes' kwenda kwa Gomez. Na wakati huo huo atengeneze mahusiano mazuri kati yake na Jack Wilshere pamoja na Santi Cazorla.

Siyo rahisi kwa Arsenal kushambulia kupitia pembeni. Bayern wataziba njia hizo kwa kuwatumia Alaba upande wa kushoto na Philip Lahm upande wa kulia.


Ila Arsenal wanaweza kupita katikati huku wakitumia vema pengo la Holger Badstuber ambaye hatokuwepo. Pia uwezo mkubwa wa Jack Wilshere na Santi Cazorla kupiga mashuti au kupitisha pasi kwa Olivier Giroud.

HISTORIA INASEMAJE?

Timu hizi zimekutana mara 4 Arsenal ikishinda mara moja wakati Bayern Imeshinda mara 2 na mara moja iliisha kwa droo huku Arsenal Ikifunga magoli 4 na Bayern kufunga magoli 6 katika michezo yote hiyo

 


                              Utabiri Wangu.
Nikitazama ubora wa vikosi vyote viwili naona kama Bayern wana nafasi kubwa ya kutawala eneo la kuanzia katikati ya uwanja mpaka 1/3 ya upande wa Arsenal.

Hiyo inaweza kuwafanya Jack Wilshere na Santi Cazorla wageuke mabeki na ikiwa hivo hakutakuwa na nafasi ya Arsenal kushinda. Naweka karata yangu kwa Bayern Munich ingawa hii ni soka na mwamuzi ni dakika 90. Nimetabiri kwa kuangalia karatasi tu.


........Richard Leonce Chardboy (Wapenda soka group of facebook)...........

No comments

Powered by Blogger.