THE GUNNING MACHINE

                           NI KAMA KUPIGA DEKI KWENYE NYUMBA INAYOVUJA

Wakati naandika makala hii,Arsenal wanashika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.siyo nafasi nzuri kwao na hata mashabiki wanaamini timu yao inafaa kushika nafasi za juu zaidi kutokana ubora wa kikosi chao. Bacar Sagna,Kieran Gibs,Tom Varmaelen,Mikel Arteta,Santi Cazorla,Podolski,Giroud, Wilshere n.k ni bonge la kikosi kwa kweli.
Lakini kwa nini wanashika nafasi ya 5 mpaka sasa?
Capteni wa arsenal Varmaelen


              THE GUNNING MACHINE inajaribu kutoa maoni yake.

Ukiitazama Arsenal kwa haraka haraka unaweza kugundua tatizo katika safu yao ya ulinzi,utaona kama mabeki wa pembeni wa Arsenal wanavujisha,lakini tunatazama chanzo cha tatizo lenyewe. Ikumbuke mechi dhidi ya Man United pale Old Trafford, goli la kwanza la Man United lilitokana na makosa ya Andre Santos,hiyo ni kweli.
Lakini kwa soka la kisasa,beki wa pembeni siyo tena wa kariba ya Shadrack Nsajigwa wa Yanga,huu ni ulimwengu wa mabeki wenye maumbo madogo na kasi kwa ajili ya kupandisha mashambulizi,
Katika suala la ulinzi wanahitaji back up kubwa.so mimi naamini waliopaswa kum-back up Andre Santos ndiyo wa kulaumiwa.
                                                   
                                                        TATIZO NI NINI?
Arteta, Cazorla na Wilshere kwa sasa wanapandisha timu vizuri tu,lakini tatizo lao ni kukosa roho ya paka pale katikati.Wana kitu kinaitwa 'Soft Core'.panakosekana ugumu aliokua nao Alex Song japo nae hakua akiutoa kikamilifu kama enzi za kina Manu Petit,Vieira na Gilberto.
Abou Diaby anaonekana kufiti kiasi katika nafasi hiyo.unaweza usielewe kwa nini wachezaji kama Michael Carick,Diaby,Shaban Nditi. Siyo vipenzi vya mashabiki lakini mara nyingi hufanya wanavyoelekezwa na makocha.
Tazama ukweli huu,
 "katika dakika 344 alizocheza Diaby katika ligi kuu, msimu huu Arsenal wameruhusu goli 1 tu"
unaweza kupata picha hapo kwanini Diaby ni mchezaji bora.
Lakini kwa upande mwingine Diaby ni tatizo Arsenal.hii ni kutokana na majeraha yake ya kila mara na anaporudi huchelewa kupata "form" yake,anapoanza kukaa vizuri anaumia tena.kibaya zaidi ni kuwa Wenger anamtegemea sana na historia inaonesha kuwa hajawahi kuishi bila mtu mrefu pale katikati. Kumbuka enzi za Patrick Vieira.
                                                        Roy Kean vs Vieira
Tatizo lingine ni upya wa kikosi cha arsenal. Hili limegawanyika katika sehemu mbili.
Kuna wachezaji waliojiunga na Arsenal msimu huu,na kuna wachezaji wanacheza nafasi ambazo hawajazizoea.
Namtazama Lucas Podolski ambaye ni mgeni kikosini,Santi Cazorla ambaye pamoja na ugeni wake,bado anacheza nafasi mpya kwake.
Cazorla amezoea sana kucheza kama winger wa kulia au kushoto na siyo kutokea katikati,ndiyo maana mara nyingi utamwona anakimbia na mpira kutoka katikati halafu anaelekea pembeni halafu  anakua kama anazunguka kuingia kwenye boksi (kumbuka goli lake dhidi ya liverpool).
 Kama sivyo basi atapiga shuti au kutoa pasi kwa Podolski. Kwa kiasi kidogo sasa hivi ameanza kuingia kutokea katikati.
Jack Wilshere pia ni kama mgeni pale,wengi aliocheza nao kabla hajapata majeraha hawapo tena, waliopo ni wapya kabisa kwake. Ndiyo maana utaona wakati mwingine anapoteza pasi isivyo kawaida.
Mikel Arteta nae anacheza nafasi tofauti na ile ya maisha yake ya nyuma.kwa asili yake yeye ni kiungo mshambuliaji, inamuwia vigumu kidogo kucheza nafasi ambayo hajaizoea ndiyo maana hadi sasa ametoa 'assist' 1 tu tofauti na Song alivyokua akicheza nafasi hiyo. Wote tunamkumbuka Song alivyokua 'master' wa 'assist' msimu uliopita.
Tatizo lingine ni kwenye safu ya ushambuliaji ambako kuna picha ya Olivier Giroud.Huyu ni mfungaji bora wa league 1 msimu uliopita hivyo sina shaka na uwezo wake.Ni bonge la straika tatizo lake ni ugeni katika ligi na bado wenzake hawajamwelewa vizuri Giroud, tunaweza kukubali kumpa muda.

                                                    NINI KIFANYIKE?

"The Gunning Machine" inaona kama anahitajika Kiungo mkabaji mwenye mapafu makubwa (mapafu ya mbwa) na mwenye uwezo wa kucheza 'box to box'  kama Yaya Toure kwa sababu Diaby siyo wa kumtegemea sana na hata Emmanuele Frimpong hajafikia kiwango ninachozungumzia hapa.
Nadhani mtu kama Mohamed Diame wa West Ham anaweza kabisa kujibu tatizo hilo kama akisajiliwa na kutumika vizuri.
 
Arsenal inaishi kiujanja ujanja. Ukichunguza kikosi kilivyo utagundua viungo wa ulinzi ni Francis Coquelin pekee ambaye nae sidhani kama anamudu vizuri nafasi hiyo.
Sioni sababu ya kutumia pesa nyingi kununua mshambuliaji mwingine kipindi hiki ambacho timu ina ma-winga wengi wenye uwezo wa kucheza kama washambuliaji nao ni Lucas Podolski,Gervinho na Walcott na hivyo kutoa nafasi kwa mawinga wengine kama Tom Rosicky,Serge Gnabry na Alex-Oxlade Chamberlain.
Kikosi hiki kikikaa pamoja kitakua kizuri sana.lakini kama tabia ya kuuza wachezaji muhimu ikiendelea, tutakua kama tunapiga deki kwenye chumba kinachovuja.
Kazi bure.
                 Tukutane tena wiki ijayo.
              Ahsanteni
Imeandikwa na Richard Leonce Chardboy kutoka ktk group la wapenda soka.
Ungana nami kupitia kwa maoni na ushauri
0658399341

No comments

Powered by Blogger.