Messi kuongeza mkataba Barca mpaka 2018
Lionel Messi amekubali kusaini mkataba mpya na Barcelona, mkataba utakao muweka kwenye klabu hiyo ya Hispania mpaka mwaka 2018.
Muajentina huyo mwenye umri wa miaka 25, hivi karibuni amefanikiwa kuweka rekodi kwa nchi na klabu yake kwa kuweza kufunga jumla ya magoli 90 ndani ya mwaka 2012.
Pia mlinzi wa timu hiyo Carles Puyol, 34, na kiungo Xavi Hernandez, 32, nao pia wamekubali kuongeza mikataba yao itakayowaweka Barcelona mpaka mwaka 2016.
"Ndani ya wiki chache zijazo Puyol, Xavi na Messi watasaini mikataba yao” taarifa toka klabu hiyo imeeleza.
"Habari hii inamaanisha kwamba FC Barcelona imefanikiwa kuwatia kitanzini wachezaji wake watatu muhimu."
Mkataba wa Messi unategemea kuisha June 2016, wakati wa Puyol utaisha mwaka 2013 na Xavi unategemea kuisha mnamo mwaka 2014.
Wachezaji hawa watatu wote ni matunda toka akademi ya timu hiyo.
Messi amekuwa na Barcelona toka akiwa na umri wa miaka 13, na mchezo wake wa kwaza kwenye ligi alicheza akiwa na umri wa miaka 17, kwenye mechi waliyocheza dhidi ya RCD Espanyol mnamo tarehe 16 Oktoba 2004.
Kiwango chake bora cha ufungaji kwa mwaka 20112 kimemfanya avunje rekodi ya miaka 40 iliyokuwa imewekwa na Gerd Mueller, aliyekuwa amefunga jumla ya magoli 85. Messi alifanikiwa kuivunja rekodi hiyo mnamo Desemba 9 pale alipoweza kufunga kwenye mechi dhidi ya Real Betis iliyoisha kwa ushindi wa magoli 2-1.
Kama haitoshi siku ya jumapili Messi alijiongezea magoli kwenye rekodi yake mwenyewe, aliweza kuifungia timu yake magoli mawili kati ya manne ambayo timu yake ya Barcelona ilishinda dhidi ya Atletico Madrid, kuweza kufikisha jumla ya magoli 90 mpaka sasa huku mwaka ukiwa bado haujisha.
Ameweza kufunga magoli mawili kwenye mechi zote nane za mwisho ambazo alianza.
Messi yupo kwenye mchakato wa kutangazwa mchezaji bora wa dunia kwa mara ya nne, akiwemo kwenye list ya wachezaji watatu wanaowania tuzo hiyo sambamba na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na mchezaji mwenzake wa Barcelona Andres Iniesta.
Puyol, alianza kuichezea Barcelona mnamo mwaka 1999 kabla ya kupewa ukeptaini wa timu hiyo mnamo mwaka 2004, mwaka ambao Messi alianza kucheza mechi yake ya kwanza ya ligi na timu hiyo. Amecheza jumla ya mechi 560 mpaka sasa na amekuwa kapteni wa klabu hiyo aliyebeba makombe matatu ya Klabu Bingwa, matano ya La Liga na mawili ya Copa del Rey.
Xavi ndie mchezaji wa Barcelona aliyecheza kwa muda mrefu na timu hiyo kati ya hao watatu, alianza kuichezea timu hiyo mnamo mwaka 1998. Anashikiria rekodi ya kucheza mechi nyingi kuliko mchezaji yeyote wa Bacelona akiwa amecheza jumla ya mechi 651 mpaka sasa.
Mpaka sasa, Barcelona wapo kwenye nafasi nzuri ya kutwaa kombe la La Liga na itakuwa ni kwa mara ya 22. Wapo mbele kwa poiti 9 kwenye msimamo wa ligi, wakiwa wameshinda mechi 15 kati ya 16 walizocheza mpaka sasa.
No comments