MIWANI PANA YA EDO KUELEKEA KATIKA PAMBANO LA TAIFA STARS VS ZAMBIA
Taifa Stars |
Si jambo la kushangaza sana kuiona timu ya Taifa ya Spain au Hispania ikicheza bila kua na Mshambuliaji na bado wakazifunga timu nyingi na ngumu duniani na hili linatokana na uwepo wa Viungo bora zaidi katika kikosi hicho kama Xavi,Iniesta,Fabrigas na Alonso kwani wamekua na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kupeleka mashambulizi kwa pasi fupi fupi zenye macho.
hapa naizungumzia timu ya kwanza kwa ubora wa soka duniani.
Sasa turudi katika mada husika na hapa tukiangalia Timu yetu ya taifa maarufu kama Taifa Stars inayonolewa na kocha Kim Poulsen raia wa Denmark anayekubalika miongoni mwa mashabiki hasa baada ya kuirudisha timu katika mfumo wa kucheza soka la kuvutia huku akiwatumia wachezaji vijana Itaingia katika uwanja wa Taifa Dar es salaam Kuwavaa mabingwa wa Afrika na timu bora ya mwaka Barani Afrika Zambia maarufu kama Chipolopolo kuanzia saa kumi jioni.
Chipolopolo |
Taifa Stars Inaingia bila ya wachezaji wake Muhimu Mbwana Samata, Tom Ulimwengu na Mtu muhimu zaidi katika siku za Karibuni katika kupachika magoli John Bocco maarufu kama Adebayor hawa wote wataikosa mechi hiyo kwakua ni majeruhi, Hivyo Stars itakua ikiwatumia zaidi viungo katika kushambulia akiwemo Shabani Nditi, Frank Domayo,Amri Kiemba na Mwinyi Kazimoto na nafasi ya ushambuliaji akiachiwa mchezaji mpya katika timu hiyo Khamis Mcha Khamis maarufu kama Vialli kutoka Zanzibar na klabu ya Azam ya Dar es Salaam na Winga mshambuliaji wa timu hiyo Mrisho Khalfan Ngassa ambaye ataonekana dimbani mara ya kwanza tangu kuzuka mgogoro wa uhamisho wake kwenda El Mereckh ya Sudan.
Khamis Mcha Khamis
Sina shaka na upande wa ulinzi katika timu yetu kuanzia golini Juma Kaseja. mabeki Erasto Nyoni,Nadir Haroub 'Canavaro', Yondani,Kapombe,Maftah,Agrey Moris hawa wote wana uzoefu na mechi kubwa.
Hawa watakua na kazi kubwa ya kuwazuia Zambia wakiwa na mchezaji bora wa BBC Chiss Katongo, Felix Katongo, Stoppila Sunzu n.k
Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikua katika mchezo wa kirafiki Tarehe 21/11/2007 hapa Tanzania na Taifa Stars kushinda 1-0
NINI TUKITEGEMEE KATIKA PAMBANO HILO?
Pambano hilo litatazamwa na Africa nzima kama sio dunia kwakua Zambia ndiyo mbabe wa Africa na hii itawapa morali wachezaji wetu wanaotaka kujitangaza na Ni pambano ambalo ni muhimu kwa Taifa Stars ambayo haijulikani katika soka wakati kwa Zambia ni pambano la maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afica baadae Januari hivyo wasingependa kupata majeruhi hapa hivyo basi natabiri kuwa Stars Itashinda 2-1.MUNGU IBARIKI TAIFA STARS!!!
MUNGU IBARIKI TANZANIA..
well kwa upande wa watanzania ni kitu cha kujivunia kucheza na bingwa wa afrika lakini je tunaiga mfano wao wanaotumia hili ndo swali ambalo hata kiongozi wa tff hawezi kulijibu na mimi nachoona hapa kwetu cha kwanza ni mchezaji kujitambua ndio la maana
ReplyDeleteBab hapo TFF wanachozingatia kiingilio na mapato sio strategies za kufikia pale wenzetu walipofikia thats why wachezaji kama Mbwana wanazingua wakijua wananufaisha watu ambao hawana upeo wa maendeleo
ReplyDelete