SAO PAULO YAMSAJILI MCHEZAJI ANAYETUMIKIA KIFUNGO GEREZANI
Breno |
Breno alihukumiwa Kifungo cha miaka mitatu na miezi tisa gerezani baada ya kukutwa na hatia ya Kuchoma moto nyumbani kwake Munich akichagizwa na ulevi wa Pombe mwezi Oktoba 2011.
Sao Paulo wametangaza kumsajili beki huyo kwa mkataba utakaoanza Oktoba 7,2015 muda ambao ndo atakua akitoka gerezani.
Taarifa zilisema "Tunataka kumwonyesha Breno kua tunamjali, tunampa ulinzi na kumhakikishia maisha mazuri baada ya kifungo na zaidi kuipa 'sapoti' familia yake" zilisema taarifa hizo.
wakati wa hukumu yake madaktari walimchunguza na kugundua kama ana msongo wa mawazo na vyombo vya habari vya Ujerumani vimeripoti kua ameanza kurudia hali yake huko gerezani.
Ikumbukwe mkataba wa Breno utaanza kutumika mara baada ya kutoka gerezani.
No comments