KOPO LA CHUMVI CHAFU LIKIWA JIKONI NA CHAKULA KITAMU TAYARI MEZANI


 Jua kali linapiga utosini,uku minyoo inasumbua tumboni.mama yupo jikoni ila mambo hayaendi sawa.
Natupia jicho jikoni,naona mama anahangaika pasi na kujua nini anatafuta.bila kusita napiga hodi jikoni nakumuuliza mama nini tatizo?

 Nikapewa jibu ambalo halina mashiko tena la kustaajabisha "mwanangu siioni chumvi na sikumbuki niliweka wapi" hilo ndo lilikua jibu la mama, jibu lenye sentesi mbili za kustaajabisha.
Mwanangu sioni chumvi ilikua sentesi ya kwanza ya mama, loh! kumbe mama anshindwa kuendelea kupika sababu ya madini chumvi? Upande wa pili wa jiko naona viungo vingine vingi,tena vya bei mbaya kuliko madini chumvi.iriki,hamdalasini na binzali ndo nilivyovigundua haraka kwa uelewa wangu mdogo wa mapishi, lakini ni kiungo kimoja tu kilichomzuia mama kupika.viungo vya maelfu havikumshawishi mama aendelee kupika, lakini kiungo chumvi chenye thamani ya shilingi mia mbili? Kiungo hiki cha ajabu si lazima uende super market ili ukipate,wakina shayo, Swai na Sanga wamerahisisha upatikanaji wake yani kinapatikana kwa urahisi kuliko dhahabu na almasi,lakini bila dhahabu na almasi maisha yatasonga tu lakini vipi bila madini chumvi.? Haya ndo maajabu ya madini chumvi yanayomuangaisha mama.
Sentensi ya pili ya mama anasema hakumbuki alipoweka,bila kupoteza muda wala kufikiria sana ikabidi nianze kumsaidia mama kutafuta madini chumvi maana sehemu ya utumbo wangu ulikua umejikunja.pembeni ya jiko kulikua na kabati zuri la kahawia,lenye vioo vizuri ndani yake kuna vyombo safi vya kuhifadhi na kulia chakula,lakini ndani kwa bahati mbaya sikuona madini chumvi. Lakini sikukata tama nikaendelea kutafuta ndipo nikainama kuangalia chini ya uvungu wa kabati,kulikua na tandabui wengi sana cha ajabu hapo ndo nilipokuta kopo lililohifadhi madini chumvi,ungeliona usingeamini kama kopo ndio limehifadhi chumvi tunayotumia kupikia chakula. Kopo hilo chafu ndo lenye nakshi muhimu na siri kubwa ya vyakula vingi vitamu,loh! chakula kitamu mezani kopo la chumvi chafu jikoni, hakuna anayejali usalama wa chumvi jikoni labda kidogo wenzetu wa kwenye mahoteli makubwa.
Duniani kuna makopo mengi ya chumvi tena machafu kweli kweli ila yamebeba chumvi nzuri zenye kuleta faida kwenye taifa husika.
     ‘MWALIMU’ ni jina jepesi kulitamka pia ni kichefuchefu kwa waliokata tamaa na waloridhika. Ngoja niseme kidogo kwa makopo ya chumvi ya soka ya hapa nchini kwetu maana wenzetu wa mahoteli makubwa wamejua kuyatunza makopo yao. Ndo maana Julia Cosma ni kopo la chumvi la Messi halilali njaa. Hapa kwetu kuna makopo ya chumvi mengi sana lakini mengi kama si yote yapo uvunguni mwa kabati,
Kuna mtu anaitwa Zagalo huyu jamaa blangata yake imesimama sana kwenye soka huyu jamaa anapatikana maeneo ya sinza, wapo wengi kama yeye kila kona ya nchi. Hapa John Bocco,Athman Chama na Haruna Moshi 'boban' wanaelewa nasema nini.
                                      Zagalo akitoa maelezo kwa wachezaji wa Sinza Star

Huyu jamaa yupo uvunguni lakini chumvi yake imepiga mabao matano kwenye CECAFA CHALLENGE CUP Pale Kampala na sisi tukaonekana tuna mshambuliaji.
                                                 John Bocco akiwa Taifa Stars
 Nazungumzia Mabao aliyopiga John Bocco zao la huyu jamaa ambaye hakuna anayemfahamu zaidi ya wafatiliaji wa Ndani wa soka letu
                                                            Boban akiwa kazini
TFF ingejali mchango wa kina ZAGALO kwa kufungua academy ya soka hata moja ili waokoe chumvi nyingi zinazopotea mtaani…………............ itaendelea
 
Imeandikwa na Allen Kaijage kutoka Wapenda Soka(kandanda) group 

1 comment:

  1. tatizo dogo tu mwalim ni kama mtu anaewekwa tu asiye na uamuzi wala mamlaka juu ya viongozi wake hilo ndio tatizo kubwa liliopo kwa vilabu vyetu, mwalimu hana mamlaka juu ya viongozi walomchagua

    ReplyDelete

Powered by Blogger.