MIWANI PANA YA EDO KATIKA MECHI ZA JUMAPILI EPL


Ni moja kati ya JUMAPILI Kubwa katika Soka la England Zikishuhudiwa Manchester City wakiikaribisha Manchester United, Everton Wataikaribisha Totenham Hotspurs Wakati katika uwanja wa Upton park Wagonga nyundo wa London watawakaribisha Liverpool
hii inaifanya Jumapili hii kwa wapenda soka kusitisha shughuli muhimu za kijamii ili wasipitwe na mipambano hiyo. Miwani yangu leo nimeitupia katika mechi hizi na ifuatayo ni tathmini yangu fupi.
                  

                           MAN CITY VS MAN UNITED Saa 10:30 Jioni



Ni mechi ngumu ambayo wachambuzi wa mambo wanaiweka kama mechi ya kupigania ubingwa baada ya kuonekana wako Imara katika mbio za ubingwa.
Man United Wamefunga mabao mengi sana msimu huu wakati pia wakiruhusu kufungwa mabao mengi.

 Wenyeji Man City watawakosa David Silva alie majeruhi na nafasi yake kujazwa na Javi Garcia katika upande wa kiungo mkabaji. Wamo pia Micah Richards na James Milner ambao ni mashaka kwao kuanza
Kwa upande wa Wageni Man United wana orodha ndefu ya majeruhi watakaoikosa mechi hii wakiwemo Anderson,Vidic,Luis Nani na Shiji Kagawa wakati Jumamosi zilitoka taarifa za kuwemo  mazoezini kwa Valencia na Tom Cleverley.

Man United Inaingia uwanjani leo huku Ikiongoza katika ligi kwa kua na point 36 lakini Ikiwa na beki zisizoaminika mpaka kupelekea Kocha Ferguson kuita ni "cartoon defending" Wakati Man City wanaingia uwanjani wakiwa katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi na point 33 wakichagizwa  na Ukuta Imara unaoimarishwa na Uwepo wa Viungo Hodari hasa Yaya Toure.

 


                                                      UNAYAJUA HAYA?
  •  Goli la penati alilofunga Wyne Rooney wikiendi iliyopita limeingia katika historia ya goli la 1000 tangua kuanza kwa karne hii.
  • Carlos Tevez na Ryan Giggs ndo wachezaji pekee katika vikosi vya leo waliozichezea timu hizi mbili kwa nyakati tofauti.
  • Man United Wameweza kuokoa pointi 21 ambazo walishakaribia kupoteza baada ya kutangulia kufungwa na kurudi katika staili ya "comeback"
  • Man City ndo timu pekee katika Epl tangu msimu kuanza hawajawahi kupoteza mchezo wowote wakati Man United ndo timu pekee ambayo haijawahi kutoa droo katika msimu huu.
  • Robin Van Perse ndo mchezaji anayeongoza kwa upande wa Man United katika kupachika mabao akiwa na Magoli 10 Wakati Carlos Tevez akiongoza kwa upande wa Man City akiwa na magoli 7.
  • Katika mechi 6 zilizopita kati ya timu hizi katika uwanja wa Etihad Man United imeshinda 1-0 mara 3 wakati mwaka 2006 ndo ilikua mara ya mwisho kwa Man City kushinda zaidi ya goli moja katika uwanja wa Etihad ilishinda 3-1.
 
                                    

                                       MAMBO YA KUKUMBUKWA

                  KATIKA MECHI 162 ZILIZOWAHI KUCHEZWA KATI YA TIMU HIZO;

  Man City imeshinda mechi 45 Sawa na 27.8%
  Man United Imeshinda mechi 67 sawa na 41.4%
  Wakati timu hizo zimedroo mechi 50 sawa na 30.9%.
  Man city ikifunga magoli 219.
  Man United ikifunga Magoli 235.
  Ushindi mkubwa wa man City dhidi ya Man United ukiwa ni 6-1 katika uwanja wa Nyumbani wa United Old Trafford msimu wa 2011/2012
  Wakati ushindi mkubwa wa Man United dhidi ya Man City ni 5-0 Katika Uwanja huo huo Old Trafford msimu wa 1994/1995.
      
   >>>  Utabiri wangu ni 2-2 <<<<<


         EVERTON VS TOTENHAM HOTSPURS saa 12 jioni





Spurs chini ya AVB wanaenda kucheza Goodson Park wakiwa katika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi wakijikusanyia point 26 sawa na Wes Brom huku wakichagizwa na ushindi mara tatu mfululizo katika michezo iliyopita wakimtegemea sana Defoe katika ufungaji akiwa na magoli 9 katika ligi nyuma ya Michu,RVP,Demba Ba na Luis Suarez
Kwa upande wao Everton wameanza msimu vizuri kazi kubwa ikifanywa na Fellain na Jelavic katika kupachika mabao na kuwafanya kushika nafasi ya 7 wakiwa na pointi 23 point 3 nyuma ya Spurs.
 
 

                                              MAMBO YA KUKUMBUKWA

                               KATIKA MECHI 163 KATI YA TIMU HIZI
 
 Everton  imeshinda mechi 54 Sawa na 33.1%
 Spurs  Imeshinda mechi 60 sawa na 36.9%
Wakati timu hizo zimedraw mechi 49 sawa na 30%
  Everton  ikifunga magoli 218
  Spurs ikifunga Magoli 246
Ushindi mkubwa wa Everton dhidi ya Spurs ukiwa ni 5-2 katika uwanja wa Nyumbani wake wa nyumbani  msimu wa 1934/1935
Wakati ushindi mkubwa wa Spurs dhidi ya Everton  ni 10-4 Katika Uwanja wa White Hart Lein msimu wa 1958/1959
        >>>>> Natabiri Spurs kushinda 2-1 <<<<

 

                        WEST HAM UNITED VS LIVERPOOL saa 1 usiku.

 


 


 

West ham United maarufu kama wagonga nyundo wa London  wanaikaribisha Liverpool ikiwa na matokeo mazuri katika uwanja wake wa nyumbani na ikiwa katika nafasi ya 10 katika msimo wa ligi ikijikusanyia point 22 itakua inatafuta nafasi ya kupanda katika msimo wa ligi na kama ikishinda leo basi itapanda mpaka nafasi ya 6 na kuishusha Arsenal. Watakua wakimtegemea zaidi nahodha Kevin Nolan na Diame
Liverpool baada ya ushindi wa Europa ligi katikati ya wiki inasafiri kuwavaa Wagonga nyundo bila ya kua na mshambuliaji wake tegemezi Luis Suarez mwenye kadi 5 za njano . Liverpool inashika nafasi ya 12 katika msimao wa Ligi na safu yao ya ushambuliaji leo itaongozwa na Steve Gerrard na Handerson.       
                        
                         
                      UNAYAJUA HAYA?
  • West Ham wameshinda mechi moja tu kati ya mechi 6 zilizopita katika EPL dhidi ya Liverpool
  • Luis Suarez amekosa michezo 8 tu tangu ajiunge na Liverpool ambayo katika michezo hiyo Liverpool imeshinda minne tu.
  • Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers hajawahi kucheza na West Ham tangu aanze kazi yake ya kufundisha soka
  • Mara ya mwisho timu hizi kukutana Upton Park West Ham walishinda 3-1 

 
                                  HISTORIA INASEMAJE?
                           
 
HIZI TIMU ZIMEKUTANA MARA 122

 West Ham imeshinda mechi 24 Sawa na 19.7%
  Liverpool Imeshinda mechi 64 sawa na 52.5%
Wakati timu hizo zimedraw mechi 34 sawa na 25.4%
  West Ham ikifunga magoli 116
  Liverpool ikifunga Magoli 204
Ushindi mkubwa wa West Ham dhidi ya Liverpool ukiwa ni 7-0 katika uwanja wa Nyumbani wake wa nyumbani Upton Park msimu wa 1930/1931
Wakati ushindi mkubwa wa Liverpool dhidi ya West Ham ni 6-0 Katika Uwanja wa anfield msimu wa mwaka 1983/1984


>>> Utabiri wangu West Ham 2-1 Liverpool<<<<

...................Tukutane baada ya mechi hizi tukiangalia yaliyojitokeza katika miwani yangu pana katika soka.

                                             kwa maoni 0762 42 72 72 au wapendasoka@gmail.com
 



4 comments:

  1. Mechi itakua ngumu sana na naamini beki za man utd leo zitakua imara zaidi kuliko walivyokua katika mechi zote za msimu huu!
    Upande wa mashambulizi amtumie RVP pamoja na Rooney ambae nadhani leo hii atakua na kazi ya kusaidia kiungo! Rafael, Evra sina wasi wasi nao ila 4 na 5, Ferdinand na Jones itakua poa zaidi!
    Pale kwenye kiondn aache mapenzi na Fletcher, Carrick, scholes, Young, na Valencia chaguo langu! Kwa kipa aanze na De Gea

    ReplyDelete
  2. Valencia alionekana mazoezini jana so anaweza akaanza hofu yangu iko kwa Maicon huyu jamaa jembe bana

    ReplyDelete
  3. mancini hes undergraduate coach believ me huwezi kwenda kwenye derby ukaanza na bollatelli,wakati tevez yupo bench hes not seriouz at all warabu wanajicheleweshea mda wa maendeleo kwa yule jamaa

    ReplyDelete
  4. sijui kawapa nini aisee

    ReplyDelete

Powered by Blogger.