MAISHA YA SIR. ALEX FERGUSON KATIKA SOKA

 
 
 
 
 
 
                                                              Sir ALEX FERGUSON

Alexander Chapman Ferguson ni zao la Alexander na Elizabeth mnamo 31/12/1941
huko Glasgow, Scotland.
Fergie pamoja na mkewe Cathy wana watoto watatu wakiume; Mark na
mapacha, Darren na Jason.
Darren pekee ndie amefuata nyayo za baba yake katika ufundishaji
ambapo anafundisha Peterborough United
                                                     Darren Ferguson

Katika kucheza mpira Sir Alex Ferguson amecheza club zifuatazo;
Queen’s Park FC (1957-60)
St. Johnstone FC (1960-64)
Dunfermline Athletic FC (1964-67)
Rangers FC (1967-69)
Falkirk FC (1969-73)
Ayr United FC (1973-74).
Akiwa mshambuliaji Sir Alex Ferguson alifunga magoli 167 katika
michezo 327 aliyocheza
                                       Alex Ferguson aliposain kuichezea Glasgow Rangers

Katika umri wa miaka 32, Sir Alex Ferguson akaanza ufundishaji mpira
mwaka 1974 East Stirlingshire FC(part-time)
Ufundishaji kamili aliuanza katika timu ya St.Mirren FC, aliisaidia
timu kushinda The Scottish First Division(1976-7 ­7), katika timu hiyo
aliibua vipaji kama Billy Stark, Tony Fitzpatrick, Lex Richardson,
Frank McGarvey, Bobby Reid and Peter Weir.
Mwaka 1978 alijiunga na Aberdeen Football Club (FC), Sir Alex Ferguson
alipata heshima pamoja na kuaminiwa baada ya Dons kushinda 5-0 katika
siku ya mwisho wa ligi ya Skotland(1979/1980).
Katika mbinu na nidhamu ya hali ya juu aliiwezesha Aberdeen kushika
nafasi ya 2 katika misimu miwili ya Scottish League Cup (1978-1980), na
ubingwa wa Scottish Premier Division(1979-1980).

Akaendeleza ujuzi wake kwa kuiwezesha Aberdeen kushinda mataji kadhaa yakiwemo
  • The Union of European Football Associations (UEFA) Cup Winners’ Cup in 1982-83
  • The Uefa Cup
  • Scottish Football Association (SFA) Cup mara 4,misimu 3 mfulurizo 1981-1984 na 1985-1986
  • Scottish Premier Division misimu 2 mfulurizo 1983-85
  • The Scottish League Cup(1985-86)




Itaendelea..... ­..

>>>>>> Imeandaliwa na Abel Chimwejo toka katika group la Wapenda Soka ( Kandanda) katika mtandao wa facebook <<<<<<<<<
                                          Abel Chimwejo

No comments

Powered by Blogger.