THE GUNNING MACHINE
ARSENE WENGER NA MAAJABU YAKE ARSENAL.
Wengi watakua wanashangaa timua timua ya makocha ktk vilabu mbalimbali duniani,lakini tunapaswa kuelewa kuwa kupata kocha wa kudumu nae ni kazi ngumu sana.
Nilisoma 'Miwani pana ya Edo' akipendekeza Ole Gunnar Solkjaer arithi mikoba ya SAF pale OT nadhani Edo anahisi Solkjaer anaweza kudumu sana OT tofauti na Kina Mourinho au Pep.
Hii inanikumbusha watu kama Stewart Houston na Bruce Rioch walivotimuliwa ktk kipindi kifupi pale Arsenal.George Graham akafuatia kabla ya kushindwa kuleta jipya pale.watu wakampendekeza Johan Cruyff kuja kuiokoa Arsenal.Lakini David Dein wkt ule akaamua kufanya maajabu.Maajabu ya kumleta mtu wa ajabu kwenye soka la England.
Tony Adams aliyekuwa nahodha wa arsenal wakati huo ananukuliwa akisema,"nilijiuliza kwamba mtu huyu anajua nini ktk soka,mtu mwembamba,mrefu,anavaa miwani.kwa haraka haraka utasema ni mwalimu wa shule".
Huyo ndiyo Arsene Wenger ambaye mafanikio yake makubwa ni makombe kadhaa aliyoipatia Monaco ya Ufaransa kama kocha.Anafika Arsenal october mwaka 1996 akiwa ni wa kwanza kutoka nje ya UK kuwa kocha wa arsenal.
Ktk msimu huo wa 1996-97 akaiongoza arsenal kumaliza ktk nafasi ya 3 nyuma ya Man utd na Newcastle hvo kupata nafasi ya kushiriki Champions League.
Msimu uliofuata wa 1997-98 mtu huyu anafanya maajabu mengine baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu England ndani ya wiki 8 za mwisho akipunguza pointi 12 za Manchester United hadi kutwaa uingwa akiwa na mechi 2 mkononi.maajabu hayo hayakutosha,kwani alitwaa kombe la FA wiki 2 b'dae na hvo kutia alama jina lake ktk ulimwengu wa soka kwa vikombe viwili ktk msimu wa kwanza.
Moja kwa moja mtu huyu akawa amekubalika ktk club,hivo akapata nafasi sasa ya kubadili mfumo wa maisha ya Arsenal ndani na nje ya uwanja,akianza na mifumo ya uchezaji mpaka ulaji wa vyakula.
Wenger anasema mwenyewe,"soka inapaswa kumburudisha shabiki na mchezaji mwenyewe".
Anakumbukwa jinsi alivombadili Tony Adams aliyekua hatarini kutopea kwenye ulevi wa pombe,mpaka kuwa mfano wa kuigwa na mabeki wengi ulimwenguni.akiuongoza ukuta wa kina Steve Bould,Nigel Winterburn,Lee Dixon na Martini Keown kupata clean sheet katika michezo 8 kuanzia Januari hadi Machi 1998.
Alifanya usajili pia kwa kuwanunua wachezaji kama Emmanuel Pettit,Patrick Vieira na Marc Overmas lkn akawapa nafasi David Seaman na Denis Bergkamp kuonesha walichonacho.
Msimu wa 1998-99 arsenal walipoteza ubingwa wao kwa Man UTD kwa point 1 tu siku ya mwisho.pia walifungwa na Man UTD ktk nusu fainali ya kombe la FA kwa goli la Ryan Giggs.
Mwaka 2000,arsenal walifika fainali ya UEFA cup lkn wakapoteza kwa penalti mbele ya Galatasaray.
2001 wakafungwa na Livepool ktk fainali ya kombe la FA ktk mechi ambayo Arsenal walipiga mpira wa hali ya juu sana ila bahati haikua upande wao. Ktk miaka yote hii arsenal walikua wakikaribia vikombe lakini walivikosa ktk dk za mwisho.
Njaa ya makombe kama ilivo hv sasa ikawakimbiza Emanuel Petit na Overmas kwenda Barcelona.ikaonekana kama nyakati za Arsene Wenger pale Highbury zinakaribia kuisha lakini cha kushangaza akasaini mkataba mwingine July 2001.
Akafanya maajabu mengine ya kumsajili bure Sol Campbell kutoka Spurs pamoja na Giovani Van Bronckhorst wakati ambao Fredrick Ljungberg,Thierry Henry na Robert Pires walionunulia misimu iliyopita wakiwa na viwango duni wakiwa tayari sasa kujitambulisha rasmi ktk kikosi cha kwanza.
Tazama kikosi hicho kilivomtosha mtu huyu kufanya maajabu mengine ktk soka kwenye msimu wa 2001-02.akatwaa kombe la ligi kuu na kombe la FA kwa kuwafunga Chelsea 2-0 ktk fainali.
Ktk msimu huo arsenal waliweka rekodi ya ajabu ya kufunga goli ktk kila mechi huku wakipata matokeo ktk mechi zote za ugenini yaani W:13,D:5
Msimu wa 2002-03 Wenger aliendeleza maajabu kwa kuikamata record ya Man utd ya mechi 29 bila kufungwa huku performance ya Arsenal ikiwa ya kuvutia kuliko kawaida kiasi cha Wenger kusema kuwa timu yake inaweza kumaliza msimu bila kufungwa lakini ajabu na kweli,arsenal wakafungwa na Everton.wakiwa wamecheza bila kupoteza kwa miezi 10.
Man Utd wakafanikiwa kupangua pointi 8 za arsenal na kutwaa ubingwa wa ligi.lakini Arsenal hawakutoka kapa msimu huo,waliambulia kutetea kombe la FA wakiwa timu ya kwanza kufanya hvo ktk kipindi cha miaka 30...
Itaendelea hapa hapa...NDIYO TUNAANZA THE GUNNING MACHINE KWA STYLE HII
.
Usikose kuungana nami Richard Leonce ChardBoy (Kutoka katika Wapenda Soka group) kwa story tamu sana kuhusu club ya Arsenal kwenye blog yako hii ya mashabiki wa soka.karibu sana

No comments