AMEANDIKA: Storming Fo (SIB)
MABINGWA ULAYA Chelsea wanyukwa 3-0 na Juve, TAJI hatarini
BARCA, SHAKHTAR, BAYERN, VALENCIA ZAFUZU!
Mabingwa watetezi wa Ulaya, Chelsea, wapo hatarini kulibwaga chini Taji lao baada ya kunyukwa Bao 3-0 na Juventus huko Mjini Turin kwenye Mechi ya Kundi E la UEFA CHAMPIONZ LIGI na sasa hatima yao haipo tena mikononi mwao maana katika Mechi za mwisho za Kundi lao ikiwa Mechi kati ya Shakhtar Donetsk, ambao tayari wamefuzu, na Juventus itakuwa sare tu basi wao hata wawafunge Nordsjaelland Bao Milioni moja wako nje.
Katika Mechi nyingine zilizochezwa Jumanne Barcelona, Shakhtar Donetsk, Bayern Munich na Valencia zimefanikiwa kufuzu na kuungana na Manchester United, Malaga na FC Porto ambao walikuwa tayari wamefuzu kabla MECHI DEI 5 kuanza.
Mitanange mingine ya Makundi A hadi D inaendelea Jumatano Usiku

No comments