KUTINYU AITWA TIMU YA TAIFA YA ZIMBABWE

Kiungo mpya wa timu ya Azam FC, Tafadzwa Kutinyu ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe kwa ajili ya michuano ya COSAFA.

Kutinyu ametambulishwa jana Meneja wa matajiri hao wa jiji, Philip Alando baada ya kusaini nao mkataba wa mwaka mmoja akitokea klabu ya Singida United.

Msemaji wa klabu hiyo Jaffer Idd amesema kiungo huyo alikuwa atambulishwe leo mbele ya Waandishi wa Habari lakini baada ya kuondoka kuelekea Zimbabwe kwa majukumu ya timu ya taifa jambo hilo litafanyika baadae.

"Kutinyu ameondoka jana kuelekea Zimbabwe kwa ajili ya michuano ya COSAFA na ataraejea mara tu baada ya kumalizika michuano hiyo," alisema Jaffer.

Kutinyu ataanza kuonekana akiwa na jezi ya Azam katika michuano ya Kagame Cecafa Cup inayotarajia kufanyika hapa Dar es Salaam kuanzia Juni 29.

No comments

Powered by Blogger.