KICHUYA, MZAMIRU WAJITIA PINGU SIMBA, KUELEKEA KENYA LEO.

Taarifa za uhakika ambazo tumepata ni kwamba tayari Simba wamefanikiwa kuwasainisha mikataba mipya nyota wao wawili waliokua wamemaliza mikataba yao ya kuitumikia klabu hiyo ambao ni Shiza Kichuya na Mzamiru Yasin.

Nyota hao walisalia nchini kuendelea na mazungumzo ya kuongeza mikataba wakati wenzao wakielekea nchini Kenya kwa ajili ya michuano ya Sport Pesa Super Cup inayoanza leo nchini humo.

Inaelezwa kuwa Kichuya amesainishwa mkataba wa miaka mitatu kwa sababu upo uwezekano wa yeye kuuzwa wakati wowote na Mzamiru amesaini mkartaba wa kuitumikia Simba kwa miaka miwili.

Baada ya taratibu hizo kukamilika, Kichuya, Mzamiru pamoja na mchezaji mwingine ambaye bado hajafahamika wataondoka nchini leo na kuungana na wenzao nchini Kenya kuongeza nguvu tayari kwa michuano ya Sport Pesa.

No comments

Powered by Blogger.