YANGA YAFUNGA MSIMU KWA KICHAPO TOKA AZAM

Waliokuwa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara timu Yanga leo imekamilisha msimu wa ligi hiyo uliokuwa mgumu kwao kwa kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Azam FC mtanange uliopigwa uwanja wa Taifa.

Azam walipata bao la kwanza mapema dakika ya tatu ya kupitia kwa Yahya Zayd baada ya kuwazidi mbio walinzi wa Yanga na kupiga mpira kwa ufundi na kumpoteza mlinda mlango kabisa Ramadhan Kabwili.

Mchezo uliendelea kwa kasi huku Yanga wakionekana kuzidiwa na mara  kadhaa hali iliyoonekana kuwanyong'onyeza mashabiki wao ambao leo walionekana wakiwa na mabango mengi yenye ujumbe mbalimbali kuhusu viongozi wao.

Baada kuanza kipindi cha pili mlinzi wa Azam, Abdalah Kheri alijifunga katika jitihada za kuokoa mpira wa adhabu uliopigwa na Hassan Kessy na kuwasawazishia Yanga.

Mabao mengine ya Azam yalifungwa na Shaban Iddi na Salum Abubakar 'Sure Boy' naw kuwahakikishia kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.

Baada ya mchezo huo nahodha wa Yanga Thabani Kamusoko alikiri kwamba hawakucheza vizuri na walizidiwa kila idara hivyo watajipanga kwa msimu ujao.

No comments

Powered by Blogger.