YANGA YAENDELEA KUGAWA POINTI LIGI KUU TANZANIA BARA.


Waliokuwa Mabingwa wa ligi kuu Soka Tanzania bara na wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya kimataifa Yanga wameendelea kugawa pointi katika mechi zake za ligi hiyo zilizobaki baada ya kupoteza Kwa bao 1-0 ugenini.

Yanga iliyokuwa mjini Shinyanga kucheza na Mwadui ilijikuta ikipoteza mchezo wake wa tatu mfululizo katika michuano hiyo baada ya kupoteza pia dhidi ya Tanzania Prisons na Mtibwa katika mechi zilizopita.

Boa pekee lililowanyima ushindi Leo lilifungwa na Awesu Ally dakika ya 19
Kuwafanya Yanga kubakia na pointi zao 48 katika nafasi ya tatu huku Mwadui wakipanda mpaka nafasi ya 10 Na kufikisha pointi 33

No comments

Powered by Blogger.