HATIMAYE: SIMBA YAPOTEZA MECHI MBELE YA JPM
Mabingwa wa ligi kuu Soka Tanzania bara wekundu wa Msimbazi Simba Leo wamekubali kichapo Kwa Mara ya kwanza msimu huu baada ya kufungwa bao 1-0 na wageni Kagera Sugar.
Umati mkubwa wa mashabiki wa timu hiyo walioujaza uwanja wa Taifa jijini huku Mgeni Rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. John Pombe Magufuli walishuhudia Simba ikifungwa bao hilo pekee dakika ya 87 ya mchezo na mchezaji wa zamani wa Wekundu hao Christopher Edward.
Simba ambao waliingia Katika mechi ya Leo mahususi kwaajili ya kukabidhiwa KOMBE LA ubingwa wa ligi kuu msimu huu walishindwa kusawazisha katika mechi hiyo baada ya kupata penati dakika tano za nyongeza na Emmanuel Okwi kushindwa kukwamisha mpira huo kimiani kipa wa Kagera Juma Kaseja akidaka penati hiyo.
Sambamba na kukabidhiwa Kombe Simba Leo pia Rais Magufuli alipokea kombe la Ubingwa wa mashindano ya CECAFA Kwa vijana wa chini ya miaka 17 pamoja na kombe la nafasi ya pili la watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

No comments